Kupitia maelezo yake aliyoweka kwenye mtandano wa Instagram Haji Manara ameandika kuwa "Nikisoma baadhi ya Comments zenu toka jana mnauliza Bughatti Mbona husemi kitu kuhusu billioni 20, ndugu zangu kama kuna Muumini namba moja aliyeshiriki kuwashawishi wanasimba wakubali juu ya muundo huu mpya ni mimi"
"Nilizodolewa sana, nikatusiwa sana na nikagombana na wengi kuhusu uwekezaji huu, iweje nisiunge mkono jambo lenye maslahi kwa Simba na mpira wetu kwa ujumla"
"Na niwaambie jana ni siku kubwa kwangu kwa sababu nililotaka na kulipigania limekuwa, nitaunga mkono kila jitihada za kuifanya Simba iwe kubwa zaidi na zaidi na Insha'Allah wiki hii nitaongea nanyi kuwashukuru"
Saturday, July 31, 2021
Kauli ya Manara baada ya Mo Dewji kutoa bilioni 20 Simba
Polisi Yakata 15 Wakamatwa Na Viuatilifu Feki Mtwara
POLISI Mkoani Mtwara imikamata watu 15 kwa tuhuma za kuuza viuatilifu feki vya salpha na vya maji ambavyo vinatumika kudhibiti magonjwa ya zao la korosho.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigadia Jenerali Marco Gaguti amewaambia waandishi wa habari mjini hapa kuwa watu hao walikamatwa na viuatilifu vya salpha tani 84.3 na vya maji tani 292 ambavyo vimeisha muda wake wamatumizi.
"Watu hao walikamatwa katika zoezi lilofanywa na jeshi la polisi mkaoni hapa baada ya kupata taarifa za awali za uwepo wa viuatilifu feki katika baadhi ya maduka maeneo mbalimbali Mtwara," amesema.
Kufuatia hatua hiyo, Gaguti ameelekeza jeshi la polisi kukamilisha taratibu za kipolisi na watuhumiwa kufikishwa haraka kwenye vyombo vya sheria.
Pia ameagiza kufungwa kwa maduka pamoja na maghala ambayo yalihusika katika hujuma hiyo ya kuuza na kuhifadhi viuatilifu ambavyo vimeisha mda wake mpaka pale kesi ya msingi itakapokamilika.
Pia Gaguti amewaomba wananchi wa pamoja na wakulima kuwa waangalifu na kufuatilia kuhakikisha ubora wa viuatilifu na madawa mengine wayanyotumia katika kudhibiti magonjwa ya korosho.
"Ninawaomba wa Mtwara haswa wakulima kuwa macho wanapotafuta viuatiliu na madawa ya mikorosho, wawe makini kuangalia na kufuatilia ubora wa madwa wanayonunua na kutoa taarifa mapeam ili tuweze kukabiliana na uwepo wa madwa feki," amesema.
Viautilifu hivyo vilikamatwa katika maeneo ya Manispaa ya Mtwara Mikindani, Tandahimb, Newala na Nanyumbu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Mark Njera amesema uchunguzi wa awali ulibaini kuwa watuhumiwa hao walitumia mbinu za kuwahadaa wakulima kwa kuwaambia kuwa wameruhusiwa na mamlaka husika kuuza hivyo viuatilifu pamoja na kuwa vimeharibika huku wakiwaambia kuwa havina tatizo.
Pia watuhumiwa hao walitumia barua ambayo walidai wamepewa na mamlaka husika ambazo ziliwapa idhini kuuza hivyo viuatilifu feki pia walitumia nyaraka za kughushi kuonyesha kwamba wamepewa idhini na mamlaka husika kuuza viuatilifu hivyo.
MWANZA FRIENDS WAKUTANA SHINYANGA MJINI KUZINDUA KATIBA ,KUSAKA FURSA ZA UWEKEZAJI
Meneja TTCL Atumbuliwa Kwa Kukwepa Ziara za Viongozi na Kupika Taarifa
Meneja wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wa Mkoa wa Kagera, Irene Shayo ametenguliwa kuanzia Julai 30, 2021 kwa tuhuma za utumishi wake kusuasua na kukwepa ziara za viongozi katika eneo lake
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew amesema pia Meneja huyo amekuwa akipika Taarifa za Mapato na Matumizi
Naibu Waziri amesema Meneja huyo apangiwe majukumu mengine kulingana na wasifu wake kitaaluma ili aweze kufanya kazi vizuri kwasababu majukumu ya sasa hana uwezo nayo
Mwanariadha wa Kenya aondolewa Olimpiki kisa matumizi ya madawa
Japan yakanusha madai kwamba kuna uhusiano kati ya Olimpiki ya Tokyo na ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona
Source
TVMC YATOA ELIMU UKATILI WA KIJINSIA, LISHE MAONESHO YA BIASHARA NA TEKNOLOJIA YA MADINI SHINYANGA
Blinken kuhusu mkataba wa nyuklia wa Iran
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema kuwa mazungumzo ya nyuklia na Iran hayataendelea milele.
