Monday, November 18, 2019
Mkutano wa Taasisi za fedha nchini wahamishiwa Dar
Mkutano wa 19 wa taasisi za fedha nchini uliokuwa ufanyike jijini Arusha tarehe 21 na 22 Novemba 2019 sasa utafanyika Dar es Salaam kwa tarehe hizo hizo.
Mkutano huo ambao umeandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania kwa kushirikiana na Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA) utawakutanisha washiriki wapatao 300 ili kujadili namna ya kuharakisha maendeleo ya ya sekta ya fedha nchini. Watakaohudhuria mkutano huo ni pamoja an mawaziri wakiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, wakuu wa taasisi za fedha, wachumi wabobezi, wanataaluma na washirika mbalimbali wa maendeleo.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano huo na Mkurugenzi wa Utumishi na Uendeshaji wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Kened Nyoni, alisema mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.
Mada katika mkutano huo zitahusu 'Matumizi ya teknolojia katika kukuza sekta ya fedha ili kuleta mapinduzi ya viwanda'; 'Maeneo yenye fursa za uwekezaji katika sekta ya fedha', 'Vigezo vinavyochangia kujenga tabia za ukopaji', 'Jinsi ya kukinga vihatarishi katika sekta ya fedha'; 'Namna ya kuoanisha sekta ya fedha na maendeleo ya viwanda'; na 'Tathmini ya mchango wa sekta ya benki katika huduma jumuishi za kifedha nchini'.
Benki Kuu ya Tanzania imekuwa ikiandaa mikutano ya taasisi za fedha kila baada ya miaka miwili tangu miaka ya 1980. Katika mikutano hii, viongozi wakuu wa taasisi za fedha, yakiwemo mabenki, mashirika ya bima, mifuko ya hifadhi za jamii na taasisi zingine za fedha wamekuwa wakikutana na kujadili masuala mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya fedha na uchumi wa nchi kwa ujumla. Mkutano wa 18 wa taasisi za fedha ulifanyika mwaka 2016 jijini Arusha na mada kuu katika mkutano huo ilikuwa ni 'Jinsi sekta ya fedha inavyoweza kuifanya Tanzania inufaike kiuchumi kutokana na uwepo wake kijiografia' (Harnessing Tanzania's Geographical Advantage: The role of financial sector).
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali shauri lililokuwa limefunguliwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...