Wednesday, October 31, 2018

Idadi ya Watu Wanaotumia Mtandao wa Facebook yapungua

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na mtandao wa kijamii wa Facebook idadi ya watu wanaotumia mtandao huo imepungua.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Facebook imetoa takwimu kuwa watu bilioni 1.49 walitumia mtandao huo mwezi Septemba ikiwa ni chini ya idadi lengwa ya watu billioni 1.51.

Aidha kiwango cha ukuaji kilipungua zaidi katika mataifa ya Magharibi ambayo ni Marekani, Canada na bara la Ulaya.

Kwa upande mwingine mtandao huo wa Facebook umeshuhudia ukuaji wa mitandao yake ya kijamii ya WhatsApp na Instagram.

Yametimia! Hatimaye Issac Gamba Azikwa Nyumbani Kwao Bunda

Yametimia! Hatimaye Issac Gamba Azikwa Nyumbani Kwao Bunda
SIMANZI NA MAJONZI vimetawala wakati mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle (DW) nchini Ujerumani, Isaac Muyenjwa Gamba ukizikwa kwenye makaburi ya familia yao, leo Jumatano, Oktoba 3i, 2018, Bunda mkoani Mara.

Zitto Kabwe atolewa Oysterbay apelekwa Central Polisi kuhojiwa zaidi, uchochezi watajwa (+video)

Baada ya kuhojiwa kwa takribani saa nne katika kutuo cha polisi Oysterbay jijini hapa, Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amehamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi kwa mahojiano zaidi. Akiongea na Waandishi wa Habari muda mfupi baada ya Zitto kutolewa kituo cha Oysterbay, Katibu Mwenezi wa ACT Wazalendo amesema kuwa kiongozi wao …

The post Zitto Kabwe atolewa Oysterbay apelekwa Central Polisi kuhojiwa zaidi, uchochezi watajwa (+video) appeared first on Bongo5.com.


Source

Picha : LHRC YAENDESHA WARSHA KWA WAANDISHI WA HABARI MIKOA MBALIMBALI KUHUSU MASUALA YA HAKI YA KUPATA NA KUTOA TAARIFA

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (Legal and Human Rights Centre - LHRC) kimeendesha warsha kwa waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari juu ya sheria mbalimbali zinazoathiri tasnia ya habari nchini Tanzania na kimataifa.

Warsha hiyo ya siku tatu imeanza leo Oktoba 31,2018 na itamalizika Novemba 2,2018 inafanyika katika Ukumbi wa Morogoro Hotel mkoani Morogoro.

Awali akizungumza katika warsha hiyo,Afisa Mradi wa Kuongeza nafasi ya ushiriki wa wananchi Tanzania unaosimamiwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Fortunata Ntwale alisema warsha hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi huo.

Alisema kupitia warsha hiyo ya siku tatu,waandishi wa habari watapata fursa ya kubadilishana uzoefu juu ya sheria na kanuni zinazoratibu haki ya kupata na kutoa taarifa.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Afisa Mradi wa Kuongeza nafasi ya ushiriki wa wananchi Tanzania unaosimamiwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Fortunata Ntwale akizungumza wakati wa warsha
kwa waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari juu ya sheria mbalimbali zinazoathiri tasnia ya habari nchini Tanzania na kimataifa.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mwanasheria wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu -LHRC, William Kahale akizungumza wakati wa warsha hiyo.
Afisa Utetezi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu -LHRC, Raymond Kanegene akiandika mwongozo wakati wa warsha hiyo.
Mwanasheria wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu -LHRC, William Kahale akitoa mada kuhusu sheria.
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini.
Warsha inaendelea.
Washiriki wakiwa ukumbini.
Mwanasheria wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu -LHRC, William Kahale akiendelea na mada ukumbini.
Kulia ni Mkurugenzi wa Malunde1 blog,Kadama Malunde akizungumza wakati wa warsha hiyo.
Mwanasheria wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu -LHRC, William Kahale akitoa mada ukumbini.

