Saturday, February 23, 2019
Hizi ndiyo njaa mbili zinazowasumbua wanandoa katika Maisha yao ya ndoa
Habari rafiki na mpenzi msomaji wa Amka Mtanzania? Na karibu tena katika makala yetu ya leo ili tuweze kujifunza. Katika makala yetu ya leo tutajifunza njaa zinazowasumbua wanandoa katika maisha yao ya ndoa. Kuzifahamu njaa zinazowasumbua wanandoa tafadhali twende sanjari mpaka mwisho wa makala hii.
Kumekuwa na mitazamo hasi sana juu ya maisha ya ndoa. Kabla mtu hajaingia ndani ya maisha ya ndoa tayari akili yake imeshajazwa mitazamo hasi juu ya maisha ya ndoa. Mtu aliyepatwa na matatizo katika maisha yake ya ndoa naye atakwenda kuwaaminisha watu juu ya matatizo yake juu ya ndoa. Siyo kwamba katika maisha ya ndoa hakuna changamoto la hasha zipo kama kawaida kama vile kwenye kazi, biashara, ujasiriamali nakadhalika. Hivyo kwenye jambo lolote changamoto haziepukiki. Kweli itakuweka huru na usipoujua ukweli utapata shida sana.
Maisha ya ndoa unayotaka kuishi unayatengeneza wewe mwenyewe na si vinginevyo hivyo usipoteze muda wa kuhangaika tengeneza yale maisha ambayo unayataka kuishi na usisikilize kelele za watu ambazo zitakuwekea ukungu katika macho yako na kushindwa kuona mbele. Na waswahili wanasema ukiona vyaelea ujue vimeundwa kwa hiyo, hata wewe unaweza kuviunda katika maisha yako ya ndoa.
Katika hali ya kawaida hakuna mtu asiyeijua njaa, mtu akiwa na njaa anapoteza kabisa nguvu na hata ufanisi wa kazi aliyokuwa anafanya unapotea, kwa hiyo njaa huwa inalegeza watu kama akikosa kula chakula na kushiba. Vivyo hivyo, kila mwanandoa ana njaa yake yaani mwanaume ana njaa yake katika maisha ya ndoa hali kadhalika kwa mwanamke naye ana njaa yake. Kwa maana hiyo, kila mwanandoa anahitaji ashibishwe njaa yake na mwenza wake.
Ikitokea sasa wanandoa hao yaani wawili hao kutoshibishana njaa zao ndio matatizo huanzia hapo. Na tunajua ya kwamba wawili hao kila mmoja ana njaa yake. Hivi ikitokea mtu ana njaa ya chakula halafu pale anapotegemea kupata chakula ili ashibishe njaa yake hapati ataendelea kusubiri kubaki na njaa yake? Jibu ni kwamba lazima atatafuta sehemu ambayo ataweza kupata chakula ili aweze kushibisha njaa yake.
Ndugu msomaji, kama kila mwanandoa ameshindwa kumshibisha mwenzake basi ujue lazima atatafuta chakula sehemu nyingine ili kuweza kukidhi njaa yake. Hivyo basi, kumbe ni wajibu wa kila mwanandoa kuhakikisha anamshibisha mwenzake njaa yake.
Zifuatazo ni njaa mbili zinazowasumbua wanandoa endapo hawatashibishana;
1. Njaa ya mwanamke ni upendo;
Mwanamke anahitaji upendo kuliko vitu vingine, hata katika vitabu vya dini vinasema; enyi waume, wapendeni wake zenu. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe, mwanaume anatakiwa kujitoa kwelikweli kumpenda mke wake kama tunavyojua upendo ndio falsafa kubwa sana katika maisha ya binadamu, upendo huvumilia, hufadhili, hauhusudu. Hivyo basi njaa ya mwanamke ni kupendwa. Wewe kama mwanaume unatakiwa kumpenda mke wako kwa moyo wako wote bila kujali udhaifu wake. Hii ndio njaa ya wanawake wanahitaji upendo katika maisha ya ndoa.
2. Njaa ya mwanaume ni kuheshimiwa;
Mwanaume njaa yake kubwa ni kuheshimiwa katika maisha ya ndoa. Sasa ikitokea mwanaume anakosa kuheshimiwa na mke wake katika maisha ya ndoa hivyo anakuwa amekosa kushibishwa njaa yake. Na kama akikosa kushiba ndio matatizo huanzia hapo itamlazimu kutafuta kushibishwa njaa yake nje. Hivyo kama wewe ni mwanamke unatakiwa kumshibisha mume wako njaa yake ya kumtii.
Kama wanandoa wanashindwa kushibishana njaa zao, hivyo wanajitengenezea shimo wao wenyewe. Watu wanajisahau sana katika kutimiza majukumu yao katika maisha ya ndoa hatimaye wanaruhusu haki za kibinadamu kuingia maisha ya ndoa, kama wanandoa mkishaingiza haki za kibinadamu katika maisha ya ndoa yaani hamsini kwa hamsini kama wanavyodai lazima mtapoteza mwelekeo tu. Kwa hiyo kila mtu ana njaa yake kama tulivyoona hapo juu sasa mkishayaingiza mambo haya ya kidunia mtakosa kushibishana njaa zenu.
Source
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Bongo Deco wauzai wa vifaa mbalimbali vya umeme kama TV, Subwoofer, Hometheator, Majiko madogo na makubwa ya Gesi, Friji, Generator nk leo w...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya ...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Kuongezeka kwa ghasia za hivi majuzi kumesababisha idadi kubwa ya raia wa Lebanon kukimbia kutoka Beirut huku milipuko ikitikisa jiji hilo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 15, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekagua ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo – Busisi) ...