Tuesday, August 6, 2024

Bandari ya Tanga yashauriwa kushirikiana na TRC


Maonyesho ya nane kanda ya mashariki yamefanyika Mkoani Morogoro ambapo yameshirikisha Mikoa ya Pwani, Dar-eslaam,Tanga,na Morogoro na hapa bandari ya Tanga imepata fursa ya kushiriki maonyesho hayo na kutembelewa na mkuu mkoa wa pwani bw, Abubakary Kunenge ambapo ameishauri bandari hiyo kushirikiana na shirika la reli la Tanzania TRC katika usafirishaji wa bidhaa.

Habiba Omary ni afisa masoko kutoka bandari ya tanga anaeleza kuwa lengo hasa yakushiriki maonyesho haya ni kuwaelimisha watu huduma mbalimbali ambazo bandari wanatoa pia kuwahamasisha wakulima kutumia bandari kusafirisha mazao yao kwani wakitumia kusafirisha mazao kwa njia ya bandari kunalahisisha kufika kwa ulahisi bila kukwama kwama na kwa njia salama bila usumbufu wowote

"Mkulima anaweza kusafirisha mazao yake kwenda nje ya nchi kwa kutumia usafiri wa bandari kwani tunatumia konteina maalum ambazo zitahifadhi mazao na kufika mahala husika zikiwa salama na ubora ule ule."alisema Habiba

Aidha Habiba ameeleza kuwa bandari ya tanga ipo hapa kuwaelezea wananchi juu ya maboresho yaliyofanywa na serikali ya awamu ya sita ya rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania dkt Samia Suluhu Hassan juu ya bandari ya tanga kwa kuongeza kina kwani kimeongezeka kutoka mita 3 hadi kufikia mita 13 kuongezeka kwa kina hiki kutaruhusu meli nyingine kutoka ndani na nje ya nchi kutia nanga kwenye bandari ya Tanga na toka tumekabidhiwa maboresho haya mwaka juzi tumeweza kupokea meli 35 kubwa za mizigo zilizotuwa katika bandari ya Tanga.

Kwa upande wake mkuu mkoa wa pwani bw, Abubakary Kunenge ametumia nafsi hiyo kuwahamasisha bandari ya Tanga kuwa na ushirikiano na shirika la reli Tanzania TRC katika sekta ya usafirishaji na ushirikiano huu utazaa matunda mazuri.




 

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...