Saturday, July 31, 2021

TVMC YATOA ELIMU UKATILI WA KIJINSIA, LISHE MAONESHO YA BIASHARA NA TEKNOLOJIA YA MADINI SHINYANGA


Mratibu wa Miradi wa Shirika lisilo Kiserikali la The Voice of Marginalized Community (TVMC) la Mjini Shinyanga, Mary Mahanya (kulia) akizungumza katika banda la TVMC kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga leo Jumamosi Julai 31,2021.

Shirika la TVMC limeshiriki Maonesho hayo  kwa kuelimisha wananchi kuhusu kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto, kutoa elimu ya masuala ya Lishe zikiwemo njia sahihi za kunyonyesha mtoto na kutoa msaada wa Kisheria  ili kusaidia kutatua migogoro mbalimbali kama vile ya ardhi na ndoa.

Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayoongozwa na kauli mbiu "Uwekezaji wa Madini na Viwanda Shinyanga kwa Uchumi Endelevu" yameanza tarehe 23 Julai, yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 1 Agosti, 2021.

Mratibu wa Miradi wa Shirika lisilo Kiserikali la The Voice of Marginalized Community (TVMC) la Mjini Shinyanga, Mary Mahanya (kulia) akielezea huduma zinazotolewa na TVMC kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
 Afisa Utawala wa Shirika lisilo Kiserikali la The Voice of Marginalized Community (TVMC) la Mjini Shinyanga, Chiku Hamis akionesha kipeperushi kinachoelezea masuala ya Lishe kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
 Afisa Utawala wa Shirika lisilo Kiserikali la The Voice of Marginalized Community (TVMC) la Mjini Shinyanga, Chiku Hamis akionesha kipeperushi kinachoelezea masuala ya Lishe kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...