Tuesday, July 2, 2019

Tundu Lissu aeleza sababu ya kutomwandika barua Spika Ndugai


Aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ameeleza sababu ya kutomwandika barua spika wa Bunge, Job Ndugai kumjuliusha kuwa yupo nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

Wiki iliyopita Spika Ndugai alitangaza kumvua ubunge Lissu kwa kile alichoeleza kuwa kiongozi huyo hajulikana halipo zaidi ya kuonekana nchi za Ulaya na Marekani.

"Ni kweli sijawahi kumuandikia Spika Ndugai barua yoyote kuhusu mahali nilipo, na hali yangu ya
kiafya. Sikumwandikia, sio kwa sababu nilisahau au nilipuuza, bali ni kwa sababu Spika Ndugai alikuwa anafahamu fika mahali nilipo, na sababu za mimi kuwa huko," amesema Tundu Lissu.

Ameendelea kwa kusema, "Kwa sheria na taratibu za Bunge, Spika na watendaji wake wanawajibika kufuatilia hali ya mbunge anayetibiwa nje ya nchi, na kutoa taarifa za maendeo yake. Sio wajibu wa mbunge mgonjwa kulitaarifu Bunge juu ya afya yake. Ndugai alipaswa kujua nilipo, na maendeleo yangu." Lissu,".

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...