Tuesday, December 31, 2024

MBUNGE RWEIKIZA ALIVYOLIPAMBA JIMBO LAKE

Abainisha miradi mikubwa ya maendeleo kupitia kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa Baba yake mzazi

Na Lydia Lugakila - Bukoba

MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dkt. Jasson Rweikiza amebainisha miradi mikubwa ya maendeleo iliyofanyika na inayoendelea kufanyika jimboni kwake huku akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi Bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera.

Mbunge Rweikiza ametoa ufafanuzi huo  wakati akiongea wananchi mbalimbali pamoja na viongozi wa Mkoa wa Kagera waliofika katika viwanja vya Rweikiza vya shule ya Rweikiza iliyopo  Kyetema Wilaya ya Bukoba  kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa Baba yake mzazi aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza. 

Rweikiza amebainisha kuwa,Dkt. Samia Suluhu Hassan amelipendelea Sana Jimbo lake kwani ametoa Mabilioni ya fedha kwa ajili ya maendeleo jimboni humo.

Akieleza miradi hiyo Mbunge huyo amesema kuwa pamoja na Daraja la Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bilioni 9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja hilo kuchoka kwasababu limejengwa muda mrefu.

Amesema Daraja hilo ambalo lipo Barabara kuu inayounganisha kata zote za Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba,Misenyi na Karagwe  Wananchi hulitumia katika kusafirisha mazao na bidhaa nyingine.

Akitaja Daraja lingine amesema ni la Chanyabasa ambapo wananchi hutumia kivuko kuvuka toka kata zaidi ya nane kuja hospitali ya Wilaya ya Bukoba Vijijini na wengime wanaovuka kwenda Bukoba mjini kwa shughuli za kujiingizia kipato jambo linalosababusha  watumie muda mrefu wakisubiri kivuko kwasababu kinavusha watu wachache na mizigo kidogo.

Aidha amesema ujenzi huo unaotarajiwa kuanza muda wowote kuanzia hivi sasa unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 12 kutokana na maagizo ya Serikali awamu ya sita.

 Ametaja daraja jingine ambalo limeingizwa kwenye mpango wa kufanyiwa ukarabati mkubwa na fedha yake italetwa wakati wowote kuwa ni Kyetema, linaunganisha

Barabara kuu kutoka Dar es Salaam na mikoa mingine kuingia Bukoba na nchi jirani ya Uganda.

"Nitumie fursa hii kwa niaba ya Wananchi wa jimbo la Bukoba vijijini nimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa upendo wake mkubwa kwetu ametoa fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo yetu"alisema Dokta Rweikiza.

Ameongeza kuwa kuna mradi mkubwa wa maji Kemondo ambao umekamilika na wananchi wanatarajia kupata maji mwezi mmoja ujao.

Naye askofu wa Dayosisi ya kaskazini magharibi (KKKT)  Abedinego Keshomshahara amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inafanya maendeleo makubwa kwa Wananchi pia mbunge Rweikiza amekuwa kiungo kizuri kati ya wananchi,Serikali na viongozi wa dini zote.

Kwa upande wa katibu mkuu mstaafu wa chama cha Mapinduzi (CCM),katibu mkuu kiongozi mstaafu,Balozi na mbunge Dkt .Bashir  amesema Mbunge huyo ameonyesha mfano mzuri kwa Wananchi wake na Taifa kwa ujumla.

"Maombi ya miradi hiyo ililetwa kwenye chama wakati wa Serikali ya awamu ya tano na mbunge Rweikiza ambapo tuliingiza kwenye Ilani ila kutokana na maono mema ya Rais Dokta Samia  ameamua kutoa fedha nyingi ili ikajengwe na kunufaisha Wananchi" alisema Dokta Bashir.

BONANZA LA MICHEZO DR. SAMIA - JUMBE HOLIDAY LA KUFUNGA MWAKA 2024 NA KUUKARIBISHA MWAKA 2025 LAPAMBA MOTO SHINYANGA


Na Marco Maduhu,SHINYANGA

BONANZA la Michezo Dr. Samia/Jumbe Holiday limeendelea kushika kasi katika viwanja vya CCM Kambarage Mjini Shinyanga, kwa kuchezwa michezo mbalimbali.
Jackline Isaro (kulia) akicheza bao mara baada ya kuzindua bonanza hilo.

