Saturday, February 23, 2019

RASMI: Hans Van Der Pluijm atimuliwa Azam FC, kipigo cha Simba champonza na huyu ndiye mrithi wake

Kocha mkuu wa klabu ya Azam FC, Hans Van Der Pluijm ametimuliwa kazi ya kuendelea kuinoa timu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Chamazi jijini Dar es salaam. Mbali na Pluijm kocha msaidizi naye Juma Mwambusi amefungashiwa virago huku, Ettiene Ndayiragije wa KMC akitarajiwa kurithi mikoba hiyo kwa muda. Kutimuliwa kazi kwa Pluijm kunatokana na …

The post RASMI: Hans Van Der Pluijm atimuliwa Azam FC, kipigo cha Simba champonza na huyu ndiye mrithi wake appeared first on Bongo5.com.


Source

Familia ya Michael Jackson imeishtaki kampuni ya HBO na kuidai fidia ya US mil 100 , kwa kurusha documentary ya inayoonyesha vitendo vya ulawiti dhidi ya watoto wadogo

Familia ya Michael Jackson imeishtaki kampuni ya televisheni ya HBO kwa kuvunja makubaliano ya mwaka 1992. Michael na HBO walisaini mkataba wa siri (NDA) mwaka huo kwa ajili ya kurusha documentary ya ‘Michael Jackson Live in Concert in Bucharest: The Dangerous Tour 1992’ – hii ilikuwa kulinda kutovujishwa kwa taarifa zozote kati ya pande zote mbili …

The post Familia ya Michael Jackson imeishtaki kampuni ya HBO na kuidai fidia ya US mil 100 , kwa kurusha documentary ya inayoonyesha vitendo vya ulawiti dhidi ya watoto wadogo appeared first on Bongo5.com.


Source

MDEE AITWA POLISI

Mbunge wa Kawe (Chadema), Halime Mdee ameitikia wito wa Polisi Kinondoni jijini Dar es Salaam aliotakiwa kufika leo Jumamosi Februari 23,2019.

Mdee kupitia akaunti yake ya Twitter ameandika, "Nimepata wito wa kuitwa Polisi Oysterbay kwa mahojiano."

"Mpaka sasa sababu ya wito ni nini. Ngoja tujongee."

Baada ya ujumbe huo, Mwananchi limezungumza na Mdee ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) kujua kama amekwisha kufika na kujibu kwa ujumbe mfupi wa maandishi, "Niko kwa RCO. Nimepokelewa, Namsubiri."
Chanzo - Mwananchi





Ruge Amekuwa na Nafasi Nyingi Sana Katika Maisha Yangu :-Nandy

Msanii wa bongo fleva nchini NANDY,  amefunguka na kusema kuwa  Mkurugenzi wa Clouds media , Ruge mutahaba amekuwa aki-play party kubwa sana katika maisha yake kiasi kwamba hata ugonjwa na magumu anayoyapitai sasa hivi yamekuwa yakimuumiza sana. Nandy ameongea hayo alipokuwa akihojiwa na Clouds Media leo na kusema kuwa Ruge amekuwa ama bosi, kama kaka na kama baba kwake kwa sababu katika kazi zae za muziki bila Ruge basi hajui yeye mpaka sasa angekuwa wapi. Hata hivyo haya yote yanakuja bada ya nandy kugombana na kujibizana na  msanii mwenzake Dudu baya ambae aliamua kusema kuwa kama Ruge ni mgonjwa na anahitaji msaada hakuna haja ya kumsaidia kwa sababu alishadhulumu wasanii wengi sana. Amekuwa akiplay party kubwa sana katika maisha yangu sio kimuziki tu , lakini hata katika maisha.tukiangalia hapa nilipo sababu ni yeye, ukiacha nafasi ya wazazi wangu nafasi inayofuata ni yeye, kwangu yeye ni kama bosi, kaka na kama baba. Akiongea huku analia, Nandy anasema kuwa mara nyingi amekuwa akikwama na anawaza kabisa kuwa tatizo kama hili angekuwepo Bosi Ruge angeweza kulitauta lakini anaona kabisa kuna kitu kinapotea.    

The post Ruge Amekuwa na Nafasi Nyingi Sana Katika Maisha Yangu :-Nandy appeared first on Ghafla! Tanzania.