Blinken alifanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari na mwenzake Ahmed Nasser es-Sabah huko Kuwait, ambapo alienda kufanya mawasiliano rasmi.
Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliotangazwa kwenye televisheni ya serikali ya Kuwait, Blinken alisema: "Tulikuwa na mazungumzo ya moja kwa moja na Wairani huko Vienna, kuonyesha nia yetu njema na ya kurudi kwenye makubaliano ya nyuklia. Mazungumzo na Iran hayataendelea milele. Mpira sasa upo kwa upande wa Iran na ndio wanaopaswa kufanya uamuzi. "
Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwaiti Sabah alisema kuwa Marekani ilionyesha umuhimu unaozingatia kuhakikisha usalama katika eneo hilo.
Sabah pia alibaini kuwa wanataka kuandaa mkutano wa tano wa mazungumzo ya kimkakati kati ya Kuwait na Marekani.
Mkutano wa kwanza wa Mazungumzo ya Mkakati wa Marekani na Kuwait ulifanyika Washington mnamo 2016 na wa pili mnamo 2018, na wa tatu ulifanyika Kuwait mnamo 2019, na wa nne ulifanyika kupitia video mwaka jana.
Mazungumzo hayo, yaliyokuwa yakiendelea kwa takriban miezi 3 huko Vienna, mji mkuu wa Austria, ambayo vyama vya Ulaya pia vilishiriki, yalikwama baada ya mgombea wa kihafidhina Ebrahim Reisi kushinda uchaguzi wa urais uliofanyika Iran mnamo Juni 19.
Mkuu huyo alisema kuwa Tehran haitakubali makubaliano ya nyuklia isipokuwa vikwazo vya Marekani vitakapoondolewa kikamilifu.
Washington pia ilisema kwamba sharti hili halikubaliki na kuonya kwamba "mazungumzo hayawezi kuendelea kwa muda usiojulikana".
CHUO CHA ROYAL KINATANGAZA NA FASI ZA MASOMO
Chuo cha Royal Training Institute Kilichopo Mbagala Jijini Dar es salaam kinawatangazia nafasi za masomo kwa kozi za mwezi April na Septemba mwaka huu.
Usajili umeanza na Unaendelea chuoni Royal Training Institute.
Chuo kimesajiliwa na NACTE kwa usajili namba REG/HAS/103.
Kozi zinazotolewa na Royal Training Institute ni:-
Ordinary Diploma in Pharmaceutical Sciences(Kozi ya Ufamasia) miaka mitatu. Uwe na Alama D nne zikiwemo Kemia na Baiolojia.
Ordinary Diploma in Pharmaceutical Sciences (In Service) Mwaka 1-uwe umemaliza NTA Level 5
Pia Chuo cha Mafunzo Royal kwa kushirikiana Na Mamlaka ya Elimu ya ufundi (VETA) kingependa kuwajulisha wahitimu wa kidato cha nne kwamba sasa Chuo kinatoa kozi ya msaidizi wa maabara (Certificate in Laboratory Assistants) ngazi ya 1, 2 na 3 Uwe umemaliza kidato Cha nne na kupata cheti muhula utaanza Mwezi wa nne . Wahitimu watafanya kazi kwenye mashule, viwanda na taasisi mbalimbali. Chuo pia kitatoa punguzo kwako na kukusaidia kupata kazi.
Pia chuo Cha Royal Institute kinatoa kozi ya Manunuzi na Ugavi(Procurement & Supply) ngazi ya cheti na Diploma. Uwe na ufaulu wa D 4 katika masomo ya kidato Cha nne.
Kwa Maelezo zaidi wasiliana na chuo Cha Royal kwa namba 0688353310, 0713325507, 0692972523, 0788083484
Au kwa barua pepe pharm_royal@yahoo.com, au tembelea tovuti yetu ya WWW.RTI.AC.TZ.
