Tuesday, April 29, 2025

Timu Zinazoongoza Kufunga Magoli Eneo la Hatari Ligi Kuu Tanzania



Katika takwimu mpya za Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara msimu wa 2024/25, klabu ya Young Africans (Yanga SC) imeendelea kudhihirisha ubabe wake kwa kuongoza kwa mabao mengi yaliyofungwa ndani ya eneo la hatari (boxi), ikiwa na jumla ya mabao 55.

Yanga SC imewazidi watani wao wa jadi Simba SC ambao wamefunga mabao 48 ndani ya boxi, huku Azam FC ikishika nafasi ya tatu kwa mabao 38. Singida Big Stars nao wameonyesha uwezo wao kwa kufunga mabao 37.

Timu nyingine zilizopo kwenye orodha ya juu ni Tabora United na Dodoma Jiji ambazo zote zina mabao 23, zikifuatiwa kwa karibu na Namungo FC yenye mabao 22 na Fountain Gate yenye mabao 20.

Hii ni dalili kuwa timu hizo zimekuwa na uwezo mkubwa wa kupenya ngome za wapinzani na kutumia nafasi zao vizuri ndani ya eneo la hatari. Kwa upande wa Yanga, mafanikio haya yanaonesha uimara wa safu yao ya ushambuliaji ambayo imekuwa moto wa kuotea mbali msimu huu.

Mashabiki na wadau wa soka wanaendelea kushuhudia ushindani mkali huku timu zikisaka pointi muhimu na nafasi bora kwenye msimamo wa ligi.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...