



OR- TAMISEMI
Serikali kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI inataendelea kuwachukulia hatua wakandarasi wanaotekeleza miradi ya ujenzi wa Barabara chini ya kiwango.
Hayo yamesemwa leo Aprili 30, 2025 Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa wakati akijibu swali la nyongeza la Mhe. Aleksia Kamguna,mbunge wa Viti maalum aliyetaka kujua serikali inawachukulia hatua gani wakandarasi wanojenga Barabara chini ya kiwango.
"Serikali inapotoa nafasi ya ujenzi wa barabara hizi kwa wakandarasi inatarajia wakandarasi waweze kuzingatia mkataba wanapokuwa wanatekeleza ujenzi wa barabara hizi za wilaya na serikali inakuwa makini kusimamia viwango" amesema Mhe.Katimba
Katika swali la msingi la Mhe. Kamguna ameuliza lini Serikali itajenga barabara za Wilaya ya Malinyi kwa kiwango cha Lami
Akijibu Swali hilo Mhe. Katimba amesema "Serikali inakusudia kujenga kwa tabaka la lami barabara za makao makuu ya wilaya zote hapa nchini ikiwemo wilaya ya Malinyi na katika mwaka 2024/25"
"Serikali inaendelea na ujenzi wa barabara ya Mnadani-Bomani inayoelekea Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi kwa tabaka la lami (kilomita 0.85) kwa thamani ya shilingi 759,000,000.00 Mpaka sasa ujenzi bado unaendelea na umefikia 30%". Mhe. Zainab Katimba
Mwenyekiti wa kamati ya uongozi ya Taifa ya TASAF Peter Ilomo ameipa mwezi mmoja kamati ya usimamizi miradi ya jamii TASAF kijiji cha Igomba kuhakikisha majengo ya zahanati ya kijiji hicho yanakamilika ili iweze kuanza kutoa huduma na kuwapunguzia adha wakazi wa Igomba kufuata huduma ya afya umbali mrefu.
Ilomo ametoa agizo hilo mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya zahanati hiyo iliyopo katika kijiji cha Igomba wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe ambapo amesema uwepo wa Zahanati ni muhimu katika kijiji hicho kwa kuwa wamekuwa wakifuata huduma ya afya kijiji jirani cha Isimike pamoja na kituo cha afya Saja vinavyopatikana umbali wa KM 6 kutoka kijijini hapo.
"Tujitahidi usiku na mchana,nimeambiwa mpango ni kumaliza mwezi wa tano lakini na mimi naongeza kidogo mpaka mwezi wa sita kwa kazi nilizoziona ili ikiwezekana mwezi wa saba huduma zianze kutolewa hapa"ameagiza Ilomo
Joyce Mdemwa ni Mratibu wa TASAF wilaya ya Wanging'ombe ameeleza kupokea maelekezo ya kukamilisha mradi huo huku wakazi wa Igomba wakishukuru kukamilishiwa zahanati yao ili kupunguza changamoto ya kufuata huduma ya afya umbali mrefu.
"Tunatarajia kukamilisha mradi huu tarehe theleathini mwezi wa tano na agizo la Mwenyekiti sisi tunamuahidi tutakamilisha na mwezi wa saba tutaanza kutoa huduma"amesema Joyce Mdemwa
Kijiji cha Igomba ni miongini mwa vijiji vya wilaya ya Wanging'ombe ambavyo vinanufaika na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ambapo licha ya kusaidia kaya maskini lakini pia kijiji hicho kilipokea Milioni 200.2 kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya Zahanati pamoja na nyumba ya mganga.
Jina langu ni Abeli Waihiga, mkazi wa Langata nchini Kenya kwa miaka zaidi ya 10 sasa, nimekuwa nikiishi maisha yangu bila wasiwasi wowote, najua hakuna ambacho kitaweza kuvamia nyumba au familia yangu.
Ngoja leo nikupe siri hii bure, unajua hakuna kinachomtisha mwizi kama kukuta hakuna kitu cha usalama kwenye mlango wa mbele, hakuna mbwa au kamera za CCTV zilizowekwa.
🔹Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Asisitiza Akili Mnemba Isaidie, Isiwe Kikwazo kwa Uhuru wa Habari
🔹 Serikali Yaanza Mchakato wa Kuandaa Sera ya Akili Mnemba kwa Uhuru wa Habari
🔹 Sera ya Habari na Utangazaji ya 2003 Kupitiwa Upya
Na Kadama Malunde - Malunde 1 Blog
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, amesema Serikali itaendelea kulinda uhuru wa vyombo vya habari kwa vitendo na si kwa maneno, akisisitiza matumizi sahihi ya akili mnemba (Artificial Intelligence) kama chachu ya uwajibikaji na si kikwazo kwa waandishi wa habari.
Akizungumza jijini Arusha leo Aprili 29, 2025, wakati akifungua rasmi maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani (World Press Freedom Day 2025) yenye kaulimbiu ya mwaka huu isemayo "Uhabarishaji katika Dunia Mpya: Mchango wa Akili Mnemba kwenye Uhuru wa Vyombo vya Habari", Mhe. Majaliwa ametoa wito kwa wanahabari kutumia akili mnemba kwa weledi na kuzingatia ukweli wa taarifa wanazotoa.