MKUU WA MKOA ATOA SIKU TANO WANANCHI WAFUTE PICHA ZA NGONO KWENYE SIMU ZAO

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewataka wakazi wa Dar es salaam kufuta video na picha za ngono zote walizonazo kwenye simu zao, ili kujiepusha kukumbana na rungu la TCRA.


Mh. Makonda ametoa wito huo leo alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari, na kusema kwamba ipo siku TCRA watafanya ukaguzi kugundua nani anahusika na kuvujisha video za ngono mitandaoni, na itakuwa aibu iwapo mtu mzima au kiongozi wa serikali kukutwa nazo.


"Naomba kabla ya Jumatatu wewe Mwana Dar es salaam uliyeweka picha za ngono kwenye simu yako, naomba zifute, TCRA wana uwezo mkubwa wa kufuatilia, heri wafuatilie wakute zilikuwepo lakini zimefutwa, na vile vile unaweza ukajisahau ukaacha simu bila kuweka password mtoto akachukua simu kucheza game, akakutana na picha za ngono, ni aibu", amesema Paul Makonda.


Leo Mh. Makonda aliitisha mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia mkakati wake wa kukomesha ushoga na biashara ya ngono jijini Dar es salaam ambapo ametangaza kuunda kamati ya kufuatilia vitendo hivyo, ambayo amevitaja kulipa laana taifa.

Ommy Dimpoz Uso kwa Uso na Zari

Mwanamama Zari the bossy amekutana uso kwa uso na msanii Ommy dimpoz ambae hapo awali iliwahi kuripotiwa lkuwa alikuwa na bifu na mwanaume aliyezaa  watoto na mwanamama huyo. Hata hivyo Zmmy na zari wamekutana nchini afrika ya kusini ambapo ndipo kuna makazi maarum ya zari na familia yake na pia ndio kumekuwa makazi ya ommy dimpoz kwa sasa na uongozi wao. Hata hivyo haijafahamika sana kuwa wawili hao walikutana kwa sababu ya tukio gani lakini imekuwa ikionekana kuwa mkutana wao umekaa kikazi zaidi. Ikumbukwe kuwa pindi cha mahusiano ya Zari na Diamond  hakukuwa na ukaribu kati ya Ommy na zari na picha hiyo imezua gumzo kwa sababu ya mahusiano yaliyopo kati ya diamond na Ommy.

The post Ommy Dimpoz Uso kwa Uso na Zari appeared first on Ghafla!Tanzania.


Source

WAANDISHI WA HABARI WAFUNZWA KUHUSU MAZINGIRA

Mabadiliko ya Tabia nchi duniani yanatanjwa kuwa tatizo sugu linalozikumba nchi mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania nakuleta athari sektambalimbali ikiwemo ya wanyamapori. Akizungumza na waandishi wa habari wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani katika wa mafunzo yaliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari  za Mazingira (JET) kwa ufadhiliwa wa Shirika la Misaada la Marakeni (USAID Protect), Mtaalamu wa […]
Source

TRA YAGAWA MAKONTENA YA MAKONDA KIMYA KIMYA



Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeyagawa 'kimya kimya' makontena 20 ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda yaliyokuwa yakishikiliwa na mamlaka hiyo.

Septemba 5, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa mamlaka hiyo, Richard Kayombo alieleza kuwa iwapo uamuzi wa kuyagawa makontena hayo utafanyika, taasisi zitakazogawiwa zitajulikana.

Hata hivyo, wakati ikisubiriwa kujulikana kwa taasisi hizo, Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere amesema tayari makontena yamekwishagawiwa.

Makontena hayo ambayo yalikosa wanunuzi katika minada yote mitatu iliyoendeshwa na kampuni ya udalali ya Yono yalikuwa na samani za viti, meza na mbao za kuandikia yakidaiwa kodi inayokadiriwa kufikia Sh1.2 bilioni.

Via>>Mwananchi

State telco to send home 600

TTCL Corporation plans to retrench more than 600 workers as part of cost-cutting measures.
Source

Zitto aitwa Polisi Kuthibitisha madai ya mauaji ya watu 100 Kigoma

Zitto aitwa polisi kuthibitisha madai ya mauaji ya watu 100 Kigoma
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma limemtaka mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe kuwasilisha vielelezo vya madai  yake kuwa yametokea  mauaji eneo la Nguruka wilayani Uvinza mkoani humo na watu 100 kupoteza maisha.

