Monday, February 15, 2021

Jokate awatolea uvivu wanaotumia jina lake kutapeli mtandaoni

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani Jokate Mwegelo amesema anasikitishwa na tabia ya baadhi ya watu wanaotumia jina lake kuwatapeli wananchi fedha zao huku akivitaka vyombo vya ulinzi na usalama na hasa Jeshi la Polisi nchini kupitia kitengo chake cha kukabili uhalifu mtandaoni kuchukua hatua dhidi ya watu hao.

Amesema ni kwa muda mrefu sasa amekuwa akipokea malalamiko kutoka kwa wananchi mbalimbali ambao wamekuwa wakichukuliwa fedha zao kwa njia hiyo ya utapeli kwenye mitandao ambapo kuna watu wamekuwa wakifungua akaunti zisizo rasmi(akaunti feki) kwa kuwaaminisha wananchi kuwa ni yeye na kuchukua fedha.

"Nimewaita ndugu zangu waandishi wa habari kuzungumza nanyi leo, ili mfikishe ujumbe huu kwa Watanzania,kuna watu wanatumia vibaya majina ya viongozi na watu mashuhuri ili kurubuni na kutapeli watu mbalimbali, binafsi kuna kikundi cha watu ambacho kimekuwa kikitumia jina langu na picha zangu wanafungua akaunti feki" Jokate

"wanaongea na umma wa Watanzania wakijifanya kama mimi, huko nyuma nimewahi kuzungumzia hili, kuna watu wanafungua akaunti mtandaoni, wanawapa watu namba za simu na wanawaambia kuna mikopo inapatikana wilaya ya Kisarawe ambayo inatolewa na Mkuu wa wilaya Jokate Mwegelo, na wakishawapa namba ya simu wanaingia Whatsap wakiwarubuni kwa kutumia ujanja ujanja" Jokate


"Na watu hao wakishapigiwa wanaamini wanaongea na mimi, binafsi naomba niwaambie umma wa Watanzania , mimi sina huduma yoyote ya kutoa mikopo, nimeliweka wazi kwenye kurasa zangu rasmi ambazo ninazitumia kwenye mitandao ya kijamii lakini bado linaendelea, narudia tena kuwaambia, sifanyi kazi ya kutoa mkopo wala huduma yoyote ya mkopo, sijawahi kufanya, sijafanya na wala sitafanya kwa siku za hivi karibuni hiyo huduma ya kutoa mikopo," Jokate.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...