Wednesday, October 9, 2024

Wabunge wa Kenya wapiga kura kumtimua Naibu Rais Rigathi Gachagua

Hatimaye bunge la Kenya lilipiga kura siku ya Jumanne kumtimua Naibu Rais Rigathi Gachagua kwa madai ya kujitajirisha na kuibua chuki za kikabila.

“Kulingana na matokeo … ya hoja ambayo nimetangaza hivi punde, jumla ya wajumbe 281 wakiwa zaidi ya theluthi mbili ya wabunge wamepiga kura kuunga mkono hoja hiyo,” Moses Wetang’ula alisema.

Gachagua, ambaye amekanusha mashtaka yote, alimuunga mkono Rais William Ruto katika ushindi wake wa 2022 na kusaidia kupatikana kwa kura nyingi kutoka eneo lenye wakazi wengi la kati mwa Kenya.

Lakini katika miezi ya hivi karibuni amezungumza kuhusu kutengwa, huku kukiwa na ripoti zilizoenea kwenye vyombo vya habari kuwa ametofautiana na Ruto huku miungano ya kisiasa ikibadilika.

Ruto alitupilia mbali sehemu kubwa ya baraza lake la mawaziri na kuwaleta wanachama wa upinzani kufuatia maandamano ya kitaifa dhidi ya ongezeko la ushuru ambalo halikupendwa mwezi Juni na Julai ambapo zaidi ya watu 50 waliuawa.

Hoja hiyo sasa itapelekwa kwa Bunge la Seneti na ikiidhinishwa huko, Gachagua atakuwa naibu wa kwanza wa rais kuondolewa mamlakani kwa njia hii tangu kuondolewa madarakani kuanzishwa katika katiba iliyorekebishwa ya 2010 ya Kenya.

 

The post Wabunge wa Kenya wapiga kura kumtimua Naibu Rais Rigathi Gachagua first appeared on Millard Ayo. 

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...