Saturday, July 11, 2020

Magufuli Ampa Makavu Kigogo wa CCM Alielalamikia Wapinzani Wanaohamia CCM Kupewa Nafasi



Katika Mkutano Mkuu wa CCM leo July 10, 2020 Rais Magufuli amemkosoa Mjumbe wa CCM alietoa lawama juu ya Wapinzania wanaohamia CCM kutoka Upinzani kupewa nafasi za kugombea na Wana-CCM kuachwa.

"Chama hiki ni cha watu, kina misingi yake, tunao watu waliokuwa Upinzania leo wapo Kamati Kuu akiwemo Makongoro, Wasira, inawezekana anaekuja mna wasiwasi atawashinda" Magufuli


Msinichagulie shikamoo mtanipa tabu, mchagueni Hussen Mwinyi namzidi umri- JPM


"Hussein Mwinyi namzidi umri, kanichagulieni huyu na mimi nitajisikia raha, sio mkanichagulie Mtu ambaye nikifika Zanzibar nitamuambia Shikamoo, inachosha, msinichagulie shikamoo mtanipa tabu, nichagulieni huyu nitampa nguvu zote kwakuwa ni Mdogo wangu"-JPM

Nahisi Mpenzi wa Kinyamwezi Kanifunga, Kila Nikitongoza Mwanamke Mwingine Nakataliwa

Ndugu zangu aisee nimekamatika najuta kukatongoza katoto ka kinyamwezi. Yapata mwaka mmoja tangu niwe kwenye mahusiano na huyu mtoto wa kinyamwezi. Nimekutana nae college namaliza mwaka wa tatu clinical officer na yeye anaanza kusoma Medical Doctor.

Mimi najikuta nataka nimpotezee lakini kila nikitongoza naambiwa ninae mtu, wewe ni muongo na neno linaloniumiza zaidi la "wewe unaye mtu." na cha ajabu hawajui chochote kuhusu mimi wala kama nina mtu

Na mtoto kaniganda mara anasema nikimaliza tu chuo unanioa. Aisee sijui nifanyeje kila nikitongoza nakataliwa na haikuwa kawaida yangu, kwa wiki nilikuwa nakula wanawake Wanne... Mpaka leo nimetimiza idadi ya wadada kumi wakichaga wananikataa. toka niwe naye

Naomba ushauri please

Katibu Tawala (DAS) Handeni Afariki Dunia Katika Ajali Mbaya....Watatu Wanusurika Akiwemo Mbunge

Aliyekuwa Katibu Tawala (DAS) Boniface Maiga Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga amepoteza maisha katika ajali huku watu watatu wakijeruhiwa akiwemo Mbunge wa Jmbo la Handeni Omary Kigoda ambaye amevunjika vidole viwili vya mkono wa kulia wakati wakielekea kwenye mkutano mkuu jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa yake dereva wa gari la Mbunge wa Handeni Omary Kigoda, Peter Mganga amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa saba usiku katika eneo la Vikonji Dodoma.

Amesema chanzo cha ajali hiyo imetokana na mwendokasi aliokuwa dereva wa basi baada ya kulipita sehemu yenye kona kitendo ambacho si sahihi.

Dereva huyo wa mbunge amesema baada ya dereva wa basi kulipita katika eneo hilo lenye kona kali alimuwashia taa ili aweze kupunguza mwendo gari ila dereva wa basi hilo hakupunguza spidi na ndipo wakavana uso kwa uso.

"Katika ajali hii dereva na kondakta wa basi wote wamefariki nilijaribu kumwashia taa nyingi ili apunguze spidi lakini cha kushangaza kama hajaziona ilibidi sisi tupaki pembeni ndipo mwendo aliokuwa nao ililazimu kulivaa gari letu hasa upande wa kulia aliokuwa amekaa mheshimiwa mbunge na DAS wetu aliyefariki,"alisema Mganga.

Amesema mara baada ya ajali hiyo DAS alipoteza maisha hapo hapo huku wao wakikimbizwa katika hospitaliti ya Chamwino kwajili ya matibabu ambapo Mbunge alilazimika kufanyiwa upasuaji wa vidole hivyo wakahamishiwa katika hospitali ya Mkoa Dodoma (General Hospital).