Jumapili iliyopita Oktoba 28,2018, Zitto alizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kudai kuwa takribani siku 10 zilizopita yalitokea mauaji hayo na taarifa alizonazo ni kuwa watu  zaidi ya 100,  wakiwamo polisi walikufa.

Jana Jumanne, Oktoba 30, 2018, Kamanda wa polisi mkoani Kigoma, Martin Ottieno alizungumza na waandishi wa habari na kusema tuhuma alizotoa Zitto hazina ukweli wowote.

Alisema  hakuna  watu 100 waliouawa na kusisitiza kuwa ni upotoshaji unaofanywa na wanasiasa.

"Hakuna watu mia moja waliouawa. Tunamtaka Zitto aonyeshe vielelezo vya hayo anayosema au aje atuonyeshe makaburi ya watu hao anaosema wameuawa Kigoma, "alisema Ottieno.

Kamanda huyo amewataka  wanasiasa kuchukua tahadhali  kwa taarifa wanazopewa na watu mbalimbali kabla ya kuzisambaza ili kuepuka kupotosha jamii.

Rayvanny atoa wito kwa wasanii ‘kidogo tunachopata, tusaidie ndugu zetu wenye Magonjwa’

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva kutoka WCB, Rayvanny amewataka Watanzania wenye uwezo kwajitoe japo kidogo kuwasaidia wagonjwa wanaosumbuliwa na maradhi mbalimbali Hospitalini. Rayvanny amesema hayo, baada ya jana kutembelea katika Hospitali ya Muhimbili kumjulia hali mama  aliyekuwa anasumbuliwa na jicho kutoka Mbeya, ambaye wiki iliyopita video zake zilisambaa mtandaoni zikimuonesha akiomba msaada wa matibabu. …

The post Rayvanny atoa wito kwa wasanii ‘kidogo tunachopata, tusaidie ndugu zetu wenye Magonjwa’ appeared first on Bongo5.com.


Source

Tuesday, October 30, 2018

Khassim Mganga Awaponda Wanaoweka Matangazo Kwenye Akaunti za Wasanii.

Msanii Khassim Mganga amefunguka na kusema tabia inayomkera katika utumiaji wa mitandao ya kijamii ni pale ambapo watu hutumia  kurasa za wasanii kufanya matangazo ya biaashara bila kuwa na ridhaa ya wenye kurasa husika. Akiongea katika mahijiano , khassim mganga anasema “utamkuta mtu  unaweka kazi zako katika ukurasa wako lakini anatokea mtu miwngine huko anaweka matangazo , tena hata haangalii aina ya tangazo  yeye anaweka” Anasma khassim. Hata hivyo hii imekuwa ni tabia ya watu wengi kutumia page za mastaa na kuweka matabgazo yaoya biashara bila kuwa na ruhusa ya mwenye akaunti hiyo na hii imekuwa ikiwakwaza wasanii wengi hata kuamua kutoruhusu sehemu ya kupokea maoni kitu ambacho pia kinawa-cost muda mwingine. khassim ni moja ya wasanii wanaosifika kwa nyimbo za mahaba  na ni moja ya wasanii wa bongo walioanza muziki muda mrefu nyuma anaeweza kuingia kwenye historia ya kukuza mudziki wa bongo.

The post Khassim Mganga Awaponda Wanaoweka Matangazo Kwenye Akaunti za Wasanii. appeared first on Ghafla!Tanzania.


Source

Mwili wa Issac Gamba Wawasili kwao Bunda Vilio vyatawala

Mwili wa Issac Gamba Wawasili kwao Bunda Vilio vyatawala
VILIO, simanzi na simanzi vimetawala wakati mwili wa wa aliyekuwa mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle (DW) nchini Ujerumani, marehemu Isaac Muyenjwa Gamba ukiwasili nyumbani kwao, Bunda Mkoa wa Mara kwa mazishi.


