Na Thabiti Madai, Zanzibar.
WAJUMBE wa Mkutano mkuu wa Shirikisho la Soka visiwani Zanzibar (ZFF), wamemchagua Abdul-latif Ali Yassin kuwa Rais mpya wa Shirikisho hilo kwenye uchaguzi uliofanyika jana Jumapili, June 27, 202 kwenye Ukumbi wa Chuo cha Mafunzo, Kilimani Zanzibar.
Abdul-latif ameibuka mshindi kwa kupata kura 16 akimshinda mpinzani wake wa karibu Suleiman Shaaban Suleiman aliyepata kura 8 kati ya kura 24.
Uchaguzi huo ulilazimika kurejewa baada ya awali Abdul-latif kupata kura 11, Suleiman Shaaban Suleiman kura 7, Suleiman Mahmoud Jabir kura 6 huku Tashi na Haji wakiambulia 0, jambo ambalo lilipelekea kurejewa zoezi la kura kwa Wagombea wawili tu walofika idadi kubwa ya kura kutokana na kura hazijavuka nusu ya wajumbe wote na mshindi alitakiwa apate kura kuazia 13 kati ya kura zote 24.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Rais Mteule wa Shirikisho hilo Abdul-Latif Ali Yasin alisema kwamba amegomba nafasi hiyo kutokanakuw ana nia a dhati kabisa ya kushughulikia mpira wa miguu viiwani humo ili kuweza kukua na kuejesha hadhi yake.
"Ndugu zangu wajumbe niliwaeleza katika kipindi cha kampeni na sasa naendelea kuwaeleza kuwa nia ya yngu ni ya kweli, kweli kabisa katika kushughulikia soka La Zanzibar hivyo ofisi zangu zitakuwa zipo wazi kabisa ili kila mmoja aweze kunipatia ushauri wa nini tufanye katka soka letu," alisema.
Aliongeza kwa kuwomba wadau wa michezo visiwani humo kumuunga mkono katika mipango na miakati atakayoianzishaambayo ina lengo la kuinua mpir wa miguu visiwani humo.
Alieleza kuwa, Ili kufikia maendeleo katika mpirawa miguu kama nchi nyingine zilifanikiwa katika sekta hiyo ushirikishwaji kwa wadau ni jambo la msingi ambapo katika uongozi athakikisha kila mdau wa mchezo huo anashirikishwa katika maoni na maamuzi kwa baadhi ya mambo.
Nae Suleimani Shabaani Suleiman ambae ambeta nafasi ya pili katika uchaguzi huo alieleza kwamba, anaheshimu maamuzi yaliyotolewa na wajumbe wa Mkutano ho Mkuu kwa kumchagu Abdul-latif Ali Yasin kuwa Rais mpya hivyo ataungana nae katika harakati ote za kukuza mchezo huo.
"Napenda kuwashukuru wajumbe wa mkutano huu mkuu ila napenda kuwaasa kuwa kila maamuzi yana gharama hivyo napenda kuheshimu maamuzi yenu, mimi ni mdu wa mpira nilikuwepo katika mchezo huu na ntaendelea kuwepo,"alieleza.
Zoezi la Upatikani wa Rais huyo Umeshuhudiwa na Kaimu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo ambae ni Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale,Leila Mohammed Mussa pamoja na Viongozi mbali mbali wa Wizara, Idara na Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF).
Mapema akifungua Mkutano huo wa Uchaguzi, Kaimu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo ambae ni Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanziar Leila Mohammed Mussa liwaasa