Source

Hizi ndiyo njaa mbili zinazowasumbua wanandoa katika Maisha yao ya ndoa


Habari rafiki na mpenzi msomaji wa Amka Mtanzania? Na karibu tena katika makala yetu ya leo ili tuweze kujifunza. Katika makala yetu ya leo tutajifunza njaa zinazowasumbua wanandoa katika maisha yao ya ndoa. Kuzifahamu njaa zinazowasumbua wanandoa tafadhali twende sanjari mpaka mwisho wa makala hii.

Kumekuwa na mitazamo hasi sana juu ya maisha ya ndoa. Kabla mtu hajaingia ndani ya maisha ya ndoa tayari akili yake imeshajazwa mitazamo hasi juu ya maisha ya ndoa. Mtu aliyepatwa na matatizo katika maisha yake ya ndoa naye atakwenda kuwaaminisha watu juu ya matatizo yake juu ya ndoa. Siyo kwamba katika maisha ya ndoa hakuna changamoto la hasha zipo kama kawaida kama vile kwenye kazi, biashara, ujasiriamali nakadhalika. Hivyo kwenye jambo lolote changamoto haziepukiki. Kweli itakuweka huru na usipoujua ukweli utapata shida sana.

Maisha ya ndoa unayotaka kuishi unayatengeneza wewe mwenyewe na si vinginevyo hivyo usipoteze muda wa kuhangaika tengeneza yale maisha ambayo unayataka kuishi na usisikilize kelele za watu ambazo zitakuwekea ukungu katika macho yako na kushindwa kuona mbele. Na waswahili wanasema ukiona vyaelea ujue vimeundwa kwa hiyo, hata wewe unaweza kuviunda katika maisha yako ya ndoa.
 
Katika hali ya kawaida hakuna mtu asiyeijua njaa, mtu akiwa na njaa anapoteza kabisa nguvu na hata ufanisi wa kazi aliyokuwa anafanya unapotea, kwa hiyo njaa huwa inalegeza watu kama akikosa kula chakula na kushiba. Vivyo hivyo, kila mwanandoa ana njaa yake yaani mwanaume ana njaa yake katika maisha ya ndoa hali kadhalika kwa mwanamke naye ana njaa yake. Kwa maana hiyo, kila mwanandoa anahitaji ashibishwe njaa yake na mwenza wake.

Ikitokea sasa wanandoa hao yaani wawili hao kutoshibishana njaa zao ndio matatizo huanzia hapo. Na tunajua ya kwamba wawili hao kila mmoja ana njaa yake. Hivi ikitokea mtu ana njaa ya chakula halafu pale anapotegemea kupata chakula ili ashibishe njaa yake hapati ataendelea kusubiri kubaki na njaa yake? Jibu ni kwamba lazima atatafuta sehemu ambayo ataweza kupata chakula ili aweze kushibisha njaa yake.

Ndugu msomaji, kama kila mwanandoa ameshindwa kumshibisha mwenzake basi ujue lazima atatafuta chakula sehemu nyingine ili kuweza kukidhi njaa yake. Hivyo basi, kumbe ni wajibu wa kila mwanandoa kuhakikisha anamshibisha mwenzake njaa yake.
 
Zifuatazo ni njaa mbili zinazowasumbua wanandoa endapo hawatashibishana; 

1. Njaa ya mwanamke ni upendo;
Mwanamke anahitaji upendo kuliko vitu vingine, hata katika vitabu vya dini vinasema; enyi waume, wapendeni wake zenu. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe, mwanaume anatakiwa kujitoa kwelikweli kumpenda mke wake kama tunavyojua upendo ndio falsafa kubwa sana katika maisha ya binadamu, upendo huvumilia, hufadhili, hauhusudu. Hivyo basi njaa ya mwanamke ni kupendwa. Wewe kama mwanaume unatakiwa kumpenda mke wako kwa moyo wako wote bila kujali udhaifu wake. Hii ndio njaa ya wanawake wanahitaji upendo katika maisha ya ndoa.
  
2. Njaa ya mwanaume ni kuheshimiwa; 
Mwanaume njaa yake kubwa ni kuheshimiwa katika maisha ya ndoa. Sasa ikitokea mwanaume anakosa kuheshimiwa na mke wake katika maisha ya ndoa hivyo anakuwa amekosa kushibishwa njaa yake. Na kama akikosa kushiba ndio matatizo huanzia hapo itamlazimu kutafuta kushibishwa njaa yake nje. Hivyo kama wewe ni mwanamke unatakiwa kumshibisha mume wako njaa yake ya kumtii.
  
