Watu 10 wamepoteza maisha katika moto uliotokea katika kituo cha mafuta huko Kabul, mji mkuu wa Afghanistan, jana usiku.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani Tarık Aryen amesema kuwa moto uliozuka jana usiku katika kituo cha mafuta katika mkoa wa Shakardara kaskazini mwa Kabul ulidhibitiwa saa za asubuhi.
Akiripoti kuwa watu 10 walipoteza maisha kwenye moto, Aryen aliongeza kwa kusema kwamba watu 14 walijeruhiwa.
Aryen alibaini kuwa moto, ambao sababu yake bado haijabainika, ulianzia kituo cha mafuta na kusambaa mpaka kwenye tenki za mafuta.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani Aryen amesema kuwa magari na matenki ya mafuta vimeteketea.