Friday, December 13, 2024

Siri ya Saudi Arabia Kuteuliwa Kuandaa Kombe la Dunia Mwaka 2034

Siri ya Saudi Arabia Kuteuliwa Kuandaa Kombe la Dunia Mwaka 2034


Oktoba 2023 rasmi FIFA ilifungua dirisha la maombi ya kuandaa WORLD CUP 2030 na 2034

Ili kuhakikisha wanatenda haki kwa bara linalopewa kuandaa WORLD CUP. FIFA wana sheria yao inayoitwa PRINCIPLE OF CONFEDERATION ROTATION.

Hii ni sheria ambayo inahakikisha kunakua na mazingira bora kuelekea maandalizi au kuchaguliwa kwa bara kupewa nafasi ya kuandaa World Cup. Kila bara linaruhusiwa kuandaa World Cup kila baada ya miaka 

Chini ya PRINCIPLE OF CONFEDERATION ROTATION, Fifa ina mabara 6 ambayo ni UEFA, CONMEBOL (South America), Asia (AFC), Africa (CAF), Oceania (OFC) & CONCACAF (Amerika ya kati na kaskazini)

Kombe la dunia linalofuata 2026 litaandaliwa na bara la CONCACAF ( Mexico, Canada & USA). So katika yale mabara 6, kimsingi hapo yanakua yamebakia mabara 5 kuelekea maandalizi ya World Cup 2030 na 2034

Sasa imekuaje Saudi Arabia ambayo ipo bara la ASIA amepata hii nafasi ya kuandaa World Cup 2034, wakati 2022 tayari Qatar walishaandaa, na kwa utaratibu ASIA ilitakiwa nafasi yao waipate tena mwaka 2042?

Sasa nisikilize kwa makini nikuelekeze

Saudi Arabia ambayo ipo ASIA imepata nafasi ya kuandaa tena World Cup 2034 japo haikua nafasi yao kwa sababu zifuatazo;

Kombe la dunia la 2030 litafanyika kwa kuhusisha mabara matatu kwa pamoja ( CAF, UEFA na CONMEBOL) kwa sababu FIFA itakua inatimiza miaka 100 ya kuandaa kombe la dunia.

So maana yake ni kwamba kwa kuwa 2030 kombe la dunia limeandaliwa kwa mabara matatu kwa mpigo hvyo kwa mwaka 2034 nafasi ya kuandaa World Cup inabakia kwa mabara ya Oceania na Asia.

Bara la Oceania ambalo kimsingi linahusisha nchi kama New Zealand na Australia, ila Australia ilishajitoa Oceania na ikajiunga na bara la Asia tangu mwaka 2006

Fifa ikasema nchi kama New zealand na wenzake hawana uwezo kuandaa World Cup. So bara la Oceania likawa limechinjiwa baharini kinamna hiyo

So nafasi ikabaki tena kwa Asia ambayo sasa nchi kama Indonesia, Vietnam, Thailand na Australia wote hao wakaamua kwa pamoja kumuunga mkono Saudi Arabia.

Saudi Arabia akabakia yeye pekee yake ambae alipeleka bid Oktoba mwaka jana na hvyo alishinda nafasi ya kuandaa kombe la dunia kwa mwaka 2034

Shaffih Dauda

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...