Wednesday, July 8, 2020

Dawa za Kuokoa Maisha ya Wagonjwa wa Corona Zauzwa kwa Magendo India



Uchunguzi wa BBC umebaini kuwa aina mbili za dawa ambazo zilitumika kutibu wagonjwa wa corona nchini India - remdesivir na tocilizumab - zimekuwa zikiuzwa katika soko la magendo kwa bei ya juu ndio maana kuna upungufu mkubwa sana wa dawa hizo.Mwandishi wa BBC, Pandey anaripoti kutoka mji mkuu wa India Delhi.

Mjomba wake Abhinav Sharma alikuwa na homa kali na alikuwa anapata tabu kupumua wakati alipolazwa hospitalini huko Delhi.

Alikutwa na virusi vya corona na madaktari waliiambia familia yake itafute dawa aina ya remdesivir - dawa ambayo imeruhusiwa kwa ajili ya matibabu ya corona wakati wa dharura nchini India ",hii ikiwa ina maana kuwa madaktari wanaweza kutoa ruhusa ya matumizi ya dawa hizo kwa kutokana na sababu maalum.

Lakini upatikanaji wa dawa hiyo umeonekana kuwa jambo ambalo haliwezekani - dawa ya 'remdesivir' imeadimika na haipatikani kokote.

Bwana Sharma alihangaika kuwapigia watu kumsaidia kupata dawa ya kumsaidia mjomba wake ambaye hali yake ilikuwa inazidi kuwa mbaya kila saa.

"Nilikuwa na machozi machoni mwangu. Mjomba wangu alikuwa anapambana na maisha yake na nilikuwa nahangaika kupata dawa ambayo ingeweza kuokoa maisha yake," alisema.

"Baada ya kupiga simu kadhaa, nililipa mara saba ya gharama halisi ya dawa nilikuwa radhi kulipia gharama yoyote ile kwa kweli, lakini nawaonea huruma watu wale ambao hawana uwezo wa kununua kwa gharama hiyo," alisema.

Changamoto aliyokabiliana nayo Bwana Sharma, inazikabili familia nyingi sana mjini Delhi, ambapo watu wengi huwa wanahangaika na kufanya lolote ili kuokoa maisha ya wapendwa wao.

Baadhi wanasema huwa wanalazimika kulipa gharama kubwa sana kwa ajili ya dawa hiyo - wengi huwa wanaishia kwenye soko la zamani la dawa la mjini Delhi.

BBC iliweza kuwapata watu wanaofanyakazi katika soko ambao wanaweza kusaidia upatikanaji wa dawa lakini kwa bei sahihi.

"Ninaweza kukuletea chupa tatu za dawa - lakini moja itakugharimu rupee 30,000 sawa na dola $401 au £321 na unahitaji kuja haraka ," alisema mwanaume mmoja ambaye alidai kuwa anafanya biashara ya dawa. ".

Bei rasmi kwa kila chupa ni rupee 5,400 na mgonjwa anakuwa anahitaji kunywa dozi tano au sita. Mwanaume mwingine alinukuliwa kununua dawa moja kwa rupee 38,000.

Uhitaji wa dawa ya remdesivir unaongezeka kutokana na ukweli kuwa dawa hiyo ina uwezo wa kuondoa dalili za corona ndani siku 15 na kwa mgonjwa ambaye yuko katika hali ya mahututi inaweza kusaidia katika siku 11 katika majaribio ya hospitali duniani kote. 

Wataalamu wameonya kuwa hakuna uhakika katika hilo. 

Lakini hakuna uthibitisho wa dawa yeyote ambayo imethibitishwa kutumika na madaktari wanazidi kuwaandikia watu dawa hiyo nchini India, na hivyo kufanya dawa hiyo kuwa na uhitaji mkubwa mjini Delhi na miji mingine ya India. 

BBC imeweza kubaini hali hiyohiyo kwa familia zenye wagonjwa wa Covid mjini Delhi na miji ya jirani kuwa wanalipa gharama za ziada ili kupata dawa hiyo ya remdesivir.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...