Wednesday, April 30, 2025

Hatimaye Hersi Said Aipongeza Timu Hii Kwa Ushindi......




Rais wa klabu ya Yanga SC na mwenyekiti wa Shirikisho la Vilabu barani Afrika ACA, Engineer Hersi Said ametoa salamu za pongezi kwa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka kumi na tano kwa kuchukua ubingwa wa mashindano ya mpira wa miguu kwa shule za Afrika (CAF Africa Schools Football Championship).


Kulingana na taarifa tulizozipata hivi sasa, timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 15 wameshinda ubingwa wa mashindano hayo kwa mara ya pili mfululizo. Jambo ambalo huenda likainua vipaji katika soka nchini Tanzania.

Mechi hiyo iliandaliwa na kuchezwa nchini Ghana. Rais Hersi Said alitoa ahadi ya zawadi kwa vijana hawa. Kulingana na taarifa tulizozipata hivi sasa, zawadi hiyo itakabidhiwa na Mtendaji mkuu wa klabu ya Yanga SC baada ya timu hiyo kutendeka nchini Tanzania.



Asante kwa kusoma taarifa hii, unaweza kutoa maoni yako ili kuboresha uandishi wetu, maoni yatolewe kwenye nafasi ya kutoa maoni iliyopo hapo chini.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...