Saturday, February 23, 2019
Watoto wawili wa Darasa moja wafariki kwa kujinyonga
Wanafunzi wawili wa Darasa la tano Shule ya Msingi Mikiroy Magugu Mkoani Manyara waliokuwa wanakaa Dawati moja wamefariki dunia katika matukio yanayofanana, wa kwanza alifariki Mwezi Januari mwaka huu kwa kujinyonga, mwingine amejinyonga februari 20.
Mwanafunzi huyo (11) wa darasa la tano Shule ya Msingi Mikiroy kijiji cha Magugu kata ya Magugu Wilaya ya Babati Mkoani Manyara amejinyonga kwa taulo hadi kufa.
Akizungumza na MUUNGWANA BLOG Mtendaji wa Kijiji cha Magugu Leonsi Daniel Lumbu ameeleza kuwa tukio hilo limetokea Februari 20 mwaka huu baada ya mwanafunzi huyo kutoka Shuleni majira ya Jioni ambapo hakuwakuta wazazi wake ndipo alipoenda kwa jirani kuchukua ufunguo na kuingia ndani na kujinyonga kwa taulo hadi kufa.
Amesema ni mtoto ambaye anaishi na Mama yake ambaye ameolewa na mwanaume mwingine huku baba yake mzazi akimuacha tangu alipokuwa na miaka miwili baada ya kufarakana.
Mtendaji huyo amemtaja Mwanafunzi huyo kuwa ni Mathayo Ezekiel huku akieleza kwamba Sio tukio la kwanza kutokea kwani January mwaka huu 2019 mwenzake waliokuwa wanasoma darasa moja na kukaa katika Dawati moja naye alikufa kwa kujinyonga hali iliyowaacha wengi midomo wazi wakijiuliza kulikoni?
Amewataka Wazazi kuwa waangalifu na Watoto muda wote waangalie mara kwa mara mienendo yao na kuwa na muda wa kuzungumza nao ili kujua matatizo yanayowasumbua.
Hata hivyo kumeibuka mzozo wa kugombea maiti kati ya baba mlezi na baba mzazi yupi anastahili kuuzika mwili huo, hali iliyopelekea Uongozi wa Kijiji kuingilia kati na kushauri waende Mahakamani na kusikiliza amri itakayotolewa na Mahakama.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Bongo Deco wauzai wa vifaa mbalimbali vya umeme kama TV, Subwoofer, Hometheator, Majiko madogo na makubwa ya Gesi, Friji, Generator nk leo w...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya ...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Kuongezeka kwa ghasia za hivi majuzi kumesababisha idadi kubwa ya raia wa Lebanon kukimbia kutoka Beirut huku milipuko ikitikisa jiji hilo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 15, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekagua ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo – Busisi) ...