Friday, April 23, 2021

JAJI MSTAAFU DKT. BWANA AHITIMISHA MKUTANO WA TUME YA UTUMISHI WA UMMA … ASEMA WAMETOA UAMUZI WA RUFAA 151 NA MALALAMIKO 11 KUTOKA MAMLAKA ZAO ZA AJIRA NA NIDHAMU

Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma Jaji (Mstaafu) Dkt. Steven J. Bwana akihitimisha Mkutano wa Tume namba 3 kwa mwaka wa fedha 2020/2021 Jijini Dar es Salaam.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Jaji (Mstaafu) Dkt. Steven J. Bwana, leo amehitimisha Mkutano wa Tume namba 3 kwa mwaka wa fedha 2020/2021 uliofanyika Jijini Dar es Salaam.

Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Dkt. Bwana amesema, katika Mkutano huu Tume imetoa uamuzi wa Rufaa 151na Malalamiko 11 yaliyowasilishwa na watumishi mbalimbali wa umma ambao hawakuridhika na uamuzi uliotolewa na Mamlaka zao za Ajira na Mamlaka za Nidhamu.

Kati ya rufaa 151zilizotolewa uamuzi na Tume rufaa 82zimekataliwa; rufaa 43 zimekataliwa kwa kuwa ziliwasilishwa nje ya muda uliowekwa kwa mujibu wa Sheria. Rufaa 12 zimekubaliwa; rufaa 11 zimekubaliwa kwa masharti kwamba zikashughulikiwe upya na Mamlaka zao za Nidhamu kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu. Rufaa 3 hazikutolewa uamuzi kwa sababu ni  kesi zilizopo Mahakamani.

Kwa upande wa malalamiko, Tume ilipokea na kutoa uamuzi wa malalamiko 11 ambapo malalamiko 6 yamekataliwa, malalamiko 4 yamekubaliwa na lalamiko 1 limekataliwa kwa sababu liliwasilishwa nje ya muda. 

Imeandaliwa na:-

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Tume ya Utumishi wa Umma

DAR ES SALAAM

23 Aprili, 2021

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...