
Na mwandishi wetu
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake (BAWACHA) Mkoa wa Kagera Mhe. Magreth Kyai, ataongozana na Wanawake wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutoka Majimbo tisa ya Mkoa wa Kagera kwenda Jijini Dar es salaam kushiriki maadhimisho ya Sherehe ya Siku ya Wanawake Duniani itakayofanyika Machi 8, 2025.
Akiongea na Malunde 1 Blog Bi Magreth Kyai amesema kuwa huwa wanafanya sherehe hizo kila Mwaka kwa Mikoa na Kanda tofauti.
Amesema kuwa kwa Mkoa wa Kagera wanatarajia kusafiri Wanawake 42 ili kukiwakilisha Chama hicho.
Aidha Bi Magreth ameongeza kuwa sherehe hizo zitafanyikia Kanda ya Pwani, Mkoa wa Dar es Salaam, Mlimani city huku Kauli mbiu ikiwa ni HARAKISHA USAWA WA KIJINSIA KWA MAENDELEO ENDELEVU.