Kupitia Instagram yake ameandika hivi: "Sijasahau nilikotoka, mengi niliyokuwa naota niliambiwa hayawezekani. Siwalaumu walionikatisha tamaa au kunidharau, hayakuwa makosa yao kwani ni kweli sikuwa naonesha dalili kwamba ningefika hapa. Sikuziacha ndoto zangu, sijawahi kuacha kutembea kwenye mchoro uliokuwa kichwani mwangu licha ya ukweli kwamba hata mimi kuna wakati nilikuwa naogopa na kuhisi kwamba labda nina wazimu.
LEO NIKO HAPA : Sijui namna sahihi ya kumshukuru Mungu wangu. Ile ndoto ya kijana wa kijijini, iliyotafutwa mtaani, ile ndoto iliyokuwa kwenye meza ya DJ wa kupiga kwenye vigodoro na harusi, yule aliyepata tabu kuajiriwa kwenye redio, yule waliyemsema kwa maneno mengi sana kila mtu akiwa na stori yake IMEKUWA KWELI.
.
@efmtanzania ni redio iliyoanzia chini kabisa kwenye kaofisi kadogo (hatukuanza na ile K-Net house yote, tulichukua sehemu ndogo sana), tumepanda mdogo mdogo katika lugha na mtindo wetu : NAMSHUKURU MUNGU NIMEKAMILISHA UJENZI WA JENGO LETU WENYEWE. Bila shaka yoyote tunakuwa media house inayomiliki jengo kali zaidi. Niseme nini?
.
Namshukuru Mungu na kila mtu aliyehusika kwenye safari yangu. Asante Serikali yangu, Nawashukuru mno wasikilizaji wetu, watazamaji na washirika wetu katika biashara.
Zaidi sana WAFANYAKAZI WENZANGU wa @tvetanzania na @efmtanzania, nawashukuru kwa kujitoa kwao na kufanya kazi kwa weledi mkubwa hata katika mazingira magumu : WE MADE IT GUYS, #HatupoiHatuboi.
.
DEDICATION : Jengo hili ni kwa ajili ya vijana Kitanzania, wale wa uswahilini na wote kutoka familia za kimaskini waliojaa ndoto. Naomba mlitazame jengo hili na mfahamu kwamba inawezekana : UNAWEZA KUWA MAJIZZO. Usisikilize kelele, usitoke kwenye mstari.
.
I am out of words : #MuzikiUnaongea