Mganga amesema baada ya kupata matibabu wawili waliruhusiwa kutoka hospitalini hapo saa kumi na moja alfajiri huku mbunge Kigoda akibaki kuendelea na matibabu ya vidole alivyoumia.

Amesema katika gari hiyo ya mbunge Kigoda walikuwa watu wanne akiwemo yeye Dereva wa Mbunge Peter Mganga, Mbunge Omary Kigoda, Mbelwa Saidy ambaye ni ndugu yao pamoja na Boniface Maiga (DAS) aliyepoteza maisha na kueleza kuwa mwili wa marehemu upo katika hospitali hiyo ya Mkoa.

Credit:Majira


Friday, July 10, 2020

Msafara wa Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Ruge mkoani Mara Wazuiliwa kwa Kupigwa Mabomu



Msafara wa aliyekuwa mbunge wa viti maalum (Chadema), Catherine Ruge mkoani Mara amezuiliwa kwa kupigwa mabomu na jeshi la polisi.

Mabomu hayo yalianza kurindima wakati akirejesha fomu ya kuwania Ubunge jimbo la Serengeti kupitia Chadema.

Licha ya kupigwa mabomu ya machozi Catherine Ruge alifanikiwa kurejesha fomu yake ya kugombea ubunge.

Ruge awajibu polisi "Polisi kaeni pembeni tuacheni huu mziki na CCM," aliandika katika ukurasa wake wa twitter.



Source

Picha : EMMANUEL NTOBI, SALOME MAKAMBA WARUDISHA KWA KISHINDO FOMU KUGOMBEA UBUNGE SHINYANGA MJINI KUPITIA CHADEMA

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Emmanuel Ntobi (aliyekuwa diwani wa Kata ya Ngokolo na Mwenyekiti CHADEMA mkoa wa Shinyanga) na Salome Makamba (aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum) wamerudisha kwa kishindo Fomu za kuomba kugombea nafasi ya ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini leo Ijumaa Julai 10,2020.

Makada hao wa CHADEMA wamewasili katika Ofisi za CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini wakisindikizwa na misafara ya wafuasi wa CHADEMA waliokuwa wanaendesha magari na pikipiki huku wakiwa wamebeba bendera za chama hicho sambamba na matarumbeta ya hapa na pale.

Mara baada ya kuwasili katika ofisi za CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini, watia nao walikabidhi fomu za kuomba ridhaa ya kuchaguliwa na chama chao kugombea ubunge jimbo la Shinyanga Mjini kisha wakapata nafasi ya kuelezea mbele ya wanachama wa CHADEMA malengo yao ya kuomba chama kiwapitishe kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.

Katibu wa CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini Joseph Ndatala amesema zoezi la kurudisha fomu kwa wanachama wa CHADEMA waliotia nia kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini ni leo Ijumaa Julai 10 saa 10 kamili jioni.

"Zoezi linalofanyika leo ni kupokea fomu za wanachama wetu waliojitokeza kuomba kugombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Shinyanga ambapo majina ya waliojitokeza yatajadiliwa katika mkutano wa chama na atapatikana mgombea mmoja",amesema Ndatala.

Ameyataja majina ya wanachama wa CHADEMA waliochukua fomu kugombea ubunge katika Jimbo la Shinyanga Mjini kuwa ni Emmanuel Ntobi, Samson Ng'wagi, Mchungaji Jilala Fumbuka, Nicholaus Luhende, Hassan Salim pamoja na Zainab Kheri Zena Gulam wanaowania nafasi ya Ubunge Viti Maalum.

