Tuesday, March 16, 2021

Wachezaji 8 wa Al Merreikh Wakutwa na Corona




Wachezaji nane (8) wa Klabu ya Al Mereikh ya nchini Sudan wamegundulika kuwa na maambukizi ya Virusi vya Corona mara baada ya kufanyiwa vipimo, hivyo wataukosa mchezo wa leo dhidi ya Simba Sc.

 

Wachezaji hao ni Abu Twenty (31), Jamal Salem (27), Bakhit Khamis (33), Abdul Rahman Karnqo (33), Tony (34), Jamaican (35), Ramadan (34), Bakry, Dia Al-Din (30) Jacob (32) na Mohammed Al-Rashid.

 

Mchezo huo wa marudiano wa kundi A la Ligi ya Mabingwa Barani Afrika utapigwa leo jioni katika Dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...