Tuesday, March 16, 2021

Yanga Wampigia Simu Molinga





INAELEZWA kuwa, uongozi wa Yanga kupitia kwa mwenyekiti wao, Dk Mshindo Msolla na makamu mwenyekiti wa usajili wa timu hiyo, Injinia Hersi Said, wamewasiliana na aliyekuwa mshambulijia wa timu hiyo, David Molinga Falcao' kwa lengo la kutaka kumrudisha msimu ujao.

 

Yanga waliachana na mshambuliaji huyo msimu uliopita akiwa amefunga mabao 12 ndani ya Ligi Kuu Bara ambayo msimu huu mpaka sasa timu hiyo ikicheza mechi 23, hakuna mchezaji wa timu hiyo aliyefikia idadi hiyo.



Kwa sasa kinara wa mabao ndani ya Yanga katika Ligi Kuu Bara ni Deus Kaseke mwenye sita.Kwa mujibu wa taarifa ambazo Spoti Xtra limezipata kutoka ndani ya Yanga, zinadai kuwa Molinga ambaye kwa sasa anakipiga katika Klabu za Zesco United ya nchini Zambia, amepigiwa simu na viongozi hao kwa lengo la kumshawishi akubali kurejea ndani ya kikosi hicho msimu ujao.

 

"Molinga amepigiwa simu na mwenyekiti pamoja na Injinia Hersi na kubwa ni juu ya makubaliano ya yeye kurejea Yanga msimu ujao kwa sababu bado timu imekosa usawa katika eneo la ufungaji.

 

"Lakini inavyoonesha ni kwamba mchezaji mwenyewe amewapa masharti yake ili aweze kurejea kwa sababu uongozi unaona atakuwa msaada kutokana na rekodi ambayo aliiweka wakati anacheza hapa kabla ya kuondoka," alisema mtoa taarifa. Spoti Xtra lilimtafuta Molinga ambaye amekiri kufanya mazungumzo na viongozi wa Yanga, lakini hakuwa tayari kusema ni nini hasa.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...