Ndatala amesema zoezi la wanachama wa CHADEMA kurudisha fomu za kugombea ubunge jimbo la Shinyanga Mjini limeenda sambamba na kumdhamini Tundu Lissu kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mwanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Emmanuel Ntobi (aliyekuwa diwani wa Kata ya Ngokolo na Mwenyekiti CHADEMA mkoa wa Shinyanga) akiwasili katika ofisi za CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini leo Ijumaa Julai 10,2020 wakati akirudisha fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge jimbo la Shinyanga Mjini. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katibu wa CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini Joseph Ndatala  akizungumza wakati wa kupokea fomu za wanachama wa CHADEMA waliojitokeza kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Katibu wa CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini Joseph Ndatala  akizungumza wakati wa kupokea fomu za wanachama wa CHADEMA waliojitokeza kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Katibu wa CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini Joseph Ndatala  akipokea fomu ya Emmanuel Ntobi kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Katibu wa CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini Joseph Ndatala  akipokea fomu ya Emmanuel Ntobi kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Katibu wa CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini Joseph Ndatala  akionesha fomu ya Emmanuel Ntobi kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Mtia nia kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CHADEMA  Emmanuel Ntobi akieleza sababu zilizomsukuma kuomba chama chake kimpe ridhaa ya kugombea  Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Mtia nia kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CHADEMA  Emmanuel Ntobi akieleza sababu zilizomsukuma kuomba  chama chake kimpe ridhaa ya kugombea  Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Mtia nia kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CHADEMA  Emmanuel Ntobi akieleza sababu zilizomsukuma kuomba chama chake kimpe ridhaa ya kugombea  Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Mtia nia kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CHADEMA  Emmanuel Ntobi akieleza sababu zilizomsukuma kuomba chama chake kimpe ridhaa ya kugombea  Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Katibu wa CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini Joseph Ndatala  akipokea fomu ya Samson Ng'wagi kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Katibu wa CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini Joseph Ndatala  akipokea fomu ya Samson Ng'wagi kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Mtia nia kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CHADEMA  Samson Ng'wagi akieleza sababu zilizomsukuma kuomba chama chake kimpe ridhaa ya kugombea  Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Mtia nia kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CHADEMA  Salome Makamba akiwasili katika ofisi za CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini kurudisha fomu ya  kuomba chama chake kimpe ridhaa ya kugombea  Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Katibu wa CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini Joseph Ndatala  akipokea fomu ya Salome Makamba kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Katibu wa CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini Joseph Ndatala  akipokea fomu ya Salome Makamba kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Mtia nia kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CHADEMA  Salome Makamba akieleza sababu zilizomsukuma kuomba chama chake kimpe ridhaa ya kugombea  Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Mtia nia kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CHADEMA  Salome Makamba akieleza sababu zilizomsukuma kuomba chama chake kimpe ridhaa ya kugombea  Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Katibu wa CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini Joseph Ndatala  akipokea fomu ya Zena Gulam kuwania nafasi ya Ubunge Viti Maalum Jimbo la Shinyanga Mjini.
Mtia nia kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CHADEMA  Zena Gulam akieleza sababu zilizomsukuma kugombea  Ubunge Viti Maalum Jimbo la Shinyanga Mjini.
Awali Makada wa CHADEMA wakiendelea na shamra shamra nje ya ofisi za CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini.
Awali Makada wa CHADEMA wakiendelea na shamra shamra nje ya ofisi za CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini.
Msanii Mussa Jumanne akitoa burudani wakati makada wa CHADEMA wakirudisha  fomu kuomba kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Msanii Mussa Jumanne akitoa burudani wakati makada wa CHADEMA wakirudisha  fomu kuomba kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Thursday, July 9, 2020

Rosa Ree Drops Maasai Bars in New Song ‘Kanyor Aleng’



Tanzanian rapper Rosa Ree has dropped a new track dubbed 'Kanyor Aleng'.

According to her caption, 'Kanyor Aleng' means 'I love you' in Maasai. In the new release, she explains what love means to her.

 "I'm trying to find the right words to address you by, is this a love song or a lullaby, tears all over my face and I don't know why, am I happy am I sad am I happy tell me why am crying, without you I'm on a road but don't know where to go…." The song's lyrics read in part.
Despite some sections of the song being in Maasai, it is still on point and very appealing due to the amazing beats.

Listening to the first part of the new jam, one may confuse Rosa Ree for one of top American female rappers due to her maturity in rapping.

The audio was produced by Ibra Jacko and the lyric video done by bang.

'Kanyor Aleng' is proof that Rosa Ree is one of the best female rappers in the East African region.
In this jam, she has shown us that she is dynamic and can try new stuff without much struggle.

