Wednesday, August 14, 2024

KMC Wagoma Kumwachia Awesu Kwenda Simba.......

KMC Wagoma Kumwachia Awesu Kwenda Simba.......

Mapema mwezi July Awesu Awesu alitangazwa kuwa mchezaji mpya wa Simba SC , siku chache baadae na mchezaji alitangaza kuwaaga KMC [ Swipe picha inayofuata ] wakati yote hayo yanatokea KMC wao walikuwa kimya mbele ya camera huku wakifanya mchakato wa kumrudisha kimya kimya kwa kwenda kufungua kesi kwenye mamlaka za mpira nchini.


Madai ya KMC ni kwamba Simba walitakiwa kupitia kwao ili kujadili thamani ya mchezaji ili wauziwe wakidai kuwa Simba wamepitia kwa mchezaji tu , taarifa za upande wa mchezaji zinaeleza kuwa mchezaji alivunja mkataba kwa kulipa kiasi cha pesa anachotakiwa kulipa kwa mujibu wa mkataba baada ya happ akawa huru ndipo Simba wakamsajili.


Kesi hii imefika kwenye mamlaka na tunasubiri taarifa ya hukumu , hii leo KMC wameamka na bango la kumkaribisha tena kiungo huyo nyumbani [ swipe hadi picha ya tatu ]


Tunaendelea kufuatilia ili tujue kama wameshinda kesi na mchezaji ameridhia kurudi KMC kwa sababu madai ya KMC ni Simba ikae mezani ilipe kiasi ambacho klabu inataka baada ya hapo watapewa mchezaji , Simba wao wameiacha kesi baina ya mchezaji na klabu back to the roots haina tofauti sana na kesi ya Feisal

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...