MAHAKAMA ya Angola imeagiza kukamatwa kwa mali na akaunti za benki za bilionea ambaye ni binti wa rais wa zamani wa Angola, Jose Eduardo Dos Santos, Bi Isabel Dos Santos.
Kukamatwa kwa mali hizo kunatokana na mipango ya serikali iliyopo kukabiliana na ufisadi katika taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta.
Utawala wa Rais Joao Lourenco unataka kuchukua takriban dola bilioni moja ambazo umekuwa ukimdai Bi Isabel Dos Santos na washirika wake.
Amepinga madai hayo na kusema kwamba hajafanya makosa yoyote wakati babake alipokuwa mamlakani.
Akidaiwa kuwa mwanamke tajiri zaidi barani Afrika, Bi Dos Santos anakadiriwa na jarida la Forbes kuwa na mali yenye thamani ya dola bilioni 2.2.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 46 anaishi ughaibuni, akisema kwamba aliondoka Angola kwa kuwa maisha yake yalitishiwa.
Anaendesha biashara kubwa akiwa na kampuni nchini Angola na Portugal ambapo anamiliki hisa katika kampuni ya Nos SGPS.
Mahakama iliagiza mali ya Bi Santos kupigwa kuchukuliwa ikiwemo akaunti zake za benki mbali na hisa zake katika kampuni nchini Angola, ikiwemo ile ya Unitel na Benki ya Fomento de Angola (BFA) kilisema chombo kimoja cha habari cha serikali ambapo naye alisema anashutumu kile alichokitaja kuwa shambulio linaloshinikizwa kisiasa.