Wednesday, February 26, 2025

Amnesty yamtaka Rais Joe Biden kulifunga gereza la Guantanamo

Shirika la kutetea haki za binadamu Amnesty International limemtaka Rais Joe Biden kuitimiza ahadi yake ya kulifunga gereza la Guantanamo wakati ambapo maadhimisho ya miaka 20 tangu kufunguliwa kwake yakiwa yanakaribia. Gereza hilo lilifunguliwa mahsusi kwa ajili ya kuwazuia washukiwa wa ugaidi waliokamatwa na Marekani katika vita vyake dhidi ya ugaidi. Ni gereza lililo kwenye …

The post Amnesty yamtaka Rais Joe Biden kulifunga gereza la Guantanamo appeared first on Bongo5.com.

Saturday, February 22, 2025

DAWASA WATANGAZA FURSA LUKUKI KWA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA


Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Mhandisi Mkama Bwire ametangaza fursa lukuki kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Wilaya ya Kigamboni zitakazotokana na ushirikiano bora uliitengenezwa baina yao na Mamlaka hiyo.

Mhandisi Bwire amebainisha fursa hizo katika kikao kazi na wenyeviti hao kilicholenga kuboresha mahusiano na kujenga ukaribu baina ya Serikali za Mitaa na DAWASA.

"Ukaribu huu unakuja na fursa nyingi ndugu wenyeviti ambazo zitanufaisha pande zote mbili , Serikali pamoja na wenyeviti kama mtu mmoja mmoja, kuanzia saa wwenyekiti atakaetusaidia kuhamasisha maunganisho na kutuletea wateja atapata kiasi cha Shilingi 10,000 kwa kila mteja mmoja anaemleta," amesema Mhandisi Bwire.

Bwire amesema sio hivyo tu lakini hata kwa wale ambao watasaidia kufichua wahujumu kwa Mamlaka mfano wezi wa maji hawataacha hivi hivi bali nao watanufaika kwa uzalendo watakaouonyesha.

"Ndugu zangu wenyeviti kwa kila mmoja wenu atakae saidia kubaini mwizi wa maji na tukamkamata na kumpiga faini basi Mwenyekiti uliesaidia kubaini hilo utapata asilimia 30 ya fedha zitakazolipwa kama faini," amesema Mhandisi Bwire

Bwire amesema motisha hii kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa itakua chachu ya wao kushirikiana na Mamlaka zaidi katika shughuli za kila siku kuwapatia huduma ya maji wananchi.

Mhandisi Bwire amesema hawataishia hapo tu bali watatoa motisha kwa kila Mwenyekiti atakaesaidia kushawishi mteja aliesitishiwa huduma Kulipa deni lake na kurudi kutumia huduma za DAWASA.

Hatua hii imepokelewa vyema na wenyeviti waliohudhuria kikao kazi hicho huku wakiahidi kufanya kazi bega kwa bega na DAWASA kuhakikisha wananchi wanapata huduma Bora ya Majisafi wakati wote.

Kamati ya kudumu ya Bunge yaridhishwa kasi ujenzi Soko la Kariakoo


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imeridhishwa na ujenzi  unaoendelea wa Mradi wa Soko la Kariakoo jijini Dar es salaam.

Akizungumza hii leo tarehe 21 Februari, 2025 mara baada ya ziara ya kutembelea na kukagua ujenzi wa Mradi wa Soko la Kariakoo pamoja na kujionea eneo lilipotokea tukio la kuporomoka kwa jengo la ghorofa Kariakoo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Florent Kyombo ameipongeza Serikali  ya Awamu ya Sita chini ya uongozi mahiri wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa namna ilivyopambana kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha inaokoa watu na mali wakati yalipotokea maafa  nchini.

Makamu Mwenyekiti huyo ameleza kuwa kuanza kwa ujenzi wa mradi wa soko la Kariakoo ni hatua nzuri ambayo itasaidia wafanyabiashara na wengine wanaopata huduma katika eneo hilo kufanya shughuli zao katika eneo rafiki na salama.

Akizungumza kuhusu jengo lililoporomoka katika eneo la Kariakoo amesema Serikali imeendelea kuratibu vyema masuala ya menejimenti ya maafa nchini kwa kuchukua hatua za haraka katika kunusuru uhai na mali za watu wake pindi maafa yanapotokea.

"Tunaendelea kuishukuru na kuipongeza Serikali kupitia Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa upendo wake mkubwa na moyo wa kujali aliouonesha wakati wote tulipopatwa na haya maafa hadi sasa Serikali inapoendelea kuimarisha miundombinu na kurejesha hali," Amesema Mhe. Kyombo.

Naye Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu  anayeshughulikia  masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mheshimiwa Ummy Nderiananga ameipongeza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kwa uamuzi wake wa kutembelea na kujionea athari zilizotokana na kuanguka kwa ghorofa hilo na hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa mradi wa Soko la Kariakoo.

"Tunamshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa upendo wake tangu maafa haya yalipotokea hadi sasa katika hatua zote za uokoaji wa watu na mali zao. Pia niwapongeze vyombo vya ulinzi na Watanzania wote kwa ushirikiano wote waliouonesha wakati wote wa maafa yalipotokea hadi kufikia hapa Serikali inapoendelea kufanya kila jitihada za  kurejesha hali," Alipongeza Mhe. Nderiananga.

Ikumbukwe Ghorofa hilo liliporomoka mnamo tarehe 16 Novemba, 2024 muda wa saa tatu asubuhi katika Mkoa wa Dar es Salaam, Wilaya ya Ilala, Kata ya Kariakoo, Mtaa wa Kariakoo Magharibi, Barabara ya Mchikichi Kiwanja Na. 12 Kitalu Na.7. Jengo hilo, lililokuwa likitumika kwa shughuli za kibiashara ikiwemo maduka na maghala ya kuhifadhi bidhaa za wafanyabiashara. Tukio hilo lilisababisha Vifo vya watu 31 na kujeruhi watu 71.


