UONGOZI wa Yanga umekamilisha taratibu za usajili wa beki wa kushoto wa Rayon Sports ya Rwanda, Ericky Rutanga anayejiunga na timu hiyo kwenye usajili wa dirisha dogo Ligi Kuu Bara maalum kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Awali, Yanga iliwahi kumfuata beki huyo na kuzungumza naye na kushindwa kufikia muafaka mzuri na kusalia Rayon huku Gadiel Michael aliyekuwa akicheza nafasi hiyo, naye akitimkia Simba.
Yanga mara baada ya kushindwana na beki huyo haraka ikakamilisha usajili wa beki wa Singida United, Muharami Salum maarufu kwa jina la Marcelo ambaye tayari yupo kambini mkoani Morogoro.
Yanga msimu ujao itashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika iliyo chini ya Shirikisho la Soka Afrika 'Caf' ambapo itaanzia hatua ya awali iliyopangwa kuanza Agosti 9, mwaka huu na michuano hiyo itamalizika Mei 30, mwakani.
Hivyo basi kama itafanikiwa kushinda mechi za awali za mtoano na kutinga hatua ya makundi, basi itapewa nafasi ya kuongeza wachezaji. Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumamosi, Rutanga rasmi atajiunga na Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo akiwa kama mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika.
Habari zinasema kwamba beki huyo atajiunga na Yanga katika usajili huo kuchukua nafasi ya mchezaji wa kigeni, Klaus Kindoki aliyekataa kutolewa kwa mkopo huku akisubiria mkataba wake kumalizika kipindi hicho.
"Rutanga tayari amemalizana na Yanga kwa asilimia 70 na anajiunga nayo kwenye usajili wa ligi na atakuja kuchukua nafasi ya Kindoki ya wachezaji wa kigeni.
"Kama unavyofahamu nafasi za wachezaji wa kigeni tayari zimefikia kumi kama idadi ambao TFF wanaitaka, hivyo wakati Kindoki anaondoka baada ya mkataba wake wa miezi sita kumalizika na Rutanga atakuwa amekuja Yanga.
"Kikubwa uongozi unataka kuwa na mchezaji mwenye uzoefu na uwezo wa michuano ya kimataifa ambayo Yanga watashiriki, mwaka huu," alisema mtoa taarifa huyo.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali shauri lililokuwa limefunguliwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...