Monday, September 10, 2018

BREAKING: Mahakama Kuu yatupilia mbali maombi ya Serikali


Mahakama Kuu Kanda ya Iringa imetupilia mbali mapingamizi ya Wakili wa Serikali yaliyokuwa yanapinga Mahakama hiyo kusikiliza maombi ya kuondolewa amri ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) inayozitaka baadhi ya  kampuni zilizokuwa zikionyesha chaneli za ndani kuondolewa kwenye ving'amuzi vyao.

POLISI SHINYANGA WAUA MAJAMBAZI WANAODAIWA KUVAMIA DUKA LA DAWA BARIDI LYABUKANDE

Wanaume wawili wanaodaiwa kuwa ni majambazi wanaotuhumiwa kuvamia duka la dawa baridi katika kijiji cha Lyabukande halmashauri ya Shinyanga (Vijijini) wamefariki dunia baada ya kupigwa risasi na polisi baada ya majibizano ya risasi.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule tukio hilo limetokea jana Septemba 9,2018 saa tano na nusu usiku katika eneo la kichaka cha kata ya Mwawaza manispaa ya Shinyanga.

Aliwataja watu hao kuwa ni Juma Shija Elewa(39) mkazi wa Kitangili na Joseph Ndugali Tall (34) mkazi wa Sikonge mkoani Tabora ambao walijeruhiwa kwa kupigwa risasi na kufariki dunia wakiwa jiani kuelekea hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.

"Chanzo cha tukio ni majambazi hao walipokuwa wanakwenda kuwaonyesha askari vielelezo na eneo ambalo majambazi wenzao wamejificha na baada ya kufika eneo hilo kukatokea majibizano ya risasi toka kwa majambazi waliokuwa wamejificha ndipo marehemu hao wakajeruhiwa kwa risasi",alieleza Kamanda Haule.

"Kwenye eneo la tukio kulipatikana silaha bastola isiyokuwa na namba ikiwa na risasi nne ndani ya magazine moja,vibuyu na vocha mbalimbali za mitandao ya simu na baadhi ya vocha zilipatikana nyumbani kwa Juma Shija Elewa baada kupekuliwa ambazo zote hizo ziliporwa kwenye duka la dawa baridi eneo la Lyabukande tarehe 6.9.2018",aliongeza.

Aidha alisema katika operesheni inayoendelea kwa kushirikiana na askari wa Mwanza,Septemba 9,2018 majira ya saa nane mchana eneo la Nyegezi-Mwanza,jambazi aliyefahamika kwa jina moja la Shaban aliwakimbia polisi na kutelekeza gari lenye namba za usajili T.820 AT aina ya Toyota Corona ambalo lilitumika katika tukio la unyang'anyi kijiji cha Lyabukande.

"Bado tunaendelea na msako kuwatafuta na kuwakamata majambazi wengine waliohusika katika majibizano ya risasi,na jambazi Shaban aliyetelekeza gari,miili ya marehemu imehifadhiwa chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga",alieleza Kamanda Haule.

Na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Bastola isiyokuwa na namba ikiwa na risasi nne ndani ya magazine moja na vibuyu walivyokutwa navyo majambazi 
Vocha zilizokutwa eneo la tukio
Gari iliyotelekezwa na jambazi Shaban

VIDEO: "Nilipata shida kidogo, japo nilitumwa na Mama Samia" Waziri Makamba


Tangu niko mdogo kabisa ametulea, ametufundisha na pia ni kiongozi wa kifamilia hivyo nilipata shida kidogo nilipoalikwa kuja hapa niwe mgeni rasmi na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Bin Zuber anipokee.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI......USISAHAU KUSUBSCRIBE

Jux Kuyaanika Maisha ya Vee Kwenye Zaidi.

MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Juma Mussa 'Jux' hivi karibuni ameachia video yake mpya ya Ngoma ya Zaidi ambayo hadi gazeti hili linakwenda mtamboni kwa upande wa Tanzania ilikuwa ni namba tano kwenye ngoma zinazotrendi. Simulizi ya video hiyo ni namna ambavyo Jux alikuwa amezama kwenye penzi zito la mwanadada ambaye alikuwa anasomea sheria na anakwenda mtaani kumtafuta alikomuona kwa mara ya kwanza. Ukiicheki video hii, Jux ni kama ameweka maisha ya mpenzi wake, Vanessa Mdee 'Vee Money' ambaye naye ni mwanasheria wa ngazi ya digrii aliyesomea nchini Kenya kwenye Chuo cha Catholic University of Eastern Africa. Akizungumzua juu ya hilo, Jux alisema: "Wakati ninaandaa namna video itakavyokuwa sikuwaza kuhusu hilo, lakini baadaye ndiye (Vee Money) alifahamu kwamba kwa namna moja au nyingine video hiyo inaendana na ukweli."

The post Jux Kuyaanika Maisha ya Vee Kwenye Zaidi. appeared first on Ghafla!Tanzania.


