Tuesday, September 11, 2018

WATU WANNE WAFARIKI DUNIA PAPO HAPO KATIKA AJALI YA GARI LA KUBEBA MBAO ROMBO

Na Dixon Busagaga,Rombo.

WATU wanne wakiwemo wawili wa familia moja wamefariki dunia papo hapo baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Isuzu kuacha njia na kwenda kugonga ngema katika eneo la Kikelelwa wilayani Hai.

Waliofariki dunia wametambulika kwa majina ya Emanual Josephat Silayo (28) ,Viviano silayo (35) wakazi wa Mbomai Juu,Juma Idd (20) maarufu kama mwarabu na mwingine aliyefahamika kwa jina moja la Deolla .

Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Hamis Issah aliyefika eneo la tukio amethibitisha kutokea kwa ajalo hiyo na kwamba dereva wa Lolri hilo lililokuwa limebeba mbao alikimbia kusiko julikana baada ya ajali..

"Jitihada za kumtafuta dereva zinafanyika na chanzo cha ajali ni kupoteza muelekeo kwa Lori hilo na baadae kugonga Gema ndipo watu waliokuwa wanekaa mbele walichomoka na kwenda kupigiza vichwa katika Gema na kupasuka"alisema Kamanda Issah.

Kamanda Issah amesema gari hilo likiwa na shehena ya mbao lilikuwa likitokea eneo la West Kilimanjaro ,eneo maarufu kwa uchanaji wa mbao na kwamba lilikiwa likielekea Rombo kupitia njia ya Rongai.

"Ni gari la kubeba mbao lilikua linatoka West Kilimanjaro kupitia njia ya Kikelelwa wilayani Rombo ,Gari aina ya Isuzu likiwa na namba za usajili T 889 ACN lilimshinda dereva na kuacha njia na baadae kugonga ngema iliyosababisha watu wanne waliokuwemo katika gari hilo kufa papo hapo." alisema Kamanda Issah.

Miili ya marehemu wote imehifadhiwa katika hosptali ya wilaya ya Rombo kwa ajili ya maandalizi ya mazishi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah akiangalia gari hilo wakati alipofika kwenye eneo la tukio.

Source

TAARIFA MUHIMU KWA WASOMAJI NA WATUMIAJI WA MUUNGWANA BLOG USIPITWE NA HII

Mtandao wako pendwa wa Muungwana Blog unaomba radhi kwa watumiaji ambao wamepakua APP yetu na hawapati habari kwa muda au hawapati kabisa kutokana na hitilafu za kiufundi zilizojitokeza tunakuomba upakue tena upya App hii ili uweze kupata taarifa za papo kwa papo.

Unachotakiwa kufanya ni kufuata hatua zifuatazo:

1. Ingia kwenye Google Play store

2. Tafuta Muungwana Blog

3. Pakua App (Instal Application ya Muungwana blog CLICK   DOWNLOAD 

Monday, September 10, 2018

Msanii Aila afunguka kuhusu muziki wake na mengine mengi (Video)

Msanii wa muziki Aila ambaye anafanya vizuri na wimbo Kila Sekunde amefunguka kuuzungumzia muziki wake pamoja na namna anavyoonekana kwamba anafanya muziki akiwa ameridhika.

The post Msanii Aila afunguka kuhusu muziki wake na mengine mengi (Video) appeared first on Bongo5.com.


Source

Wema Sepetu Adaiwa Kumwaga Mpenzi Wake

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu ametudi Kwenye headlines ambapo anadaiwa amemwaga aliyekuwa mpenzi wake anayeitwa kwa jina la Lawrence Masanja maarufu Kwenye mitandao ya kijamii kama R.A.H.U.R. Global Publishers wanaripoti kuwa kuvunjika kwa penzi hilo kulitokana na baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa Wema kumng'ata sikio kuwa jamaa aliyenaye hafai na akiendelea naye atakuja kujuta. Chanzo cha karibu cha Wema kimetiririkia gazeti la Ijumaa Wikienda: Wema kaamua kumwaga manyanga kwa yule jamaa yake, mwenyewe alishaanza kushitukia kuwa kaingia 'cha kike' na hata watu wake walipomtonya kuwa jamaa siyo hakuona ugumu kumtosa. Sasa hivi nasikia ana jamaa mwingine". Baada ya Tetesi hizo Gazeti hilo lilimsaka Wema ili kupata ukweli kutoka kwake na alikiri kuwa yeye na mwanaume huyo hawapo wote: Jamani huyo mtu siko naye na sidhani kama itakuwa ni vyema nikimuongelea kwa sababu sihitaji kufanya hivyo ila kwa kifupi hayupo katika maisha yangu". Mahusiano ya Wema yalisemekana kuingia doa wiki chache zilizopita baada video zilizomuonyesha Wema na Diamond wakiwa na ukaribu wa ajabu kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii.

