Maelfu ya Ngamia kusini mwa Australia watauawa kwa risasi kutoka kwenye helikopta kutokana na kuwepo kwa joto kali na ukame.
Zoezi hilo la siku tano limeanza Jumatano, jamii ya eneo hilo imeripoti kuwepo kwa makundi makubwa ya ngamia kuharibu miji na majengo.
"Wanaambaa mitaani wakitafuta maji ya kunywa. Tunahofukuhusu usalama wa watoto", anasema Marita Baker, ambao wanaishi kwenye jamii ya Kanypi.
Baadhi ya wanyama pori pia watauawa.Ngamia
Kwa mujibu wa BBC, Maafisa watakaofanya kazi hiyo wanatoka katika idara ya mazingira na idara ya maji.
Imeelezwa kuwa kutokana na hali ya ukame ngamia wamekuwa tishio kwenye jamii hivyo unahitajika udhibiti wa haraka.
Jamii zinazoishi karibu na makazi ya ngamia hao wamesema wamekuwa wakiishi katika mazingira magumu, kwa sababu ngamia hubomoa uzio, huzunguka nyumba wakijaribu kupata maji kupitia maji yanayodondoka kutoka kwenye viyoyozi.
Joto kali na ukame kumesababisha moto wa nyika nchini Australia kwa kipindi cha miezi kadhaa, lakini hali ya ukame ya nchi hiyo imekuwepo kwa miaka kadhaa.
Ngamia hawana asili ya Australia- walipelekwa nchini humo na walowezi kutoka India, Afghanistan na mashariki ya kati katika karne ya 19.
Ngamia hao huharibu uzio, huharibu vifaa vya shamba na makazi, na pia hunywa maji yanayohitajika kwa matumizi ya watu katika eneo hilo.
Pia hutoa gesi ya methane, gesi ambayo inachangia mabadiliko ya hali ya hewa.Maafisa wa zima motoKaribu makazi 2,000 yameharibiwa kutokana na moto uliodumu kwa miezi kadhaa.
Karibu watu 25 wameuawa tangu mwezi Septemba.
Maeneo ya mashariki na kusini mwa Australia yameharibiwa vibaya- na wanyama wengi wameuawa kwa moto.
Nchi hiyo imekuwa ikikumbwa na joto kali katika kipindi cha miongo ya hivi karibuni na hali inatarajiwa kuendelea.
Wanasayansi wametahadharisha kuwa hali ya joto kali, na ukame utachangia matukio ya moto mara kwa mara na wenye madhara .Binti wa afisa wa zima moto akiwa karibu na jeneza la baba yake