"Kwa kweli, kucheza nyumbani ni faida kubwa kwetu. Tutakuwa na programu za mazoezi kwa siku chache zilizopo mbele yetu ili kuwa tayari kwa mchezo huu. Nitahakikisha mpango wetu wa kimbinu ni tofauti na ule tulioutumia kule Algeria."
"Nidhamu ya kulinda itakuwa sehemu muhimu ya mchezo wetu, lakini tunahitaji kuwa na mashambulizi ya haraka na kuzuia makosa tuliyofanya kwenye mchezo wa awali, Lengo ni kuhakikisha kuwa tunapata matokeo mazuri na kuweka hesabu zetu sawa katika michuano hii ya CAF."
.