Sunday, September 9, 2018
Dk Ndugulile awaasa wananchi kutoa taarifa wanapokosa matibabu
Na.Ahmad Mmow, Nachingwea.\
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto ,Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) amewaasa wananchi kutoa taarifa pale watakapokwenda hospitali na kukosa matibabu kwasababu ya kukosekana dawa.
Ndugulile ametoa rai hiyo jana katika kijiji cha Naipanga,wilaya ya Nachingwea wakati wa kilele cha kampeni ya kupima kwa hiyari maambukizi ya virusi vya UKIMWI ambayo imepewà na kutambulika kwa jina la "Furaha Yangu ".
Aliwahakikishia wananchi hao na wengine wote hapa nchini kwamba serikali ya awamu ya tano haitaki kuona wananchi wakienda kununua dawa madukani hivyo imejipanga kuhakikisha dawa zote zinazotolewa na serikali zinawafikia.
Alisema katika kuhakikisha huduma za afya zinatolewa kwa wananchi Serikali imewapeleka watumishi wa idara ya afya 48 katika wilaya hiyo ili wakatoe huduma kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vilivyopo wilayani humu.
"Upimaji wa virusi vya UKIMWI ni mpango wa kitaifa ili kuhakikisha kila Mtanzania anapima na kutambua afya yake, lengo ni kuwafikia asilimia 90 ya watu walioambukizwa na kutoa dawa,"alisema DkNdugulile ambae pia ni mbunge wa jimbo la Kigamboni.
Kwa upande wake ,mkuu wa wilaya Nachingwea, Rukia Muwango alisema zoezi la upimaji afya katika wilaya hiyo ni endelevu, kwani umuhimu wa wananchi kupima na kutambua afya zao ni mkubwa huku akiweka wazi kwamba maendeleo yatatokana na uimara wa afya za wananchi kwasababu mtaji wa kwanza wa maendeleo na uchumi wa taifa ni afya.
Mkuu huyo wa wilaya alibainisha kwamba kampeni hiyo ya upimaji kwa hiari inayoendelea wilayani humo ambayo yeye kwa kushirikiana na watalaam wa idara ya afya anaratibu na kusimamia.Tayari wanawake 809 na wanaume 531wamejitokeza na kupimwa.
"Hadi sasa miongoni mwahao waliopima ni watu saba tu ndio waliokutwa na maambukizi ya VVU na wameshapata ushauri nasaha na kuanzishiwa dawa za kupunguza makali ya Virusi Vya UKIMWI,"alisema Muwango.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Bongo Deco wauzai wa vifaa mbalimbali vya umeme kama TV, Subwoofer, Hometheator, Majiko madogo na makubwa ya Gesi, Friji, Generator nk leo w...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 29, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya ...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Kuongezeka kwa ghasia za hivi majuzi kumesababisha idadi kubwa ya raia wa Lebanon kukimbia kutoka Beirut huku milipuko ikitikisa jiji hilo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 15, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...