Source

Sunday, September 9, 2018

Dk Ndugulile awaasa wananchi kutoa taarifa wanapokosa matibabu


Na.Ahmad Mmow, Nachingwea.\
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto ,Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) amewaasa wananchi  kutoa taarifa pale watakapokwenda hospitali na kukosa matibabu kwasababu ya kukosekana dawa.

Ndugulile ametoa rai hiyo jana katika kijiji cha Naipanga,wilaya ya Nachingwea wakati wa kilele cha  kampeni ya kupima kwa hiyari maambukizi ya virusi vya UKIMWI ambayo imepewà na kutambulika kwa  jina la  "Furaha Yangu ".

Aliwahakikishia wananchi hao na wengine wote hapa nchini kwamba serikali ya awamu ya tano haitaki kuona wananchi wakienda kununua dawa madukani hivyo imejipanga kuhakikisha dawa zote zinazotolewa na serikali zinawafikia.

Alisema katika kuhakikisha huduma za afya zinatolewa kwa wananchi Serikali imewapeleka watumishi wa idara ya afya 48 katika wilaya hiyo ili wakatoe huduma kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vilivyopo wilayani humu.

 "Upimaji wa virusi vya  UKIMWI ni mpango wa kitaifa ili kuhakikisha kila Mtanzania anapima na kutambua afya yake, lengo ni  kuwafikia asilimia 90 ya watu walioambukizwa  na kutoa dawa,"alisema DkNdugulile ambae pia ni mbunge wa jimbo la Kigamboni.

Kwa upande wake ,mkuu wa  wilaya Nachingwea, Rukia Muwango alisema zoezi la upimaji afya  katika wilaya hiyo ni endelevu, kwani umuhimu wa wananchi kupima na kutambua afya zao ni mkubwa huku akiweka wazi kwamba maendeleo yatatokana na uimara wa afya za wananchi kwasababu mtaji wa kwanza wa maendeleo na uchumi wa taifa ni afya.

Mkuu huyo wa wilaya alibainisha kwamba kampeni  hiyo ya upimaji kwa hiari inayoendelea wilayani humo ambayo yeye kwa kushirikiana na watalaam wa idara ya afya anaratibu na kusimamia.Tayari wanawake 809 na wanaume 531wamejitokeza na kupimwa.

 "Hadi sasa miongoni mwahao waliopima ni watu saba  tu ndio waliokutwa na maambukizi ya VVU na wameshapata ushauri nasaha na kuanzishiwa dawa za kupunguza makali ya Virusi Vya UKIMWI,"alisema Muwango.

Friday, September 7, 2018

Bright Amkana Mtoto wa Nyoshi

Mwanamuziki wa kizazi kipya nchini,Bright amefunguka na kukanusha kuwa na mahusiano na mtoto wa mwanamuziki wa dansi Nyoshi El Sadaat na kusema kuwa mwanadada huyo ni rafiki yake tu na wala sio vinginevyo. Akiongea na PB ya EATV , bright amesema hayo alikuwa amekwenda kwa ajili ya ktambulisha ngoma yake mpya ya kingasti na kusema kuwa taarifa hizo amekuwa akizisikia lakini hakuna ukweli wowote kuhusu hilo. sina mahusiano na mtoto wa nyoshi yule ni rafiki yangu tu.nimefahamiana nae baada ya kuambiwa kuwa amechora tatoo ya jina langu katika bega lake,kipindi hicho nilikuwa zangu Ifakara.“ Lakini pia anasema kuwa hata swala lililouwa likizushwa na msichana huyo kuwa na mimba halikuwa na ukweli  wowte kwa sababu wao ni marafiki tu.

The post Bright Amkana Mtoto wa Nyoshi appeared first on Ghafla!Tanzania.


Source

Kwa Mara ya Kwanza Taifa Stars Wameitwa Wachezaji 9 Wanaocheza Soka la Kulipwa


Kwa mara ya kwanza katika historia timu ya taifa imeitwa ikiwa na wachezaji tisa (9) wanaocheza soka nje ya nchi kwa ajili ya mechi dhidi ya Uganda kuwania kufuzu fainali za AFCON 2019.

Kutokana na ongezeko kubwa la wachezaji wa Tanzania kwenda kucheza nje ya nchi siku za hivi karibuni, nahodha wa Taifa Stars @samagoal77 amesema, tunapoelekea ni pazuri.

"Tunapoelekea ni pazuri, siku zote nilikuwa nikiomba na kupigana ili wachezaji wengi watoke Tanzania waende kucheza professional haijalishi ni wapi."

"Unapocheza kwenye ligi ambazo zimeendelea zaidi ya Tanzania kuna kitu kingine tofauti unajifunza. Unapokua kwenye ligi ya nyumbani unaweza kubadilishiwa makocha wanakuja kutoka sehemu tofauti lakini vitu ambavyo unaenda kukutana navyo kwenye ligi vinakua havina tofauti kubwa."