Mratibu wa bonanza hilo Jackline Isaro akizungumza juu ya bonanza hilo amesema linafanyika leo Desemba 31,2024 na kutamatika Januari Mosi 2025 majira ya saa 7 usiku katika viwanja vya mpira wa kikapu Risasi huku washindi wakipewa zawadi zao.
Jackline akizungumza kwa niaba ya James Jumbe ambaye ndiyo muandaaji wa bonanza hilo, amewataka majaji watende haki ili washindi wapatikane kwa uhalali.

Aidha, michezo ambayo inachezwa kwenye bonanza hilo ni mbio za baiskeli, mchezo wa bao,drafti,karata,ususi,Ps Game,Mpira wa pete,kikapu,kufukuza kuku kwa jinsia zote,kushindana kula,Polltable,kucheza mziki.
Michezo mingine ni mpira wa miguu, ambapo itakuwa kati ya bodaboda dhidi bajaji,bingwa wilaya 'Ranges' dhidi ya ngokolo, pamoja na DERBY ya upongoji.

Zawadi za washindi ni kwamba katika mbio za baiskeli mshindi katika makundi manne zawadi ni sh.milioni 2.1,mchezo wa bao mshindi wa kwanza sh.100,000,drafti mshindi wa kwanza sh.100,000, karat ash.100,000,msusi sh.100,000, Ps game mshindi wa kwanza sh.200,000 wapili sh.100,000, watatu sh.50,000.
Mpira wa pete, washindi wa kwanza watapewa sh.500,000, kleti za soda 7, mchele kilo 50, washindi wa pili sh.300,000, mchele kilo 50 na soda kleti 7.

Mpira wa kikapu kwa njinsia zote, mshindi wa kwanza atapa sh.500,000 na wapili sh.300,000.
Mchezo wa kufukuza kuku kwa jinsia zote washindi wa kwanza watapa kuku na sh.20,000, na mchezo wa kushinda kula washinda wakwanza watapata sh.20,000, huku mchezo wa polltable mshindi wa kwanza ataibuka na kitita cha sh.100,000, wapili sh.50,000.

Kwa upande wa mpira wa miguu timu ya bodaboda dhidi ya bajaji, mshindi wa kwanza atapata sh.500,000, Ng'ombe mmoja,kleti 7 za soda na mchele kilo 100, wapili sh.300,000, ng'ombe mmoja na mchele kilo 100.
Zawadi zingine bingwa wa wilaya Rangers dhidi ya Ngokolo, mshindi wa kwanza atapata 500,000,Ng'ombe mmoja, mchele kilo 100 na kleti 10 za soda, wapili atapata sh.300,000,Ng'ombe mmoja na soda kleti 10.

DERBY ya upongoji kwamba mshindi wa kwanza atapata sh.1,000,000, Ng'ombe mmoja,mchele kilo 100 na kleti 10 za soda, huku mshindi wa pili akipata sh.500,000,Ng'ombe mmoja, mchele kilo 100 na soda kleti 10.

TAZAMA PICHAπŸ‘‡πŸ‘‡
Mratibu wa bonanza la michezo Dr.Samia/ Jumbe Holiday Jackline Isaro akizindua bonanza hilo.
Mratibu wa bonanza la michezo Dr.Samia/jumbe Holiday Jackline Isaro akicheza bao.
Michezo mbalimbali ikiendelea kuchezwa kwenye bonanza hilo.

Friday, December 27, 2024

Msimu Huu Ligi ya NBC ni Ngumu Sana, Huwezi Hata Kutabiri Bingwa

 

Msimu Huu Ligi ya NBC ni Ngumu Sana, Huwezi Hata Kutabiri Bingwa

Msimu huu Simba kapiga Azam,Yanga kapigwa na Azam halafu Simba kapigwa na YangaπŸ˜„

Bado mechi moja Simba na Yanga wakamilishe mechi 15 Za Round ya kwanza.

Simba wako kileleni kwa tofauti ya alama moja mbele ya Yanga.