Kama wanandoa wanashindwa kushibishana njaa zao, hivyo wanajitengenezea shimo wao wenyewe. Watu wanajisahau sana katika kutimiza majukumu yao katika maisha ya ndoa hatimaye wanaruhusu haki za kibinadamu kuingia maisha ya ndoa, kama wanandoa mkishaingiza haki za kibinadamu katika maisha ya ndoa yaani hamsini kwa hamsini kama wanavyodai lazima mtapoteza mwelekeo tu. Kwa hiyo kila mtu ana njaa yake kama tulivyoona hapo juu sasa mkishayaingiza mambo haya ya kidunia mtakosa kushibishana njaa zenu.
Source

Watoto wawili wa Darasa moja wafariki kwa kujinyonga


Wanafunzi wawili wa Darasa la tano Shule ya Msingi Mikiroy Magugu Mkoani Manyara waliokuwa wanakaa Dawati moja wamefariki dunia katika matukio yanayofanana, wa kwanza alifariki Mwezi Januari mwaka huu kwa kujinyonga, mwingine amejinyonga februari 20.

Mwanafunzi huyo (11) wa darasa la tano Shule ya Msingi Mikiroy kijiji cha Magugu kata ya Magugu Wilaya ya Babati Mkoani Manyara amejinyonga kwa taulo hadi kufa.

Akizungumza na MUUNGWANA BLOG Mtendaji wa Kijiji cha Magugu Leonsi Daniel Lumbu  ameeleza kuwa  tukio hilo limetokea Februari 20 mwaka huu baada ya mwanafunzi huyo kutoka Shuleni majira ya Jioni ambapo hakuwakuta wazazi wake ndipo alipoenda kwa jirani kuchukua ufunguo na kuingia ndani na kujinyonga kwa taulo hadi kufa.

Amesema ni mtoto ambaye anaishi na Mama yake ambaye ameolewa na mwanaume mwingine huku baba yake mzazi akimuacha tangu alipokuwa na miaka miwili baada ya kufarakana.

Mtendaji huyo amemtaja Mwanafunzi huyo kuwa ni Mathayo Ezekiel huku akieleza kwamba Sio tukio la kwanza kutokea kwani January mwaka huu 2019 mwenzake waliokuwa wanasoma darasa moja na kukaa katika Dawati moja naye alikufa kwa kujinyonga hali iliyowaacha wengi midomo wazi wakijiuliza kulikoni?

Amewataka Wazazi kuwa waangalifu na Watoto muda wote waangalie mara kwa mara mienendo yao na kuwa na muda wa kuzungumza nao ili kujua matatizo yanayowasumbua.

Hata hivyo kumeibuka mzozo wa kugombea maiti kati ya baba mlezi na baba mzazi yupi anastahili kuuzika mwili huo, hali iliyopelekea Uongozi wa Kijiji kuingilia kati na kushauri waende Mahakamani na kusikiliza amri itakayotolewa na Mahakama.

Friday, February 22, 2019

Chid Benz aionyesha nyumba yake, afungua mradi huu, amuomba Rais Magufuli mambo haya (+ Video)

Msanii na mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva Chid Benz ameamua kuionyesha nyumba yake mpya na kuonyesha kwa mara ya kwanza mradi wake ambao ni wa kuchoma mkaa, lakini pia amuomba Mh. Rais Magufuli mambo kadhaa:- Sehemu ya kwanza akionyesha nyumba yake h Sehemu ya Pili akionyesha miradi yake By Ally Juma.

The post Chid Benz aionyesha nyumba yake, afungua mradi huu, amuomba Rais Magufuli mambo haya (+ Video) appeared first on Bongo5.com.


Source

PASTA MGENI ASEPA NA KAPU LA SADAKA WAUMINI WAKIWA WAMEFUMBA MACHO KUOMBA

Tukio la ajabu limetokea katika kijiji cha Misuu, Kaunti ya Machakos nchini Kenya baada ya pasta mgeni kutoroka na kapu lililokuwa limejaa sadaka wakati waumini walipokuwa wamefunga macho kuomba.

 Kwa mujibu wa mdokezi aliyesema na Taifa Leo, pasta wa kanisa hilo alimualika mwenzake kutoka kaunti jirani ili awalishe waumini chakula cha kiroho na hatimaye kuongoza harambee ya kupanua kanisa hilo.

 Kila mmoja alianza kuomba kwa ndimi na kupandwa na jazba kubwa! Ni wakati huo pasta mgeni alipotoroka na kikapu cha pesa: 

 "Mtumishi wa Mungu alikuwa na matumaini makubwa kuwa mwenzake angechangisha pesa nyingi katika harambee hiyo kwa sababu alikuwa na ufasaha wa kuongea. Hii ndio sababu kuu ya kumualika kanisani," alisema mdokezi.

