Rais Samia Suluhu ameadhimisha miaka 57 ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa msamaha kwa wafungwa 5001 waliokuwa na adhabu za vifungo mbalimbali
Kati ya wafungwa 5,001 waliosamehewa 1,516 wameachiwa huru baada ya kupunguziwa robo ya adhabu ya vifungo vyao. 3,495 waliopunguziwa robo ya adhabu zao wataendelea kutumikia vifungo vilivyobaki
Rais Samia amewataka walioachiwa huru kutumia vyema mafunzo waliyoyapata wakiwa jela ili wayatumie katika kujenga taifa kwa kuzingatia sheria