Thursday, August 20, 2020

Ujumbe wa Mwana FA baada ya kuteuliwa kugombea ubunge jimbo la Muheza Tanga



Baada ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na kamati yake kupitisha majina ya wagombe wa Ubunge, Udiwa na viti maalumu kupitia chama cha mapinduzi CCM hivi leo.

Baadhi ya wadau wa muziki wameteuliwa ambao ni msanii wa muziki wa Bongo Fleva Mwana FA na meneja wa Diamond Platnumz Bbutale.


Baada ya uteuzi huo Mwana FA  ameandika ujumbe huu 

"Mungu ni mwema sana, Leo ni miongoni mwa zile siku chache, mimi nimeishiwa na sina la kusema, alama nyingine kuhusu ukubwa wa Mungu"



Mtoto Mwingine Atupwa Chooni Kagera



MTOTO mwingine wa kike mwenye umri wa siku tatu, ameopolewa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwenye choo cha Zahanati ya Mshikamano wilayani Ngara mkoani Kagera akiwa hai.

Hilo ni tukio la pili kutokea wilayani humo, kwani Mei 21 mwaka huu, mtoto Isabela aliopolewa akiwa hai kwenye choo cha Shule ya Msingi Murganza wilayani humo na jeshi hilo.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Kagera, Hamis Dawa, amesema walipata taarifa ya kutupwa kwa kichanga hicho katika choo cha Zahanati ya Mshikamano kupitia kwa Jeshi la Polisi wilayani humo.

"Baada ya taarifa hiyo, tuliwatuma askari wawili ambao ni ZM 3338 Sajenti Bahati Rudisha na FC 3802 Amos Mwita, ambao walifanikiwa kumuokoa mtoto huyo akiwa hai.

"Mtoto huyo tumemkabidhi kwenye Hospitali ya Mshikamano kwa ajili ya matibabu wakati huo Jeshi la Polisi likiendelea kumtafuta mama wa mtoto huyo aliyemtupa kwenye shimo la choo," alisema kamanda Hamisi Dawa.

Kwa mujibu wa Kamanda Dawa, kichanga hicho ambacho kilikuwa bado hakijakatika kitovu, kiliopolewa katika choo hicho kilichokuwa kinatumika, hivyo baada ya askari hao kubomoa mfuniko wa choo, walikiona kikiwa kinaelea.

"Mtoto hakukutwa na majeraha, bali alikuwa na afya njema, hivyo wahudumu wa afya hospitalini, wanaendelea kumfanyia uchunguzi wa kitabibu

"Tunashirikiana na watu wa Ustawi wa Jamii na wahudumu wa afya kitengo cha afya ya uzazi, ili kuweza kutoa elimu kwa akina mama ambao ndiyo wanaobeba ujauzito, jinsi ya kulea na kukabiliana na changamoto za kifamilia zinazowasababishia kutenda ukatili kwa watoto kama huu," alisema Kamanda Dawa.


Source

Picha : ASKOFU SANGU AONGOZA IBADA YA MASIFU YA JIONI

Askofu wa Jimbo Katoliki la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu,leo Jumatano Agosti 19,2020 ameongoza Ibada ya masifu ya jioni ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kutoa daraja Takatifu la Upadre kwa Mashemasi sita ambapo watatu ni wa jimbo la Shinyanga ,wawili ni wa shirika la Mtakatifu Agustino na Mmoja ni wa shirika la SMA.

Ibada hiyo imefanyika katika Kanisa Kuu la Mama Mwenye Huruma Ngokolo mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na Mapadre,Watawa,na Waamini kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya jimbo Katoliki.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Askofu wa Jimbo Katoliki la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu ameongoza Ibada ya masifu ya jioni .PICHA KWA HISANI YA RADIO FARAJA FM STEREO

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...