Alikataa kuandika urithi kwa kuamini kuwa marastafari huwa hawafi.
Robert Nesta Marley,ambaye baadaye alikuja kujulikana kama Bob Marley,alizaliwa Februari 6,1945 katika kijiji cha Nine Mile kwenye Parishi ys mtakatifu Ann huko Jamaica.
Baba yake Norval Sinclair Marley alikuwa mzungu na mama yake Cedelia Booker alikuwa Mjamaica mweusi.
Historia ya maisha yake haitofautiani sana na wanamuziki wenzake wa reggae Peter Tosh aliyelelewa na shangazi yake na Bunny Wailer aliyelelewa na baba yake zaidi,ni historia ya huzuni iliyo muacha Bob Marley chini ya mzazi mmoja(mama yake) pale alipofiwa na baba yake akiwa na umri wa miaka kumi tu.
Norval Sinclair (baba yake Bob Marley) alikuwa nahodha wa meli na muangalizi wa mashamba,alikufa mwak 1955 akiwa safarini,wakati huo alikuwa na umri wa miaka 60.
Kifo hicho kilimfanya mama yake Bob Markey ahamishe makazi kwenye mji wa Kingston,huko Bob alikutana na Bunny Wailer wakawa marafiki na kujifunza muziki pamoja.Akiwa na umri wa miaka 14,
Bob Marley aliacha shule na kujiunga na chuo cha ufundi wa kuchomelea vyuma,muda wakewa kupumzika alikuwa na Bunny Wailer kwenye muziki,kipindi hiko mwalimu wao alikuwa Joe Higgs,
Muimbaji wa mtaani mwenye imani ya kirastafari.Chini ya Joe Higgs walikutana na Peter Tosh na kuungana naye.
Mwaka 1962 Bob Marley alirekodi nyimbo zake mbili za kwanza ambazo ni;"Usihukumu"(judge not) na "kikombe kimoja cha chai"(one cup of tea) chini ya muandaaji Leslie Kong,
lakini nyimbo hizo hazikukubalika sana.Mwaka 1963 akashirikiana na Bunny Wailer,Peter Macintosh(Peter Tosh),Junior Braithwaite,Beverly Kelso na cherry Smith n kuunda kundi la "The Teenagers" kundi hilo lilijibadili majina na kuwa "The wailing rude boys","The wailling wailers" na mwishowe "The wailers".
Mwaka 1964 na 1965 watoa vibao vikali kama "Usiwe na wasiwasi"(simmer down) na "Nafsi isiyokubali"(soul rebel)nyimbo hizi zilikonga nyoyo za Wajamaika wengi
Hata hivyo kufikia mwaka 1965 lilibakiwa na wakali watatu tu,yaani Bob Marley,Bunny Wailer n Peter Tosh,baada ya wengine kujiengua.
Mwaka 1966 Bob Marley alimuoa kimwana Rita Anderson na kwenda kuishi kwa muda na mama yake huko Wilmington,Delaware nchini Marekani..
Na kuibuka na imani kali ya kirastafari na kuja na mtindo wa kufuga nywele uitwao "dreadlocks".
Baada ya hapo Bob Marley na kundi lake la The wailers walitoa vibao kemkem vilivyoitikisa Dunia.
Kati ya vibao hivyo ni;Africa unit,Zimbabwe,Could oyu loved?,Iron lion zion,Is this love,Buffalo soldier na vingine vingi.
Huyo ni Bob Marley,mfalme wa reggae aliyepinga ubaguzi kwani hata yeye mwenyewe alisema "Wananiita chotara,lakini mimi siegamii upande wowote bali nipo upande wa Mungu aliye niumba kutoka kwa weusi na weupe".
Hiyo ni biograph ya mwanaharakati huyo wakupinga ubaguzi."REST IN PEACE RASTAFARAE"
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali shauri lililokuwa limefunguliwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina...
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...