Watu saba wamepoteza maisha na wengine 10 wamejeruhiwa kwenye ajali iliyohusisha lori na Coaster eneo la Michungwani Kata ya Segera wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Alberto Msando amesema kutokana na kujirudia rudia kwa uzembe barabarani, amemwelekeza OCD kuwa atakayekiuka sheria za barabarani eneo la Handeni atafikishwa mahakamani na kupewa adhabu ya kifungo.
"Kwa ambao mmekuwa mkipiga simu kusaidiwa madereva wenu wakikiuka sheria za barabarani, wala msisumbuke. Hakuna msaada zaidi ya kukaa lock-up kwa mujibu wa sheria na kupandishwa kizimbani. Ukifika Kijiji cha Manga Wilaya ya Handeni, ewe dereva usipofuata sheria za usalama barabarani usitulaumu," amesema.