Kabla ya kupoteza mechi Yao kwa kwanza dhidi ya Azam,Yanga walipiga mechi 8 bila kupoa wala kuruhusu goli,baada ya kufungwa na Yanga,Simba wamepiga mechi 8 mfululizo bila kudondosha alama.

Trust me Msimu huu tunakwenda kuwa na ligi ngumu sana,sitarajii bingwa kupatikana kwa tofauti ya alama 5 au 6 BIG NO!

Natarajia bingwa atapatikana kwa tofauti ya alama 1 au magoli ya kifungwa na kufunga.

Yes! Ligi ya msimu huu ni ngumu sana

Thursday, December 26, 2024

Airtel yamwaga zawadi kwa wateja wake kupitia promosheni ya Santa Mizawadi



KAMPUNI ya Airtel imetangaza Washindi wa droo ya Kwanza ya Santa Mizawadi inayotolewa na Bwana Santa wa Airtel.

Akizugumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam leo Desemba 24, 2024 Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano, Jackson Mmbando  amesema promesheni hiyo  bado inaendelea na droo ya kwanza imetangazwa leo ambapo washindi ni kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Amesema Airtel Santa Mizawadi ni promosheni kabambe ambayo itawapa washindi fursa ya kuondoka na zawadi kemkem ikiwemo pocket WiFi, simu janja, pikipiki, runinga na pesa Taslim hadi shilingi milioni moja.

"Jinsi ya kushiriki na  kujishindia Mizawadi ya Airtel Santa Mizawadi, Wakala wa Airtel  atatakiwa kufanya miamala ya kuweka na kutoa fedha, ambapo pia ili Mteja aweze kuingia kwenye droo anatakiwa tu kufanya miamala kama vile kununua bando, Kutuma pesa,  kutoa pesa, kulipa bili, kufanya miamala ya kibenki, kutuma au kupokea pesa nje ya nchi, kununua muda wa maongezi.

"Ndugu mteja , Wakala usipitwe na zawadi hizi kutoka kwa Mr Santa ambspi leo Jumanne Desemba 24 tumeshawatangaza.." Amesema

Mmbando amesema droo ya kuwapata washindi wengine itakuwa ikifanyika jumanne mpaka mwezi wakwanza ambapo washindi wakipigiwa simu kupitia namba 100 pekee na kuambiwa ni kitu gani ameshinda katika droo kama ilivyofanyika leo.

"Mteja wetu usikose kuendelea kutumia huduma zetu za Airtel ikiwemo kuweka Pesa na kutoa, kulipa bili mbalimbali ili kuweza kuingia katika droo ya kujishindia zawadi mbalimbali." Amesema

Washindi waliotangazwa ni kutoka Mkoa wa Dar es Salaam, Shinyanga washindi wawili, Nzega pamoja Ifakara Mkoani Morogoro.


Source

ISSA GAVU ATOA ZAWADI KWA WASHINDI WA MASHINDANO YA MICHEZO MBALIMBALI - UNGUJA


Mwakilishi wa Jimbo la Chwaka Mkoa kusini Unguja Mhe. Issa Ussi Gavu ambaye ni Katibu wa Oganazesheni wa CCM Taifa (MCC) ametoa zawadi mbalimbali za medali, vikombe na fedha kwa washindi walioshinda kwenye mashindano ya waendesha baiskeli, mchezo wa bao, karata, kukimbiza kuku nk.

Kabla ya kuanza kwa mashindano hayo wananchi wa Jimbo hilo na viongozi mbalimbali wa Chama walianza kwa matembezi ya amani kuhamasisha kuelekea miaka 61 ya sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar ambayo yanatarajiwa kufanyika mwezi Januari 12 mwaka 2025.

Wakizungumza kwenye tamasha hilo wananchi hao wameshukuru Serikali ya CCM Chini ya Rais Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi na Mwakilishi wa Jimbo hilo kwa kuwaletea maendeleo na kutimiza zaidi ya asilimia 95 ya ahadi zake katika kipindi cha muda wake wa uongozi na kutekeleza ilani ya CCM ikiwemo barabara, afya, elimu na fursa za uchumi kwa vijana na wanawake.