"Ombi langu na mawazo yangu siku zote ni wachezaji kwenda kucheza nje ya Tanzania kitu ambacho sasa hivi kinatokea, nadhani tunapiga hatua nzuri." - #regrann

Source

Dawa Za Nywele Zinazosababisha Uvimbe Wa Kizazi Kwa Wanawake


Dawa za kulainisha nywele (relaxer) zimekuwa zinapendwa na wanawake wengi wa Afrika kwa kuwa zina uwezo wa kulainisha nywele na kumfanya apendeze na awe wa kuvutia.

Hata hivyo, wataalamu wa afya wanadai kuwa dawa hizo zinasababisha uvimbe kwenye kizazi kutokana na kemikali za dawa hizo ambazo huingia mwilini kupitia majeraha au ngozi wakati wa kupaka.

Daktari wa Manispaa ya Ilala, Laurent Chipata alifanya utafiti na kubaini kuwa dawa za nywele na vipodozi zina kemikali ambazo husababisha uzalishwaji wa vichocheo kwa kiasi kikubwa na kusababisha uvimbe kwenye kizazi uitwao fibroids au leimyoma.

"Kemikali hizi hupenya kwenye ngozi na wakati mwingine hata kwa harufu tu, husababisha kuzalishwa kwa wingi wa vichocheo aina ya estrogen ambavyo huchangia kuota kwa uvimbe wa fibroids," anasema.

Dk Chipata anasema kukua kwa uvimbe kwenye kizazi hutokea katika kipindi ambacho mama yupo kwenye uzazi yaani kabla hajakoma hedhi.

Utafiti wa Dk Chipata ulifanywa nchini na kujumuisha wanawake wa kada tofauti tofauti wanaotumia dawa za nywele na wale wasiotumia na ukubwa wa tatizo hili ulibainika.

"Zipo kemikali tofauti tofauti zinazosababisha uvinbe kwenye kizazi, zipo za kwenye dawa za kilimo kama DDT na za kwenye mafuta ya ngozi kama vile mercury na hydroquionone," anasema.

Dk Chipata anasema madhara yanayopatikana katika kemikali za vipodozi ni makubwa siyo tu kwenye kizazi bali nyingine husababisha saratani au kufeli kwa figo. Anatoa mfano wa kemikali ya zebaki (mercury).

"Dawa za nywele zina madhara si lazima zipenye kwenye ngozi baada ya mtu kupata jeraha la kuungua bali zinaweza kupenya zenyewe kwenye ngozi kutokana na mfumo wa ngozi," anasema.

Anashauri kuwa ni vyema watu wakasoma kipodozi kimetengenezwa kwa nini kabla ya kukitumia na kuongeza kuwa ni salama zaidi kubaki na ngozi au nywele halisi badala ya kujibadilisha.

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imekataza vipodozi vyenye kemikali kama biothionol, hexachlorophene, mercury, vinyl chloride, zirconium na bidhaa zenye aerosol, chloroquionone, steroids, methylene na chloroform.

Utafiti mwingine uliofanywa mwaka 2012 na Dk Lauren Wise na wenzake nchini Marekani na kuchapishwa kwenye jarida la afya la nchini Marekani ulibaini kuwa vipodozi vingi vina kemikali zenye vichocheo vya estrogen ambavyo kwa kawaida huchochea kasi ya kuota kwa uvimbe kwenye kizazi cha mwanamke na wakati mwingine kwenye mji wa mimba. Kitaalamu uvimbe au vivimbe hivi hujulikana kama fibroids au myoma.

Dk Wise anasema aliwafanyia uchunguzi wanawake wanaotumia dawa za kulainisha nywele na kuangali umri walioanza kutumia dawa hizo, mara ngapi, waliungua kiasi gani na walikaa na dawa hizo kichwani kwa kipindi gani.

Aliwafuatilia wanawake 23,580 wanaotumia dawa za kulainisha nywele na baada ya kipindi fulani walipimwa. Kati yao, 7146 waligundulika kuwa na uvimbe kwenye kizazi baada ya kupimwa kwa mionzi na wengine kufanyiwa upasuaji.

Kwa nini relaxer ni hatari kwa wanawake?
Dk Wise anasema mchanganyiko ulio kenye dawa za nywele hasa zilizoandikwa "Lye Relaxer" ni sodium hydroxide wakati makopo ya dawa yaliyoandikwa "No Lye Relaxer" yana calcium hydroxide na guanidine carbonate.

Bidhaa za kulainishwa nywele zilizoandikwa 'no lye relaxer' zinadaiwa kusababisha majeraha kwa kiasi kidogo ukilinganisha na zile zilizoandikwa "Lye Relaxer".

Video: Snazzy Raffish X Kelvin Diploma – Rose

Msanii wa muziki Snazzy Raffish ameachia wimbo wake mpya uitwao Rose akiwa ameshirikiana na Kelvin Diploma. Wimbo huo unazungumzia masuala ya mapenzi na maisha, enjoy muziki mzuri kwa kuangalia video hapa chini.

The post Video: Snazzy Raffish X Kelvin Diploma – Rose appeared first on Bongo5.com.


Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...