Tuesday, July 2, 2019

Weusi wajibu tuhuma za kumtenga producer Luffa

Wasanii wanaounda kundi la Weusi, wameibuka na kuweka mambo sawa kuhusiana na tuhuma zilizokuwepo mtaani kuwa wamemtenag producer Luffa baada ya kuumwa.

Akiongea na eNewz ya East Africa Television leo, Gnako amesema watu wanaosema hayo meneno hawajui lolote kuhusu kuumwa kwa Luffa.

''Unajua watu wanaongea tu lakini siku ya kwanza Luffa ameumwa mimi na Lord Eyez ndio tulimpeleka hospitali na bado tunafuatilia maendeleo yake'', amefunguka Gnako.

Mkali huyo wa Chorus ameongeza kuwa kwasasa Luffa yupo hospitali ya Lugalo anaendelea na matibabu ambapo kuna oparesheni anatakiwa kufanyiwa.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...