Tuesday, March 16, 2021

Museveni amtuhumu Bobi Wine kuiba kura

 

Kwa mara ya kwanza Rais Yoweri Museveni wa Uganda amekituhumu chama cha siasa cha NUP kwa kuhusika na vitendo vya udaganyifu wa wizi wa kura katika zoezi la uchauzi mkuu uliofanyika tarehe 14 January 2021.


Museveni amesema madai ya Kyagulanyi yaani Bobi Wine kwamba ushindi wake katika uchaguzi mkuu ulichukuliwa na rais Museveni na kumutaka kurudisha maamuzi ya wananchi.


Katika hotuba yake usiku wa kuamukia leo rais Museveni amedai kwamba chama cha NUP kilifanya udaganyifu mkubwa katika zoezi la uchaguzi mkuu wa rais na wabunge ndiyo sababu walipata kura hizo hasa katika mkoa wa kati na baadhi ya sehemu za mkoa wa Busoga na kumuonya Kiongozi wa chama cha NUP mipango yake anayopanga kufanya ya maandamano:


"Ni upande wa upinzani hususani kundi la Kyagulanyi ambao walifanya udaganyifu mkubwa kila mtu nchini Uganda anafahamu nani aliyeiba ni kundi la Kyagulanyi, hizo kura wanazodai zaidi ya milioni tatu hazipo, kulikuwa na vitisho vilivyofanywa na wafasi wa NUP" Museveni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...