The post Wema Sepetu Adaiwa Kumwaga Mpenzi Wake appeared first on Ghafla!Tanzania.


Source

WANANCHI WAJITOLEA KUCHONGA BARABARA ILI WAVUTIWE UMEME SHINYANGA


Wananchi wa mtaa wa Imalilo Kata ya Kitangili manispaa ya Shinyanga wamechangishana fedha kwa ajili ya kuchonga barabara za kupita kwenye mtaa wao ili wapate kuvutiwa umeme kama walivyopewa masharti na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoani Shinyanga.

Wananchi hao wakizungumza na Malunde1 Blog leoe wakati walipokuwa wakichonga barabara za mtaa huo kupitia wanachuo cha ufundi Stadi Veta mkoani humo, walisema baada ya kuona miaka ina kwenda bila ya barabara zao kuchongwa na manispaa, ndipo wakaamua kuchangisha fedha na kuzichonga wenyewe ili wapate kuvutiwa umeme. 

Walisema huu ni mwaka wa tatu sasa tangu walipoomba kuwekewa umeme katika mtaa wao, na kutokana na kushidwa kutekeleza masharti waliyopewa na TANESCO, kuwa mpaka barabara zao za mitaa zitakapochongwa na kuonyesha ramani za mipaka ndipo watavutiwa umeme huo na ndiyo maana wameamua kuchonga barabara. 

Mmoja wa wananchi hao ambaye alichanguliwa kuwa Mwenyekiti wa kusimamia zoezi la uchongwaji wa barabara hizo, Florence Kihundo, alisema baada ya kuwa na shida ya umeme ndipo wakaitana  kwenye kikao na kuchangisha fedha kila kaya Shilingi 25,000/-, ambapo kuna jumla ya kaya 115 lakini zilitoa  kaya 20 tu na kupatikana shilingi 500,000/=. 

"Baada ya kuona muitikio wa zoezi hili umekuwa mdogo, ndipo tukaandika barua kwenye chuo cha Ufundi Stadi Veta ili watupatie msaada wa mtambo (Greda), ambapo sisi tutachangia mafuta, ndipo wakakubali ombi letu ikiwa nao ni sehemu ya wanafunzi wao kujifunza kwa vitendo kuchonga barabara mpya. 

Naye mwenyekiti wa mtaa huo Magdalena Mushashi, alipongeza wananchi wake kujitolea kuchangisha fedha za uchongaji wa barabara hizo kilomita moja, na kubainisha kuwa bajeti ya manispaa ya Shinyanga (2017-18) iliisha ambapo walipewa kilomita 39, na hivyo kuwaomba TANESCO watekeleze majukumu yao. 

Kwa upande wake kaimu meneja wa Shirika hilo la Umeme TANESCO mkoani Shinyanga Athony Tarimo aliwatoa wasiwasi wananchi hao na kubainisha kuwa mwaka huu hautaisha lazima watakuwa tayari wameshavutiwa umeme huo, ikiwa bajeti yao ipo na wameshawekwa kwenye mpango. 

Aidha Mwalimu wa Mitambo kutoka chuo hicho cha Veta Yona Elisha, ambaye aliambatana na wanafunzi kwenye uchongaji wa barabara mpya za mtaa huo, alisema wamefurahia kazi hiyo ikiwa ni sehemu ya kutoa elimu kwa vitendo, ambapo wanachuo hao wataelewa vizuri masomo yao. 