Mashindano hayo yamefanyika ikiwa ni kuelekea miaka 61 ya sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar.

Wednesday, December 25, 2024

Watu Saba Wafariki Ajali ya Lori na Coaster Handeni Tanga



Watu saba wamepoteza maisha na wengine 10 wamejeruhiwa kwenye ajali iliyohusisha lori na Coaster eneo la Michungwani Kata ya Segera wilaya ya Handeni mkoani Tanga.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Alberto Msando amesema kutokana na kujirudia rudia kwa uzembe barabarani, amemwelekeza OCD kuwa atakayekiuka sheria za barabarani eneo la Handeni atafikishwa mahakamani na kupewa adhabu ya kifungo.

"Kwa ambao mmekuwa mkipiga simu kusaidiwa madereva wenu wakikiuka sheria za barabarani, wala msisumbuke. Hakuna msaada zaidi ya kukaa lock-up kwa mujibu wa sheria na kupandishwa kizimbani. Ukifika Kijiji cha Manga Wilaya ya Handeni, ewe dereva usipofuata sheria za usalama barabarani usitulaumu," amesema.

Monday, December 23, 2024

Jean Baleke Apotea Kusiko Julikana, Mazoezini na Yanga Haendi Tena...



MSHAMBULIAJI wa Yanga Jean Baleke amejiweka karibu na mlango mgumu wa kutokea baada ya kukacha mazoezi ya timu hiyo. Baleke hajaonekana ndani ya kambi ya Yanga kwa zaidi ya wiki moja akikosa ratiba zote za mazoezi ya timu hiyo huku pia hata uwanjani akikosekana.
.
Mshambuliaji huyo alikuwa katika msafara wa Yanga ikiifuata MC Alger ya Algeria kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika lakini hakukaa hata benchini. Baada ya hapo Baleke ambaye anaichezea Yanga kwa mkopo hajaonekana tena kwenye kambi ya Yanga.
.

Saturday, December 21, 2024

Allan Okello Usajili Mpya Simba

Allan Okello Usajili Mpya Simba


Mabosi wa klabu ya Simba wanapiga hesabu kali ya kuimarisha kikosi kama mapendekezo ya kocha Fadlu David na sasa wamevuka mpaka hadi Uganda kufuata fundi wa mpira kiungo mshambuliaji, Allan Okello anayetumia mguu wa kushoto, ili kuja kuongeza nguvu.

.

Okello, mwenye umri wa miaka 24 amewahi kupita KCCA na Paradou zote za Uganda kwa sasa anakipiga Vipers iliyopo Ligi Kuu ya nchi hiyo, anayetajwa ni fundi wa mpira kwelikweli kwani analijua boli na inaelezwa kama atashuka Msimbazi na kuungana na wachezaji waliopo basi balaa litakuwa kubwa kwa wapinzani siku watakapokutana uwanjani iwe katika Ligi, Kombe la Shirikisho nchini au lile ya CAF, ikiwa Kundi A.

.

Hatua nzuri kwa Simba ni kwamba kama itampata fundi huyo atatumika moja kwa moja katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu kwani Vipers haikushiriki mashindano hayo msimu huu. Utata pekee wa Simba kumpata Okello ni uwepo wa Rais wa klabu hiyo, Lawrence Mulindwa ambaye amekuwa mtata kuachia mastaa wake muhimu wa kikosi hicho kuuzwa. Mulindwa ndiye aliyeweka ngumu kumuachia alive kuwa mshambuliaji wa timu hiyo Cesar Manzoki aliyekuwa anawindwa na Simba.

.


Source

UZINDUZI WA NYUMBA 109 KWA WAATHIRIKA WA MAPOROMOKO YA TOPE MKOANI MANYARA


Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Ndugu John Mongella, leo Desemba 20, 2024, amemwakilisha Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, katika hafla ya uzinduzi wa nyumba 109 zilizojengwa kwa waathirika wa maporomoko ya tope yaliyotokea tarehe 3 Desemba 2023, mkoani Manyara.

