Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amesema kuwa watu zaidi ya tisa kutoka Mataifa mbalimbali ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), wamewekwa karantini chini ya ulinzi wa Mkoa wa huo baada ya kuhofiwa kuwa na maambukizi ya Virusi vya Corona.
Taarifa hiyo imetolewa leo April 1, 2020, na Mkuu wa Mkoa huo na kusema kuwa watu hao wamewekwa karantini katika baadhi ya hoteli zilizo pembezoni mwa Mji kwa muda wa siku 14 na wanahudumiwa na wahudumu ambao wamepata mafunzo maalumu.
"Tulichokifanya katika mipaka ni kuhakikisha wale wageni wote wanaoingia, wanapimwa kwanza na kukaa karantini kwa siku 14 kwa gharama zao, mpaka sasa hatuna kesi yoyote lakini tuna watu zaidi ya tisa, ambao wametengwa kwenye karantini hizo" amesema RC Chalamila.

Source