Monday, January 13, 2020

Chama Cha Wamiliki wa Mabasi (TABOA) mbioni kuanza kukatisha tiketi Kielectroniki



Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma

Chama cha wamiliki wa mabasi nchini (TABOA)kimesema kipo katika hatua nzuri kukamilisha zoezi la  kuanza kukatisha tiketi kwa njia ya kielektroniki  ili kupunguza msongamano na usumbufu kwa abiria hasa wakati wa msimu wa sikukuu.

Akizungumza na Muungwana blog Katibu wa TABOA Enea Mruto amesema baada ya kikao chao na mamlaka ya mapato nchini TRA kufikia makubaliano  taratibu za ukatishaji tiketi kwa njia ya elektroniki unaarajia kuanza mwezi ujao kwa mabasi yote.

"Kama TRA hawatatuangusha kile tulichokubaliana nao basi mpango huo utaanza rasmi mwezi ujao tunahitaji kufanya kazi kwa kwenda na teknolojia mpya kuondoa usumbufu kwa wateja wetu "amesema Mruto.

Amesema wakakamilisha baadhi ya taratibu mpango huo utazinduliwa rasmi na kuwekwa agizo kwa mabasi kuanza kutumia njia hiyo ambayo inawarahisishia wateja kupata tiketi rahisi au kuweka booking kwa njia ya mtandao.

Amesema licha ya kuwa baadhi ya kampuni zimejaribu kuanza mpango huo ila rasmi itakuwa mwezi ujao kwa mabasi yote kuanza kutumia mfumo huo utakao warahisishia wateja wao kupata tiketi kwa njia salama.

Akizungumzia agizo la Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye,  kuhakikisha mabasi yote yasiyokuwa na vibali kusafirisha vifurushi.

Amesema hata katika mkutano wao wamiliki walisisitiza agizo hilo ili kuendana na Sheria zinavyohitaji na kwenda sambamba na Serikali inavyoagiza.

"TABOA tunatekeleza agizo hilo atakayekiuka atakupambana na mkono wa sheria hivyo kila mmoja anapaswa kutekeleza sheria, "amesema.

Katika hatua nyingine Mrutu amesema moja ya mikakati waliojiwekea ni kuhakikisha wanapunguza ajali za barabarani kwa kuhimiza umakini katika kampuni za mabasi hususa ni kwa madereva kutii Sheria na taratibu zilizowekwa.

Amesema wao kama TABOA watakuwa wakisisitiza wamiliki wa mabasi kufanya ukaguzi katika vyombo vyao vya moto ili kunusuru ajali zinazotokea mara kwa mara.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...