Akizungumza kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Mongella ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa juhudi zake za kuhakikisha ujenzi wa nyumba hizo unakamilika kwa wakati. Alisema hatua hiyo ni kielelezo thabiti cha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, inayolenga kuimarisha ustawi wa jamii na kuboresha maisha ya wananchi.

"Tunajivunia kazi kubwa inayotekelezwa na serikali chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Chama Cha Mapinduzi wakati wote kitakuwa karibu na Serikali katika juhudi zote za kuwaletea wananchi maendeleo na ustawi," alisema Mongella.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, amepongeza Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake kwa kushirikiana na serikali wakati wa zoezi la uokoaji na katika hatua za kufanikisha ujenzi wa nyumba hizo.

"Tunatoa shukrani za dhati kwa CCM kwa msaada wao mkubwa katika mchakato wa kusaidia waathirika, ikiwemo rasilimali na nguvu kazi. Nyumba hizi ni ushuhuda wa mshikamano wetu wa kitaifa katika kukabiliana na changamoto za majanga," alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

Nyumba hizi 109, zilizojengwa kwa ustadi na kwa kuzingatia mahitaji ya waathirika, zimekuwa alama ya matumaini mapya kwa familia zilizoathirika. Uzinduzi huu ni hatua muhimu ya kuwawezesha waathirika kuanza maisha upya kwa heshima na usalama, huku ukidhihirisha dhamira ya serikali na CCM ya kuwaletea maendeleo wananchi wote.

Airtel yashusha Santa Mizawadi kwa wateja na mawakala wake


KAMPUNI ya Airtel imewaomba wateja na mawakala wanaotumia mtandao huo kuendelea kuchangamkia promosheni maalum ya Airtel Santa Mizawadi ili waweze kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo pesa taslimu.

Akizugumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam leo Desemba 20, 2024 Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando amesema promesheni hiyo bado inaendelea na droo ya kwanza itafanyika Jumanne na kila Juma nne ya kila wiki ndani ya Mwezi mmoja wa sikuku.

Amesema Airtel Santa Mizawadi ni promosheni kabambe ambayo itawapa washindi fursa ya kuondoka na zawadi kemkem ikiwemo pocket WiFi, simu janja, pikipiki, runinga na pesa Taslim hadi shilingi milioni moja.

"Jinsi ya kushiriki na kujishindia Mizawadi ya Airtel Santa Mizawadi, Wakala wa Airtel atatakiwa kufanya miamala ya kuweka na kutoa fedha, ambapo pia ili Mteja aweze kuingia kwenye droo anatakiwa tu kufanya miamala kama vile kununua bando, Kutuma pesa, kutoa pesa, kulipa bili, kufanya miamala ya kibenki, kutuma au kupokea pesa nje ya nchi, kununua muda wa maongezi.

Kwa upande Meneja wa huduma kwa wateja, Celine Njuju amesema mtandao wa Airtel umekuwa ukiwathamini sana wateja wake pamoja na mawakala ndo maana wameamua kuja na Airtel Santa Mizawadi katika msimu huu wa sikukuu

Amesema katika msimu huu balozi wa mtandao huo Mr Santa atakuwa akizunguka katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya kutoa zawadi mbalimbali na kemkem kwa mawakala pamoja na watumia wa mtandao huo.

Zawadi zitakazotolewa ni pocket WiFi, simu janja, pikipiki, runinga na pesa Taslim hadi shilingi milioni moja.

"Ndugu mteja , Wakala usipitwe na zawadi hizi kutoka kwa Mr Santa.."amesema

Mmbando amesema droo ya kuwapata washindi itakuwa ikifanyika mara moja kwa wiki siku ya Jumanne na kusisitiza kuwa washindi watakuwa wakipigiwa simu kupitia namba 100 pekee na kuambiwa ni kitu gani ameshinda katika droo hiyo.

"Mteja wetu usikose kuendelea kutumia huduma zetu za Airtel ikiwemo kuweka Pesa na kutoa, kulipa bili mbalimbali ili kuweza kuingia katika droo ya kujishindia zawadi mbalimbali.

Akizungumza wakati wa kutambulisha zawadi hizo, Mr. Santa amesema kwa zawadi zitatolewa kwa kila mtumiaji wa airtel pamoja Mawakala wote wa Airtel.




