Thursday, September 6, 2018

Hakuna Mtu Aliyeumizwa na Msiba Wa Patrick Zaidi Yangu-Muna

Mwanamuziki wa nyimbo za Injili na mdau mkubwa wa Bongo fleva Rose Alphonce maarufu kama Muna Love amefunguka na kusema hakuna mtu aliyeumizwa na msiba wa mtoto Patrick Zaidi yake kama mama. Muna amefunguka kutokana na maneno ambayo amekuwa akikumbana nayo Kwenye mitandao ya kijamii ambapo watu wamekuwa wakimponda kutokana na maamuzi yake ya kutumia Kifo Cha mwanaye kama ushuda kanisani. Siku ya leo Muna alifanya mkutano na waandishi wa habari kwa ajili ya kutangaza Tamasha lake la Kidini litakalofanyika siku ya Jumamosi na aliweka wazi kuwa atatoa ushuhuda wake kuhusu Kifo Cha mtoto wake Patrick. Kwenye mahojiano na vyombo vya habari, Muna alijibu tuhuma za kumtumia mtoto wake ambapo alifunguka: Kwanza hakuna mtu anayeweza kusema ameumizwa na Kifo Cha Patrick zaidi ya mama mzazi na mimi tangu niingie Kwenye wokovu naamini hakuna mtu atakayeweza kuishi milele kila nafasi itaonja mauti lakini mimi natumia mwanangu ili kubasdilisha watu Ikiwa mimi mwanangu amenibadilisha nilikuwa mtu wa ajabu nilikuwa natukana na kufanya mambo mengi ya ajabu lakini niangalie leo hii nilivyobadilika". Mtoto wa Muna, Patrick alifariki dunia miezi michache iliyopita baada ya kuugua kwa muda mrefu.  

The post Hakuna Mtu Aliyeumizwa na Msiba Wa Patrick Zaidi Yangu-Muna appeared first on Ghafla!Tanzania.


Source

Tanzania, S. Africa ICT experts search for health, agriculture innovative solutions

Experts in Information and Communication Technology (ICT) from Tanzania and South Africa have embarked on a project to address challenges in the countries' agriculture and health sectors by using technology.
Source

Kanye West amwangukia Drake ataka wamalize bifu lao

Kanye na Drake.

Rapa Kanye West amemwomba radhi mwimbaji mwanzake, Drake,   kupitia mtandao wa Twitter akitaka wamalize bifu ya muda mrefu kati yao.

Wawili hao walikuwa katika mtafaruku wa muda mrefu ambapo Drake alikuwa akimkandia Kanye kupitia wimbo wa "Duppy Freestyle" kupitia kwa Pusha T.   Imeripotiwa pia kwamba miongoni mwa bifu kati ya hao ni pale Kanye alipovujisha siri za kile kinachoitwa "mtoto wa Drake" ambapo Pusha aliutumia dhidi yake kupitia wimbo wa "The Story of Adidon".

Katika kuomba radhi, Kanye, alimtumia Drake salamu za kumtakia kila la heri katika kumaliza mtafaruku kati yao.

MREMBO AFARIKI AKIONGEZA UKUBWA WA MAKALIO YAKE


Picha ya mwanamke mwenye makalio makubwa...haihusiani na habari hapa chini

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 23, anaripotiwa kufariki dunia, baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuongeza makalio kwa lugha ya kitaalamu Brazilian Butt Lift.



Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC, mwanamke huyo, Leah Cambridge kutoka mjini Leeds nchini England, alikutwa na umauti huo, baada ya kusafiri hadi nchini Uturuki kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji huo, lakini wakati kazi hiyo ikiendelea alipata mishtuko mitatu ya moyo.

Mwenzake ambaye aliongozana naye, Scott Franks, aliliambia gazeti la The Sun kwamba mwanamke huyo akifariki baada ya kudungwa sindano ya ganzi katika kliniki moja iliyopo katika mji wa Izmir uliopo Magharibi mwa nchi hii.

"Mrembo huyo alikubali kufanya upasuaji ughaibuni ambapo ni bei nafuu ikilinganishwa na Uingereza baada ya kukerwa na mafuta mengi katika sehemu yake ya tumbo baada ya kupata watoto," alisema Frank.

Wakizungumza na gazeti hilo, majirani zake walimtaja mwanamke huyo kuwa alikuwa anayevutia na wakasema kwamba wanaamini alienda kufanyiwa upasuaji huo mwezi uliopita bila kumshauri mpenzi wake.

Hata hivyo, Cambridge si mwanamke wa kwanza kutoka Uingereza ambaye amewahi kuwa na hamu ya kuwa na makalio ya kuvutia kupoteza maisha akiwa ughaibuni.

Mwanamke mwingine ambaye aliwahi kukutana na kifo ni Joy Williams ambaye alifanyiwa upasuaji kama huo, Oktoba 2014 mjini Bangkok nchini Thailand, lakini vidonda vyake vilipata maambukizi na mwanamke huyo ambaye alikuwa na umri wa miaka 24, alifariki wakati akidungwa sindano ya ganzi.


Miaka mitatu kabla ya kutokea kifo hicho, Claudia Aderotimi, mwenye umri wa miaka 20 kutoka katika mji wa Hackney, uliopo Mashariki mwa Jiji la London alifariki akiwa hotelini nchini Marekani wakati akipatiwa matibabu ya vidonda vya kujiongeza makalio yake.