Waziri Mkuu ameeleza kuwa teknolojia ya Akili Mnemba inaweza kuwa msaada mkubwa katika kuboresha kazi za uandishi wa habari, lakini pia inaweza kuwa chanzo cha changamoto iwapo haitatumika kwa busara na uangalifu.
"Akili Mnemba itumike kama nyenzo kwa waandishi wa habari na siyo kikwazo. Mjitahidi kuitumia vizuri kwa uwajibikaji, kutoa taarifa sahihi na zenye kuzingatia maadili ya taaluma. Serikali kwa kushirikiana na wadau tunaendelea na mchakato wa kutengeneza sera kuhusu Akili Mnemba," amesema Mhe. Majaliwa.
Mhe. Kassim Majaliwa
Ameeleza kuwa Serikali imeanzisha mchakato wa kuandaa Sera ya Akili Mnemba, ili kuhakikisha teknolojia hiyo inaendana na misingi ya uhuru wa vyombo vya habari, uwazi na uadilifu katika taaluma ya uandishi wa habari.
Aidha, sambamba na mchakato huo, Serikali inaendelea kupitia upya Sera ya Habari na Utangazaji ya mwaka 2003 ili kuhakikisha inaimarisha na kulinda taaluma ya uandishi wa habari nchini.
"Hivyo, kupitia mijadala yenu katika maadhimisho haya, toeni maoni yenu kuhusu namna sera hiyo ya Akili Mnemba inavyopaswa kuwa, ili iendane na misingi ya uhuru wa vyombo vya habari," amesema Mhe. Majaliwa.
Katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, Mhe. Majaliwa ametaka vyombo vya habari kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru, haki na wa uwazi, akihimiza utoaji wa taarifa sahihi, zinazojenga amani na mshikamano.
"2025 huu ni mwaka wa uchaguzi. Sisi kama Serikali, kama wadau wa uchaguzi, pindi Tume Huru ya Uchaguzi watakapotoa ratiba, tunatarajia nyie ndiyo mtalieleza taifa. Na sisi ushiriki wetu ni kuhakikisha kwamba yale yaliyo muhimu ya kuufanya uchaguzi huu kuwa wa usalama, na kila mmoja atakwenda kushiriki kwa usalama wake... Na watu wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi wametuambia kwamba uchaguzi huu watausimamia kwa uhuru na haki na uwazi. Na sisi Serikali kama wadau wa uchaguzi tunataka tuwahakikishie kuwa uchaguzi huu utakuwa ni wa amani na utulivu," amesema Waziri Mkuu.
"Uchaguzi huu utakuwa wa amani na utulivu. Ninyi waandishi wa habari mtakuwa sehemu ya walinzi wa amani. Toeni taarifa zinazohamasisha kulinda tunu zetu za kitaifa," amesisitiza.
Waziri Mkuu pia amesema Serikali itaendelea kulinda uhuru wa habari kwa vitendo kwa kushirikiana na waandishi wa habari, ambapo tayari imeunda kamati ya kutathmini hali ya tasnia hiyo na kutatua changamoto zake.
Amesisitiza umuhimu wa vyombo vya habari kuelimisha na kuhabarisha jamii kuhusu maendeleo ya taifa kwa kuzingatia ukweli na uadilifu.
Profesa Paramagamba Kabudi
Kwa upande wake, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Paramagamba Kabudi, amewataka waandishi wa habari kutoitegemea tu teknolojia ya Akili Mnemba, bali waendelee kutumia uwezo wao wa kiakili kuchakata na kuandaa maudhui ya habari.
"Akili Mnemba isiwafanye mfubae, Waandishi wa habari tumieni akili yenu pia",amesema Profesa Kabudi.
Gerson Msigwa
Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Gerson Msigwa, amewapongeza waandishi wa habari kwa kutekeleza majukumu yao licha ya changamoto mbalimbali, huku akiwaasa wasikate tamaa kwani wao ni nguzo ya matumaini kwa wananchi.
Mhe. Paul Makonda
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Makonda, amesema waandishi wa habari wanalo jukumu kubwa la kulinda uchumi wa Taifa, na hivyo kuwataka wazipe kipaumbele habari zinazohamasisha wananchi kujikita katika shughuli za kiuchumi.
"Waandishi wa habari andikeni kuhusu uchumi, habari mnazoandika ziguse masuala ya kuchagiza uchumi",amesema Makonda.
Awali, Mwenyekiti wa Maadhimisho hayo ya uhuru wa vyombo vya habari mwaka huu 2025, Maxence Melo, ambaye pia ni Mkurugenzi wa JamiiAfrica, akiwasilisha baadhi ya maazimio ya mijadala ya wadau wa habari, amesema wamependekeza kufanyike mapitio ya Sera ya Habari na Utangazaji ya mwaka 2003 ili iendane na maendeleo ya teknolojia ya Akili Mnemba.Maxence Melo
Maazimio mengine ni pamoja na kuboreshwa kwa kanuni za maadili ya habari na kuhakikisha usalama na ulinzi wa waandishi wa habari, hususan kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.