Monday, February 15, 2021

Harmonize amfariji Kajala "kuwa imara, nifanye nijivune mpenzi wangu wa maisha"






Baada ya sakata la kuvuja kwa video isiyo na maadili ya mtoto wa msanii Kajala Masanja, anayefahamika kwa jina la #Paula, Harmonize ampa moyo msanii huyo ambaye ni mpenzi wake mpya.
Kajala ambaye ni msanii wa filamu, tunaweza sema jana Jumapili Februari 14, 2021 Valentine yake iliingia doa baada ya video hiyo mbaya kuvuja na kugeuka kuwa gumzo mtandaoni.

Video hiyo isiyo na maadili inamuonyesha mtoto huyo wa Kajala akiwa kwenye gari na msanii kutoka lebo ya WCB, Rayvanny.

Licha ya mwenyewe kuelekeza tuhuma za aliyesababisha hayo yote kuwa ni mrembo Hamisa Mobeto, Mobeto naye jana hiyo hiyo alichomoa kwa kuandika utetezi mrefu kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Hata hivyo katika siku hiyo ya wapendanao ni kama #Harmonize amempa moyo kwa magumu anayoyapitia mpenzi wake huyo kwa kumuandikia ujumbe mtamu.

"Heri ya siku ya wapendanao mpenzi wangu wa maisha, kuwa imara, nifanye nijivune," aliandika Harmonize.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...