Monday, February 15, 2021

Mwanafunzi Wa Darasa La Sita Akamatwa Akidaiwa Kumnajisi Mwanafunzi Mwenzake

 


Mwanafunzi mwenye umri wa 13 wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Maguja, Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumlawiti mwanafunzi mwenzake wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Likangara.


Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo, Foka Dinya alisema mtuhumiwa anadaiwa kufanya kitendo hicho Februari 5 saa tano mchana.


Alisema kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kumetokana na baba wa mtoto anayedaiwa kufanyiwa kitendo hicho kumbaini kijana wake akiwa amekosa uchangamfu na kutembea kwa shida.


Dinya Alisema mtoto huyo alipouliza akaeleza kile alichofanyiwa na mwenzake.


Alisema kutokana na maelezo ya baba wa mlalamikaji, alilazimika kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi kisha mtuhumiwa akakamatwa na kufanyiwa mahojiano.


Alisema mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani baada ya kukamilika kwa taratibu za kiupelelezi.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...