Wednesday, December 18, 2024

TASAF WAJENGA JENGO KUTOLEA HUDUMA YA CHANJO YA MAMA NA MTOTO MAKOLE, MTENDAJI ATIA NENO

 


Na Mwandishi Wetu

UJENZI wa Jengo la kutolea huduma ya chanjo ya mama na Mtoto uliofanywa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF) katika kituo cha afya cha Makole Jijini Dodoma  umesaidia kuwezesha wananchi kupata huduma katika mazingira bora na rahisi.

Kabla ya Ujenzi wa jengo hilo wananchi wa Kata ya Makole hasa waliokuwa wakifuata huduma za Mama na Mtoto zikiwemo za chanjo walikuwa wanapatiwa huduma katika turabai lililokuwa limefungwa katika kituo hicho na kusababisha utolewaji huduma kutakuwa mazingira rafiki.

Akizungumza kuhusu ujenzi wa jengo hilo uliofanywa na TASAF , Mtendaji wa Kata ya Makole Suzan Yohana amesema kabla ya jengo kujengwa wananchi walikuwa wanapata adha kubwa ikiwemo ya kunyeshewa mvua wakati wa msimu wa mvua,vumbi lakini na kukosa hewa safi kwasababu ya ufinyu wa eneo ambalo lilifungwa turubai.

"Kata ya Makole ni kubwa sana hivyo watu walikuwa wanatoka maeneo mbalimbali kuja kupata huduma ya kliniki  ya mama na mtoto .Mazingira eneo la utoaji huduma halikuwa rafiki kwani lile turubai  halikuwa nzuri na lilikuwa halifai kwa matumizi.Kwa sasa tunashukuru tumepata jengo nzuri  na wananchi wanapata huduma katika mazingira mazuri,"amesema.

Ameongeza kuwa wanaishukuru TASAF kwani wamapeleka faraja katika huduma za mama na mtoto na kwa sasa wananchi wamekuwa wakipata huduma katika mazingira mazuri,safi na salama.

"Imekuwa faida kwetu na tunawashukuru TASAF kwa kujenga jengo hili ambalo sasa limesaidia huduma kutolewa katika mazingira bora zaidi.TASAF wamekuwa wadau wazuri sana katika kuboresha huduma hizi za mama na mtoto,"amesema Yohana.

Kwa upande wake Joyce Kimario ambaye ni Kaimu Muuguzi Mfawidhi wa Kituo cha Afya Makole Mkoani Dodoma amesema kabla ya jengo hilo la TASAF walikuwa wakitoa huduma katika mazingira magumu.

"Siku za nyuma tulikuwa tunatoa huduma ya chanjo ya mama na mtoto chini ya miaka mitano katika turubai lakini baada ya TASAF kuona mazingira yalivyokuwa mwaka jana wakatujengea jengo nzuri ambalo tunalitumia."

Wakati huo huo Muuguzi Mkunga katika kituo hicho Tumain Myeule amesema wa wanashukuru kwani wananchi wanafurahia huduma baada ya kujengwa jengo hilo na wameomba TASAF."Tunawashukuru  TASAF kwa ujenzi wa jengo hilo."

Awali Mwanakamati anayeshughulikia mpango wa walengwa wa TASAF ngazi ya mtaa  Neema Tandi amesema wananchi wa Kata ya Makole ambao ndio walengwa kwa jengo hilo wanafurahia huduma kwani huko nyuma walikuwa wakizipata katika mazingira magumu.

"Wakati kukiwa na turubai kuna muda huduma zilikuwa zinasimama kwa mfano upepo au mvua zilikuwa zinasababisha turubai linaanguka hivyo huduma zinasimama,Leo hii tumepata jengo hili ambalo limejengwa na TASAF mwaka jana,walengwa wanafurahia huduma za chanjo ya mama na mtoto."

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa Kata ya Makole wametoa pongezi kwa TASAF kwa kuona umuhimu wa kujenga jengo hilo ambalo limewezesha kuwa wanapata huduma katika mazingira mazuri ukilinganisha na ili ilivyokuwa kabla ya kujengwa kwa jengo hilo.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...