KUMBUKA KUNA PUNGUZO GHARAMA ZA HOSTELI KWA WALE WATAKAOWAHI..
Vikosi vya Rwanda vyafanya vema Msumbiji
Jeshi la Rwanda lililopelekwa Cabo Delgado nchini Msumbiji limetangaza kufanya vyema kwenye uwanja wa mapigano huku kukiwa na wasiwasi kuhusu kamanda wa kikosi hicho.
Msemaji wa jeshi la Rwanda ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba wanamgambo 14 wameuliwa wiki hii na wanajeshi kutoka Rwanda waliopelekwa Msumbiji.
Ronald Rwivanga amesema operesheni za kijeshi zilizoendeshwa kwenye maeneo ya Mbau na Awese,mkoani Cabo Delgado, baada ya kikosi cha wanajeshi wake kuvamiwa, zilisababisha jumla ya wanamgambo 14 kuuliwa. Rwivanga amesema ni majeraha madogo yaliowapata wanajeshi wa Rwanda kufuatia operesheni hizo.
Mapema mwezi huu, Rwanda ilipeleka kikosi cha wanajeshi na polisi 1,000 nchini Msumbiji kusaidia katika kupamabana na kundi la waasi linaloendesha mashambulizi kaskazini mwa nchi hiyo. Takriban raia laki nane waliyahama makaazi yao kwenye mkoa wa Cabo Delgado na mapigano hayo yalisababisha kampuni ya Mafuta ya Ufaransa ya Total kusitisha mradi wake wa dola bilioni 20 wa kuzalisha gesi asilia kwenye mkoa huo.
Ikiwa kupelekwa kwa kikosi cha wanajeshi wa Rwanda nchini Msumbiji kunalenga kuwasaka wanamgambo wenye itikali kali. Lakini wakosoaji wa serikali ya Rwanda wanaoishi nchini humo wanahofia usalama wao pia. Jenerali Innoncent Kabandana anayeongoza kikosi hicho, ameelezwa na wapinzani kuwa ni mkono wa rais Paul Kagame katika kuwalenga wakosoaji wake.Mtandao wa TheRwandan.com, uliandaka kuwa Meja-jenerali Kabandana alihusika na mauwaji ya maaskofu wa kanisa katoliki wa Gakurazo mwaka 1994 nchini Rwanda na vilevile kuwalenga wakosoaji wa serikali ya Rwanda nchini Marekani na Canada ambako alifanya kazi kama mwambata wa kijeshi katika ubalozi wa Rwanda jijini Washington.
Cleophas Habiyareme, mkuu wa jamii ya wakimbizi wa Rwanda wanaoishi nchini Msumbiji amesema alisoma taarifa pia kwamba kamanda huyo anahusika na kuwalenga wapinzani wanaoishi nje ya nchi. Lakini amesema hilo haliwezi kuwatisha jamii ya wakimbizi wa Rwanda nchini Msumbiji. Habiyareme amesema Msumbiji ni nchi iliyosaini mkataba wa Geneva kwa jili ya kuwapa hifadhi wakimbizi. Amesema halitokuwa jambo la busara kwa kikosi kilicho alikwa kwa shughuli malumu baadae kuanza kuwalenga wakimbizi. Hata hivyo ameiomba serikali ya Msumbiji kuhakikisha usalama wao.
Nchini Msumbiji ambako jenerali Kabandana amepewa majukumu mapya, jamii ya wakimzizi wa Rwanda ni takriban watu 4,000 ambao wamekuwa wakibughudhiwa na kuuliwa miaka ya hivi karibuni. Kisa cha hivi karibuni ni kutoweka bila maelezo yoyote hadi sasa kwa mwandishi habari na mkosoaji wa serikali ya Rwanda Ntamuhanga Cassien aliyekuwa akiishi kwenye kisiwa cha Inhaca,nchini Msumbiji.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Bongo Deco wauzai wa vifaa mbalimbali vya umeme kama TV, Subwoofer, Hometheator, Majiko madogo na makubwa ya Gesi, Friji, Generator nk leo w...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya ...
-
Kuongezeka kwa ghasia za hivi majuzi kumesababisha idadi kubwa ya raia wa Lebanon kukimbia kutoka Beirut huku milipuko ikitikisa jiji hilo...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 15, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekagua ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo – Busisi) ...