Monday, May 3, 2021

Afrika Kusini yapiga marufuku kuzalisha simba na kuwafuga nyumbani





Afrika kusini imeweka wazi mpango wa kuzuia watu kuwazalisha simba majumbani kwa lengo la kuwahifadhi kama wanyama wa nyumbani, kuwavutia watalii ama kuwindwa .

Hatua hiyo imejiri baada ya kuchapishwa kwa matokeo ya uchunguzi wa miaka miwili kuhusu mtindo wenye utata wa baadhi ya watu kuendeleza uzalishaji wa simba ambao wamezuia katika mbuga za binafsi na majumbani .

Iligundulika kwamba mtindo huo ulihatarisha juhudi za uhifadhi wa wanyama hao na pia madhara kwa wafugaji .

Serikali ya Afrika Kusini imekubali mapendekezo ya jopo lililofanya uchunguzi huo hatua ambayo huenda haitawafurahisha wadau katika sekta ya uwindaji.

" Ripoti hiyo inapendekeza kupigwa marufuku kwa mipango ya kuzalisha simba au kuwaweka majumbani ' waziri wa Mazingira Barbara Creecy amesema .

" Hatutaki kuzalishwa kwa simba waliozuiliwa majumbani ,kuwekwa kwao kama wanyama wa nyumbani au matumizi ya wanyama hao kama vivutio vya utalii wakiwa wamzuiliwa .

Hata hivyo amesema kuwindwa kwa simba wa porini kutaruhusiwa kuendelea . Shughuli hiyo huleta pato kubwa la utalii kwani maelfu ya watu husafiri kwenda Afrika Kusini kuwawinda simba wa porini .

Jopo hilo lilipewa jukumu la kutathmini sera za Afrika kusini kusimamia uwindaji wa simba ,chui , ndovu na vifaru.

Kuhusu pembe za vifaru na ndovu, jopo hilo lilipendekeza mazungumzo na nchi nyingine za kusini mwa Afrika kabla ya kuamua ikiwa zinaweza kutolewa.

Takriban simba 8000 wanaaminika kuwa majumbani nchini Afrika Kusini ikilinganishwa na simba 3500 walio msituni .

Wanaounga mkono kuwekwa kwa simba majumbani wanasema ni hatua inayoweza kuwatunza wanyama hao lakini wakosoaji wanadai ni matesi dhidi ya wanyama hao wanaofaa kuwa porini

Shirika la kutetea maslahi ya wanyama World Animal Protection limetaja uamuzi huo wa Afrika kusini kama 'ushindi katika kuwalinda wanyama wa pori'

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...