Wakati wa kuwasili kwa mwili huo, ndugu, jamaa na marafiki wameshindwa kuzuia hisia kwa mpendwa wao huyo, na kujikuta wakiangua vilio huku wengine wakiishiwa nguvu na kupoteza fahamu, hakika inasikitisha.


Mwili wa gamba ambao umewasili Bunda leo ukitokea Mwanza baada ya kuagwa asubuhi katika viwanja vya Umoja wa Vyama vya Waandishi wa Habari (UPTC) jijini humo, utazikwa kesho majira ya saa 5 asubuhi nyumbani kwao, Bunda.

DIWANI WA CHADEMA APIGWA MARUFUKU KUHUDHURIA VIKAO AKIMTUHUMU MKURUGENZI KUPIGA VIWANJA..RC SHINYANGA AONYA


Diwani wa Kata ya Ngokolo (CHADEMA) manispaa ya Shinyanga Emmanuel Ntobi.



Diwani wa kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga Emmanuel Ntobi, amesimamishwa kutohudhuria vikao vitatu vya baraza la madiwani, kutokana na utovu wa nidhamu kwa kumtuhumu ndani ya baraza mkurugenzi wa manispaa hiyo Geofrey Mwangulumbi kujimilikisha viwanja Vinane kinyume na taratibu.


Maamuzi hayo yametolewa leo Oktoba 30,2018 kwenye kikao cha baraza la kawaida la madiwani hao, wakati ikitolewa taarifa ya kamati ya maadili juu ya diwani huyo kuwa kwenye baraza lilopita alitoa tuhuma kuwa mkurugenzi anajimilikisha viwanja, na hivyo kushindwa kudhibitisha hoja yake hiyo na kuamuliwa kusimamishwa.


Akisoma taarifa ya kamati hiyo ya maadili, Naibu Meya wa manispaa ya Shinyanga John Kisandu, alisema kutokana na diwani huyo kushindwa kuthibitisha ukweli wa kauli yake hiyo, pamoja na kuitwa kwenye kamati kushindwa kuhudhulia na kutotoa maelezo, hivyo wameadhimia kumsimamisha kutohudhulia vikao vitatu na kunyima stahiki zake zote.


"Kanuni ya 28 kipengele cha tatu za kanuni za kuduma za halmashauri (2013) namba mbili, kinasema endapo mjumbe aliyetoa hoja za kashfa akakataa kufuta kauli yake kwa kuomba msamaha kwa maadishi kama alivyoelekezwa na kamati ndogo, Meya wa mkutano atamsimamisha mjumbe huyo kutohudhulia vikao vitatu,"alisema Kisandu


"Mjumbe aliyesimamishwa kwa mujibu wa kanuni hiyo atapoteza haki zake za posho, nauli na kulelewa na kinga kwa muda wote wa kusimamishwa kwake, kutoka na kusema uongo ndani ya baraza,"aliongeza.


Naye mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack, ambaye alihudhuRia kwenye baraza hilo aliunga mkono maamuzi hayo, na kusema kwamba madiwani ambao wataendelea kuwa na utovu wa nidhamu kwenye vikao na kutoa taarifa za uongo na kuleta migogoro, wanapaswa kushughulikiwa.


Alisema kinachopaswa madiwani ni kuwa wamoja na kujadili masuala ya maendeleo ya manispaa hiyo ambayo yapo nyuma, na siyo kuanza kutafuta marubano yasiyo na tija yatakayo kwamisha kujadili mambo ya msingi kwa ajili ya mustakabali wa manispaa hiyo.


Pia alitoa onyo kwa watumishi wa Serikali ambao wamekuwa hawatunzi siri na kuanza kuzitoa hovyo nje hasa kwa wanasiasa, ambao nao wamekuwa wakizianika kupitia mitandao ya kijamii, kuwa atakaye bainika watamshughulikia kisheria ikiwa hata faa tena kuwa mtumishi wa umma.