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI
Baadhi ya wananchi wa mtaa wa Imalilo kata ya Kitangili manispaa ya Shinyanga wakiangalia uchongwaji wa barabara kwenye mtaa wao ambapo wametumia nguvu zao wenyewe kwa kuchangishana fedha ili wapate kuvutiwa umeme kwenye mtaa huo.Picha zote na  Marco Maduhu Malunde1 Blog.
Wanachuo cha Veta mkoani Shinyanga wakichonga barabara hiyo mpya ya mtaa wa Imalilo kata ya Kitangili manispaa ya Shinyanga, kama sehemu ya mafunzo kwao kwa vitendo ambapo wananchi wa mtaa huo wamegharamia fedha za mafuta.
Wanachuo Veta wakichonga barabara za mtaa wa Imalilo Kata ya Kitangili manispaa ya Shinyanga ili wapate kuvutiwa umeme.
Florence Kihundo ni Mwenyekiti aliyechaguliwa na wakazi wa mtaa huo wa Imalilo kusimamia uchongwaji wa barabara kwenye mtaa huo, ili wapate kuvutiwa umeme , kulingana na masharti waliodai kuwekewa na Tanesco ya kuchonga barabara za mtaa huo.
Uchongaji wa barabara ukiendelea.
Uchongaji wa barabara za mtaa wa Imalilo ukiendelea ambazo ni Kilomita moja.
Mwananchi Hadija Ndabi wa mtaa huo wa Imalilo akielezea furaha yao ya kukamilisha zoezi la uchongaji wa barabara za mtaa huo, ili waweze kuvutiwa umeme na Tanesco na kuwatoa kuishi kwenye giza.
Mwananchi Witness Isack akielezea namna walivyohamasika kuchangisha fedha ili kuchonga barabara za mtaa wao huo wa Imalilo kata ya Kitangili ambazo zitawafanya kupata umeme pamoja na kufungua shughuli zingine za kibiashara zitokanazo na matumizi ya umeme na hatimaye kuwaingizia kipato ikiwa mtaa huo ni mpya.
Sehemu ya barabara ya mtaa wa Imalilo Kata ya Kitangili manispaa ya Shinyanga ikiwa imechongwa na wanachuo kutoka Veta mkoani Shinyanga. 

Picha zote na  Marco Maduhu Malunde1 Blog.

SERIKALI KUAJIRI WATENDAJI KATA 1000

Serikali ina mpango wa kuajiri watendaji kata 1,000 ili kupunguza pengo kubwa la ukosefu wa watendaji hao katika maeneo mengi nchini.

Kauli hiyo imetolewa leo bungeni na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Joseph Kandege.


Kandege alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Tundulu Kusini (CCM), Daim Mpakate ambaye alitaka kujua ni lini Serikali itaajiri watendaji kata kwani maeneo mengi yako wazi.


Naibu Waziri huyo alikiri watendaji ni watu muhimu katika shughuli za maendeleo hivyo Serikali imeona umuhimu wa kuwaajiri ili kusukuma mbele kurudumu la maendeleo.


"Tumeomba kibali na tumepewa kuajiri watendaji kata 1,000, hivyo tuna amini tukishaajiri hao tutakuwa tumepunguza pengo hilo kwa kiasi kikubwa," alisema Kandege.

Naibu Waziri huyo alisema mpango huo utafanyika mapema kwa kuwa uhitaji wao ni mkubwa.

Fahamu jiwe la ekari 7 lenye ramani ya bara la Afrika linalotumika katika ibada za kimila Tanzania

Huwenda umepata kusikia maajabu mengi duniani hebu fahamu na hili, huko Mkoani Njombe Kusini Magharibi mwa nchi ya Tanzania kuna jiwe kubwa kwa jina la Lwiwala lenye ramani ya bara la Afrika. Jiwe hilo la ukubwa ekari 7.8 limejizoelea umaarufu mkubwa kutokana na kuwepo kwa ramani ya bara la Afrika ambayo haijachorwa na mtu. Katika …

The post Fahamu jiwe la ekari 7 lenye ramani ya bara la Afrika linalotumika katika ibada za kimila Tanzania appeared first on Bongo5.com.


Source

Breaking: Mahakama Yatupilia Mbali Mapingamizi ya Serikali Kuhusu Ving’amuzi Chaneli za Ndani

Mahakama yatupa mapingamizi ya Serikali ving'amuzi chaneli za ndani

Mapingamizi ya Wakili wa Serikali yaliyokuwa yanapinga Mahakama  kuondolewa amri ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) inayozitaka baadhi ya  kampuni zilizokuwa zikionyesha chaneli za ndani kuondolewa kwenye ving'amuzi vyao ymetupilia mbali na Mahakama Kuu Kanda ya Iringa.


AICT church speaks on killing of choir member

The African Inland Church of Tanzania (AICT) hopes that justice will be served in the death of its choir member, Ms Miriam Charles, 26, stressing they will leave the matter to police.
Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...