Wednesday, August 14, 2024

Naibu Waziri Nyongo azindua mfuko wa Alpha Halal Fund


NAIBU waziri wa nchi Ofis ya Rais Mipango na uwekezaji Stanslaus Nyongo ameitaka Kampuni ya Alpha Capital na wadau wengine kuongeza ubunifu zaidi ili kuleta bidhaa bora katika uwekezaji wa masoko ya mitaji.

Rai hiyo ameitoa leo Jijini hapa alipokuwa katika uzinduzi wa uwekezaji wa pamoja wa mfuko wa Halal Fund uliozinduliwa na Kampuni Alpha Capital.

Nyongo alisema kitendo cha kuzinduliwa kwa huduma hii ambayo itazingatia na imani za watu itakuwa nzuri kwa kuwa watu kama hao walikosa fulsa hiyo.

Aidha Nyongo aliwataka wawekezaji kuchagua kuwekeza katika mfuko huu wa Alpha Halal ambao unafika nchi zote za Afrika Mashariki na SADEC.

Aidha Nyongo aliwataka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana CMSA kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi ili waweze kutambua umuhimu wa kuwekeza kwenywe mifuko ya pamoja.

"Huu mfuko ni wa kiimani zaidi hivyo naamini utasimamiwa vilivyo na wahusika kuhakikisha unafanikiwa na kutimiza lengo,"alisema Nyongo.


Gerase Mugisha Kamugisha mtendaji Mkuu Alpha Capital alisema mfuko huo utazingatia maadili na ndio maana wametumia neno Shari'ah  kwa kuwa ni mfuko uliokaa kimaadili zaidi.

Alisema Alpha itawekeza katika bidhaa tatu, Hisa katika makampuni yaliyosajiliwa katika masoko ya hisa nchi husika, watawekeza katika Sukuk ambayo ni bidhaa ya kislam inayizingatia shariah na pia katika mifuko kama wa kwao ambayo inazingatia maadali kama wao wanavyokwenda.

Alisema wanakusudia kukusanya sh bil 10 mpaka kufikia Oktoba 17 mwaka huu kupitia wawekezaji wa ndani na wa nje.

Kwa upande wake Exaud Julius mwakilishi kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na dhamana CMSA alisema, wao wana mamlaka ya kuhakikisha kila jambo linalohusu masoko ya mitaji linafanyika kwa kufuata sheria.

Alisema CMSA ilitoa idhini kwa Alpha Capital kwa kukidhi matakwa ya sheria za masoko ya mitaji kwa ajili ya kuwahudumia wawekezaji mbalimbali wenye mitaji yao midogo, ya kati na mikubwa.
"Katika juhudi za kuwezesha kufikia malengo CMSA imeidhinisha kushusha kiwango cha ushiriki katika uwekezaji kwenye mfuko huu kutoka sh mil 1 hadi sh 100,000,"alisema Exaud.


 


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...