Mmoja wa madaktari ambao wanafanya kazi hiyo ya upasuaji, Bryan Mayou, alisema licha ya upasuaji huo wa kuongeza makalio kutoonekana kuwa hatari, lakini ni tishio kama aina nyingine zozote za upasuaji.


"Hatari hiyo inatokana na kuwa upasuaji huo kufanywa na madaktari ambao hawajahitimu, nje ya hospitali bila kuwa na maelezo ya jinsi ya kujichunga baada ya matibabu hayo kufanywa," alisema Daktari Mayou, ambaye ni mwanachama wa muungano wa madaktari wa upasuaji nchini Uingereza.

Water woes, land disputes dominate JPM’s tour

Water and land challenges are characterising President John Magufuli's Lake Zone tour with residents believing that the coming of the Head of State will bring a lasting solution to their pressing issues.
Source

Wednesday, September 5, 2018

Joh Makini Atoa Sababu ya Kuimba Gospel.

Mwanamuziki Joh Makini Ambae hivi karibuni alitoa wimbo wenye maadhi ya kidini amefunguka na kusema kuwa aliamua kutoa wimbo huo ikiwa kama ishara ya kuwafikishia watu ujumbe juu ya kile Mungu anamfanyia katika maisha yake. Joh makini anasema wimbo huo hautakuwa wa kwanza kuimba kwa sababu anampangwa kuimba nyimbo za aina hiyo kila mara atakapokuwa akipata idea kwa sababu Mungu ni kila kitu kwake. “Hakuna mtu ambae hafahamu kuwa mungu ni kila kitu katika maisha yetu,nimeimba wimbo huu kwa mashabiki zangu ili kila mtu ajue kuwa swala la Mungu kuwa anatifanikisha katika maisha yetu sio swala la kumuachia yeye tu, sisi pia tunatakiwa kupambana kwa njia zetu ili na yeye aweze kubariki njia hizo ili kupata kile tunachotamani.”    

The post Joh Makini Atoa Sababu ya Kuimba Gospel. appeared first on Ghafla!Tanzania.


Source

Muhimu : JINSI YA KUPATA COMFIRMATION CODE KUTOKA TCU KWA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA UDSM 2018/2019


The following applicants have been selected to join various undergraduate degree programmes for the 2018/2019 academic year.

However, they have also been selected to join other Institutions. Kindly log into your UDSM Admission system and confirm your admission to UDSM before 10th September 2018. Failure to confirm by the deadline will indicate that you have not accepted the offer and your slot will be filled by other applicants. After confirmation, the selected applicants should report at their respective Campus on Saturday 27th October 2018

For the orientation week which will start on Monday 29th October 2018. Joining instructions and admission letters should be collected at the respective Campus. Joining instructions and other important information can also be downloaded from the University website at www.udsm.ac.tz (go to Undergraduate Section).

MLIMANI

NOTE: For candidate who did not receive special code from TCU for confirmation please send a text to 0771 607 687 to request a new code. In your message
Include the following:
1.Form IV index number
2.Candidated names as they appear in form IV certificates
3.User name (email) registered in the UDSM Admission System
4.Telephone number that will receive a new confirmation code

Akili the Brain Afunguka Kilichompoteza kwenye Game

Akili the Brain Afunguka Kilichompoteza kwenye Game
Msanii na mtayarishaji wa muziki wa bongo fleva, Akili The Brain amesema ukimya wake katika muziki ulitokana na yeye kuwaacha wasanii wenzake watangulie kutoa kazi zao pamoja na kusoma soko jinsi lilivyo kusudi aweze kuachia ngoma zake.

Akili The Brain amebainisha hayo alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha PLANET BONGO 'PB', inayorushwa na East Africa Radio, muda mchache alipomaliza kutambulisha wimbo wake mpya wa 'mashallah'.

"Kabla sijaachia ngoma yangu, nilifanya 'research' kidogo juu ya watu wanataka kitu gani kwa sasa, pamoja na namna muziki jinsi ulivyo kwa sasa. Naweza kubadilika kutokana na 'time' inavyokwenda kusudi niweze kuwapa kile wanachokihitaji watu", amesema Akili.

Pamoja na hayo, Akili ameendelea kwa kusema kuwa "nina 'plan' kubwa ninayotaka kuifanya lakini kwa sasa siwezi kuiweka wazi, kwasababu kuna baadhi ya mambo bado hayajakaa sawa ila Mungu akijalia kila kitu kitakuwa sawa tu".

Mbali na hilo, Akili The Brain ameweka wazi kuwa mara nyingi hupendelea kuwatumia waandishi kuandika mashairi ya ngoma zake, kwa lengo la kutaka kuwatendea haki mashabiki zake.

Akili The Brain ni miongoni mwa wasanii walioweza kuiteka jamii katika miaka ya 2006 kwa vibao vyake kama Bongo Bhangra, Nakupenda Regina na nyingine nyingi.
Source

EXCLUSIVE: Samatta afunguka ligi anayoitaka na dili lake la Levante ya Hispania

Nyota wa klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji na timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars" Mbwana Samatta amesema kuwa anatamani mno kwenda kucheza ligi kuu ya Uingereza huku akimtaja mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane kuwa ndiye anayemkubali barani Ulaya. Mbwana Samatta kutimkia La Liga ya Hispania, aandaliwa dau nono Bofya hapa kupata orodha ya vijana …

The post EXCLUSIVE: Samatta afunguka ligi anayoitaka na dili lake la Levante ya Hispania appeared first on Bongo5.com.


Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...