Wednesday, October 9, 2024

Marufuku kucheza kwenye magari na kuvimwagia maji vijora

Katibu wa Baraza la Sanaa Zanzibar Bassfu Juma Chum amepiga marufuku tabia zilizoonekana kushamiri Zanzibar za wanawake kucheza na vijora wengine kuvimwagia na maji kwenye magari huku kukiwa kunapigwa mziki tabia ambazo zimekua zikijitokeza pindi watu wakiwa wanakwenda kwenye mipira na shughulini

 

Chum amesema kumekua na tabia za watu kukodi magari na kuingiza makundi ya mziki ikiwemo mabeni ,vidumbaki na Madj wakipiga mziki na spika kubwa na kukiwa na makundi ya wanawake wanaokatiw sare maalum za Vijora na kisha kusasambua na kucheza pindi wanapokwenda kutazama mipira na shughulini wakiwa wanacheza

 

kwenye operesheni hiyo endelevu magari ikiofanyika mkoa wa mjini imefanikiwa kuzuiya gari saba ambazo zimeshikiliwa katika kituo cha Madema Zanzibar ambapo Baraza la Sanaa limepania kudhibiti matendo hayo yalio kinyume na mila na Desturi za Zanzibar.

The post Marufuku kucheza kwenye magari na kuvimwagia maji vijora first appeared on Millard Ayo.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...