Mji mkubwa wa Saint Petersburg nchini Urusi umetangaza rikodi ya idadi kubwa ya vifo kutokana na kirusi kipya kinachosambaa kwa haraka cha Delta huku baadhi ya mataifa ya Ulaya yakiondoa vizuizi vya kudhibiti maambukizi licha ya kuenea kwa kasi kwa kirusi hicho.
Wakati hayo yakiarifiwa waziri wa Afya wa Uingereza amejiuzulu baada ya kufichuka kwamba alikiuka taratibu za serikali yake za kudhibiti maambukizi katika mahusiano yake ya kimapenzi na mshirika wake wa karibu. Kampeni za utoaji chanjo zimepunguza maambukizi katika nchi tajiri, lakini kirusi cha Delta kilichogunduliwa kwa mara ya kwanza nchini India kimeibua hofu kwamba janga la corona huenda likachukua muda mrefu kutokomezwa.
Mji mkubwa wa Australia, Sydnea umeanza wiki mbili za vizuizi vya corona kudhibiti ongezeko la ghafla la maambukizi ya kirusi cha Delta. Bangladesh nayo imetangaza itaanzisha vizuizi vipya nchini nzima kuanzia Jumatatu, huku ofisi zikifungwa kwa wiki moja na usafiri unaohusiana na utoaji wa matibabu ukiruhusiwa.
Source