Kwa upande diwani huyo wa Chadema Emmanuel Ntobi, ambaye hakuwepo kwenye kikao akizungumza na Malunde 1 blog kwa njia ya Simu, alisema hajaridhia maamuzi hayo ikiwa kauli yake ni ya kweli na hajapokea barua yoyote ya kusimamisha kwenye baraza, ambapo kesho atahudhulia kikao hicho.


TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Naibu Meya wa manispaa ya Shinyanga John Kisandu akisoma taarifa ya kamati ya maadili pamoja na vifungu vya kanuni ambayo vimesababisha diwani huyo wa Kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi kusimamishwa kutohudhulia vikao vitatu mfululizo vya baraza la madiwani sambamba na kukosa stahiki zake zote kipindi amesimamishwa.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack akizungumza kwenye baraza hilo na kuwataka madiwani wawe na umoja na kuacha masuala ya kuichafua halmashauri kupitia mitandao ya kijamii bali waijenge manispaa hiyo ili kuiletea maendeleo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza kwenye baraza la madiwani, na kuwataka, wamalize miradi ambayo ni viporo,kuhamasisha usafi kwa wa mazingira kwa wananchi, kumaliza uhaba wa madawati mashuleni, na mikopo kwa akina mama,vijana na walemavu.
Madiwani wa mansipaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikoa chao cha kawaida wakijadili ajenga mbalimbali kwa ajili ya Mustakabali wa manispaa hiyo.
Baraza la madiwani likiendelea.
Diwani wa Kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga David Nkulila kichangia mada kwenye kikao cha baraza.
Mkurugenzi wa mansipaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi akijibu maswali kwenye baraza hilo.
Madiwani wakiendelea na kikao cha baraza.
Diwani wa Viti maalumu CCM Shela Mshandete akichangia hoja kwenye baraza la madiwani.
Diwani wa Kata ya Masekelo manispaa ya Shinyanga Samweli Sambayi akichangia hoja kwenye baraza .
Diwani wa Kata ya Mwawaza manispaa ya Shinyanga Juma Nkwabi akichangia hoja kwenye baraza.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack mkono wa kulia akiwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko kwenye kikao cha baraza la kawaida la madiwani wa manispaa ya Shinyanga.
Watumishi wa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye baraza la madiwani.
Watumishi wa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye baraza la madiwani.
Wachukua kumbukumbu (CC) wa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye baraza la madiwani wakiandika ndondoo za kwenye baraza hilo.

Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog.

Dkt. Mengi kuja na smartphone zinazokaa na chaji wiki nzima soma hapa



Kampuni ya IPP imetangaza kuanza ujenzi wa kiwanda cha kwanza cha kutengeneza simu janja maarufu kama smartphone, simu zitakazokuwa na uwezo wa kukaa na chaji kwa muda wa wiki moja na kwa wasiokuwa na umeme wanaweza chaji kwa nguvu ya Jua.



Kiwanda hicho kitakachokuwa cha kwanza nchini na Afrika Mashariki, kitajengwa eneo la Mikocheni jijini Dar es salaam, ambapo uwekezaji wake ukikadiriwa kuwa ni shilingi bilioni 11 na kitaanza uzalishaji ndani ya miezi mitatu ijayo, kikitarajia kuajiri takribani watu elfu mbili.

Akizungumza na wanahabari Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi amesema kiwanda hicho kitakuwa na mchango mkubwa kwenye uchumi na sehemu kubwa ya watakaoajiriwa ni watu wenye ulemavu.

"Simu zitakazotengenezwa na IPP TouchMate zitakuwa na uwezo wa kukaa na chaji kwa muda wa wiki moja na lengo litakuwa ni kuendana na mazingira ya maisha halisi ya Tanzania", amesema Dkt. Mengi. Tayari ufungaji mitambo kwenye kiwanda hicho kitakachojulikana kama IPP TouchMate umeshaanza ambapo mbali ya simu, bidhaa nyingine zitakazotengenezwa ni pamoja na Tablet, Kompyuta mpakato, headphones pamoja na bidhaa za kielektroniki za majumbani pamoja na vipuri vyake.


SOURCE:EATV
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...