 Katika ripoti hiyo ya Jumanne, Februari 19 ambayo TUKO.co.ke imeisoma, wakati wa ibada ulipowadia, kanisa lilikuwa limejaa hadi pomoni.

 Kwaya iliburudisha kwa nyimbo mbili kisha pasta akanyanyuka na kumkaribisha mgeni.

Inaelezwa kuwa bado pasta wa kanisa hilo anamsaka mgeni wake ili amchukulie hatua za kisheria na kulazimishwa kurejesha pesa hizo.

 "Wajua mahubiri ya pasta huyo mgeni yalikuwa moto moto na yaliwagusa wengi rohoni," anasema mdokezi huyo.

 Inadaiwa kwamba, sadaka zilitolewa kwa wingi na kikapu kikawekwa madhabahuni alipokuwa ameketi pasta huyo mgeni.

 Baada ya kipindi cha mahubiri, inadaiwa kwamba pasta wa kanisa hilo aliinuka na akawaongoza waumini kwa maombi kabla ya kuanza mchango.

 Kila mmoja alianza kuomba kwa ndimi na kupandwa na jazba kubwa! Ni wakati huo pasta mgeni alipochukua kikapu kilichojaa sadaka na akaondoka polepole na kutoroka kupitia kichaka kilichoko karibu na kanisa. 

Duru za mtaani zanasema kuwa, waumini walipomaliza maombi na kufungua macho yao, walipigwa na butwaa walipopata mgeni wao hayupo na mfuko wa sadaka ulikuwa hauonekani.

 Kwa mujibu wa gazeti hilo, juhudi za waumini kumsaka pasta huyo ziliambulia patupu maana alikuwa ametokomea na kila alipopigiwa simu jibu lilikuwa, "Mteja wa nambari uliyopiga hapatikani kwa sasa."

 Waumini na pasta wao waliishia kuduwaa huku wakimlaani kwa kuiba sadaka bila kuhofia adhabu kali ya Mungu. 

Thursday, February 21, 2019

MBUNGE AZZA HILAL ACHANGIA MABATI KUSAIDIA UJENZI WA VYOO VYA SHULE ZA MSINGI "TINDE A" NA "TINDE B"


Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) amechangia mabati 23 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyoo katika shule za msingi Tinde A na Tinde B zilizopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ambazo zinakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vyoo.

Mheshimiwa Azza amekabidhi mabati hayo leo Februari 21,2019 kwa uongozi wa serikali ya kijiji cha Jomu na kamati za ujenzi za shule hiyo ikiwa ni mchango wake baada ya kuona wananchi wamejitokeza kuanzisha ujenzi wa vyoo hivyo.

Mbunge huyo alisema mabati hayo yenye geji 28,futi 10 yatatumika katika upauaji wa vyoo vya shule hizo hizo zenye jumla ya wanafunzi 2064 ambapo sasa wana matundu manne pekee ambayo nayo yamejaa.

"Mimi ni zao la Tinde, nimesomea hapa Tinde,Nimekuja kuwashika mkono kwa kuchangia mabati haya 23 ili wanafunzi wetu wasome katika mazingira bora,ni wajibu wetu sote kushirikiana ili kuboresha miundombinu ya shule",alisema Azza.

Naye Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko aliwashukuru wananchi kujitokeza kushiriki kujenga vyoo vya shule na madarasa huku akiwakumbusha pia kujenga vyoo katika familia zao.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza wakati akichangia mabati 23 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyoo katika shule za msingi Tinde A na Tinde B zilizopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akiwahamasisha wakazi wa Tinde kuendelea kuchangia katika shughuli za maendeleo.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza na wakazi wa Tinde.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiwasisitiza wakazi wa Tinde kujenga vyoo kwenye shule na kwenye familia zao.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akikabidhi mabati 23 kwa uongozi wa kijiji cha Jomu kwa ajili ya ujenzi wa vyoo katika shule za msingi Tinde A na B.
Zoezi la kukabidhi mabati likiendelea.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko akiangalia vyoo vilivyochimbwa kwa nguvu ya wananchi katika shule ya Msingi Tinde A ambapo mabati yaliyotolewa na mbunge Azza Hilal yatatumika katika upauaji.
Mwenyekiti wa kijiji cha Jomu akionesha vyoo vya shule ya msingi Tinde B ambapo pia mabati yaliyotolewa na Mbunge Azza Hilal yatatumika katika upauaji.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...