ADF: Lifahamu kundi la waasi kutoka Uganda linaloshirikiana na Islamic State
Kati ya makundi yenye sifa mbaya zaidi yanayoendesha shughuli zao DRC ni lile la kutoka nchini Uganda la Allied Democratic Forces (ADF). Kundi hilo la kiislamu liliundwa miaka ya 1990 na mara nyingi lilihusika na mizozo ya ndani na taifa la Uganda.