Thursday, February 20, 2025

ZIARA YA WAZAZI CCM SHINYANGA MJINI KATA KWA KATA YAPAMBA MOTO... MAKAMBA AONYA 'ULEVI KWA AKINA MAMA'


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji  Jumuiya ya wazazi CCM wilaya Shinyanga Mjini wanaendelea na ziara ya kutembelea kata mbalimbali za Jimbo la Shinyanga Mjini. 

Ziara hii inahusisha kuzungumza na wanachama na viongozi wa CCM, kufanya tathmini ya utekelezaji wa Ilani ya CCM, kuangalia hali ya uhai wa chama, na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo hayo.

Ziara hiyo ilianza tarehe 18 Februari 2025 na hadi sasa, na leo Februari 20,2025 wajumbe wamefika katika kata ya Ndembezi, Chibe, na Ibinzamata.

 Wakiwa katika ziara hiyo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko, amesisitiza umuhimu wa wanachama wa CCM kudumisha mshikamano na umoja ili kuimarisha chama na kuendelea na utekelezaji wa mipango yake ya maendeleo.

Mrindoko pia ameipongeza Serikali kwa kutoa fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo, ikiwemo miradi ya barabara, elimu, maji, na afya, na kuhimiza jamii kuendelea kushirikiana kwa pamoja katika utekelezaji wa miradi hiyo.

Aidha, Mrindoko ametoa wito kwa jamii kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vya unyanyasaji, huku akionya kuhusu vitendo vya ulawiti na ubakaji, na kuhamasisha jamii kuchukua hatua za haraka ili kukomesha vitendo hivi vinavyohatarisha usalama wa watoto.

Naye, Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mary Makamba, ametoa onyo kwa akina mama kuhusu madhara ya ulevi kwa familia.

Mary Makamba

 Amesisitiza kwamba ulevi, hasa pombe, unachangia migogoro ya familia na hata kudhoofisha afya ya akili ya akina baba. 

Ameeleza kwamba baadhi ya ndoa zimevunjika au kuingia matatizoni kwa sababu ya tabia ya wanawake kujiingiza katika ulevi.

Makamba pia amewahimiza akina mama kupunguza matumizi ya pombe na kuzingatia malezi bora ya familia. 

"Mama zangu tupunguze pombe, tupunguze ulevi... kuna msemo tunasema 'kumwagilia moyo'. Ndoa nyingi zipo mahakamani kwa sababu ya sisi akina mama tumekuwa walevi, tunakunywa sana pombe, unakuta mama anaenda kulewa anarudi nyumbani usiku wa manane matokeo yake imekuwa chanzo migogoro katika familia, tunawatengenezea akina baba matatizo ya afya ya akili, wanashindwa kutafuta pesa",amesema Makamba.

Aidha ametahadharisha kuhusu mavazi yasiyofaa na athari zake katika jamii, na akatoa tahadhari kuhusu wanawake kujihusisha na mikopo umiza, ambayo pia imetajwa kuwa chanzo cha migogoro ndani ya familia.

Ziara hii inaendelea kuhamasisha umoja, maendeleo, na maadili mema katika jamii, huku wakazi wa Shinyanga Mjini wakiwa na nafasi ya kujadili masuala ya kijamii, kisiasa, na kiuchumi kwa lengo la kujenga mustakabali bora kwa wote.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Ndembezi
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Ndembezi
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Ndembezi

Wajumbe wa kamati ya utekelezaji wazazi ccm wilaya Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji  Jumuiya ya wazazi CCM wilaya Shinyanga Mjini wakitembelea Daraja la Chibe - Old Shinyanga
Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji  Jumuiya ya wazazi CCM wilaya Shinyanga Mjini wakitembelea Daraja la Chibe - Old Shinyanga
Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji  Jumuiya ya wazazi CCM wilaya Shinyanga Mjini wakitembelea Daraja la Chibe - Old Shinyanga
Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji  Jumuiya ya wazazi CCM wilaya Shinyanga Mjini wakitembelea Daraja la Chibe - Old Shinyanga
Muonekano wa sehemu ya Daraja la Chibe - Old Shinyanga
Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji  Jumuiya ya wazazi CCM wilaya Shinyanga Mjini wakitembelea Daraja la Chibe - Old Shinyanga
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza katika daraja la Ibinzamata Makaburini
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza katika daraja la Ibinzamata Makaburini
Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji  Jumuiya ya wazazi CCM wilaya Shinyanga Mjini wakiwa katika daraja la Ibinzamata Makaburini
Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji  Jumuiya ya wazazi CCM wilaya Shinyanga Mjini wakiwa katika daraja la Ibinzamata Makaburini
Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji  Jumuiya ya wazazi CCM wilaya Shinyanga Mjini wakiwa katika daraja la Ibinzamata Makaburini
Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji  Jumuiya ya wazazi CCM wilaya Shinyanga Mjini wakiondoka katika daraja la Ibinzamata Makaburini
Ujenzi wa daraja la Ibinzamata Makaburini ukiendelea
Ujenzi wa daraja la Ibinzamata Makaburini ukiendelea
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza na wanachama na Viongozi wa CCM Kata ya Chibe
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza na wanachama na Viongozi wa CCM Kata ya Chibe
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza na wanachama na Viongozi wa CCM Kata ya Chibe
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhandisi James Jumbe akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Chibe
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...