Wednesday, July 8, 2020

Dawa za Kuokoa Maisha ya Wagonjwa wa Corona Zauzwa kwa Magendo India



Uchunguzi wa BBC umebaini kuwa aina mbili za dawa ambazo zilitumika kutibu wagonjwa wa corona nchini India - remdesivir na tocilizumab - zimekuwa zikiuzwa katika soko la magendo kwa bei ya juu ndio maana kuna upungufu mkubwa sana wa dawa hizo.Mwandishi wa BBC, Pandey anaripoti kutoka mji mkuu wa India Delhi.

Mjomba wake Abhinav Sharma alikuwa na homa kali na alikuwa anapata tabu kupumua wakati alipolazwa hospitalini huko Delhi.

Alikutwa na virusi vya corona na madaktari waliiambia familia yake itafute dawa aina ya remdesivir - dawa ambayo imeruhusiwa kwa ajili ya matibabu ya corona wakati wa dharura nchini India ",hii ikiwa ina maana kuwa madaktari wanaweza kutoa ruhusa ya matumizi ya dawa hizo kwa kutokana na sababu maalum.

Lakini upatikanaji wa dawa hiyo umeonekana kuwa jambo ambalo haliwezekani - dawa ya 'remdesivir' imeadimika na haipatikani kokote.

Bwana Sharma alihangaika kuwapigia watu kumsaidia kupata dawa ya kumsaidia mjomba wake ambaye hali yake ilikuwa inazidi kuwa mbaya kila saa.

"Nilikuwa na machozi machoni mwangu. Mjomba wangu alikuwa anapambana na maisha yake na nilikuwa nahangaika kupata dawa ambayo ingeweza kuokoa maisha yake," alisema.

"Baada ya kupiga simu kadhaa, nililipa mara saba ya gharama halisi ya dawa nilikuwa radhi kulipia gharama yoyote ile kwa kweli, lakini nawaonea huruma watu wale ambao hawana uwezo wa kununua kwa gharama hiyo," alisema.

Changamoto aliyokabiliana nayo Bwana Sharma, inazikabili familia nyingi sana mjini Delhi, ambapo watu wengi huwa wanahangaika na kufanya lolote ili kuokoa maisha ya wapendwa wao.

Baadhi wanasema huwa wanalazimika kulipa gharama kubwa sana kwa ajili ya dawa hiyo - wengi huwa wanaishia kwenye soko la zamani la dawa la mjini Delhi.

BBC iliweza kuwapata watu wanaofanyakazi katika soko ambao wanaweza kusaidia upatikanaji wa dawa lakini kwa bei sahihi.

"Ninaweza kukuletea chupa tatu za dawa - lakini moja itakugharimu rupee 30,000 sawa na dola $401 au £321 na unahitaji kuja haraka ," alisema mwanaume mmoja ambaye alidai kuwa anafanya biashara ya dawa. ".

Bei rasmi kwa kila chupa ni rupee 5,400 na mgonjwa anakuwa anahitaji kunywa dozi tano au sita. Mwanaume mwingine alinukuliwa kununua dawa moja kwa rupee 38,000.

Uhitaji wa dawa ya remdesivir unaongezeka kutokana na ukweli kuwa dawa hiyo ina uwezo wa kuondoa dalili za corona ndani siku 15 na kwa mgonjwa ambaye yuko katika hali ya mahututi inaweza kusaidia katika siku 11 katika majaribio ya hospitali duniani kote. 

Wataalamu wameonya kuwa hakuna uhakika katika hilo. 

Lakini hakuna uthibitisho wa dawa yeyote ambayo imethibitishwa kutumika na madaktari wanazidi kuwaandikia watu dawa hiyo nchini India, na hivyo kufanya dawa hiyo kuwa na uhitaji mkubwa mjini Delhi na miji mingine ya India. 

BBC imeweza kubaini hali hiyohiyo kwa familia zenye wagonjwa wa Covid mjini Delhi na miji ya jirani kuwa wanalipa gharama za ziada ili kupata dawa hiyo ya remdesivir.

Azam FC yanyakua pointi tatu mbele ya Mwadui FC

Azam FC imefanikiwa kuchukua pointi tatu muhimu baada ya kuipiga Mwadui FC 1-0 kwa goli pekee la Andrew Simchimba.

FT: Azam FC 1-0 Mwadui FC.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...